Tatizo la Tanzania halikuwa ujamaa wala vita vya Kagera bali ombwe la uongozi

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,784
Watanzania huwa tunapenda majibu marahisi kwenye maswali magumu.

Huwa tunapenda kusingizia haya yafuatayo kwenye umasikini wetu, hasahasa anguko na mdororo wa uchumi wa miaka ya 80's hadi 90's:

1. VITA VYA KAGERA,
2. UJAMAA,
3. HUJUMA ZA KIBEPARI,
4. ANGUKO LA UCHUMI WA DUNIA MIAKA YA 70's
5. UKAME WA MIAKA YA 70'S.

Huwa hatuzingatii kwamba aina ya uongozi ambao ulikuwepo Tanzania ndiyo umechangia na unazidi kuchangia nchi kudidimia. Hebu tuilinganishe Tanzania na Ethiopia, nchi ambazo zote zimewahi kutawaliwa na Wajamaa, zimewahi kupigana Vita za uvamizi, na zimewahi kukumbwa na ukame na njaa. Ukimaliza utafahamu kwamba mbali na matatizo yote, Ethiopia wametuacha sisi mbali sana (In terms of GDP) na kuwakuta inahitaji hatua za ziada.

Hebu tuzingatia haya yafuatayo:

Mosi
, kama tatizo ni Ujamaa, nchi kama Ethiopia walikuwa wajamaa na wakomunisti kuliko sisi, lakini leo hii wametupita mbali sana kiuchumi. Wenzetu walitawaliwa na Military Junta, The Derg chini ya Waziri Mkuu Mengitsu ambaye aliingia madarakani kwa fujo na kutawala kwa mkono wa chuma. Aliaua maelfu ya raia, huku akiiga ukatili wa wasovieti na wachina, ambao walitumia kampeni za RED TERROR kuhakikisha ukomunisti unaendelea kutawala. Huku Tanzania haya mambo hayakuwepo, ila wenzetu wakatuacha.

Pili, kama tatizo ni Vita, nchi ya Ethiopia imepigana vita kubwa na za muda mrefu zilizoua maelfu ya watu kuliko. Vita ya Ogaden, ambayo Ethiopia alipambana na Somalia, ilikuwa ni kubwa kuliko ile ya Kagera. Jumla ya vifaru vilivyotumika na Ethiopia vilikuwa siyo chini ya 300, pamoja na mizinga ya kisasa, huku wakisaidiwa na maelfu ya wanajeshi wa Cuba ambao ilibidi wale, wavae na wapewe silaha. Makadario yanasema kwamba Ethiopia alitumia zaidi ya trilioni saba za kitanzania. Kule Kagera makadirio yanasema kwamba ilitumika Trilioni moja hadi Mbili. Nachoshangaa mpaka sasa, mbali na gharama kubwa ya vita, Ethiopia wako mbele yetu kiuchumi.

Mbali na hapo, Ethiopia ni nchi ambayo haijawahi kuwa na Amani na Utulivu kama Tanzania. Nchi imejaa ukabila mkali mno. Wao wamekuwa kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe tokea mwaka 1974 hadi 1971. (The Ethiopian Civil War), lakini mbali na hayo yote walishika madaraka kina Meres Zenawi, nchi ilipiga hatua zisizo za kawaida.

Tatu, kama tatizo ni Ukame, nchi ya Ethiopia ilikumbwa na ukame uliopelekea baa kubwa la njaa tokea mwaka 1983-1985 ambapo, watu zaidi ya milioni saba wa Ethiopia waliathirika. UN wanasema kwamba, njaa ile ilitengeneza mayatima laki mbili, huku mamilioni wakigeuka wakimbizi. Wataalamu wa kitanzania hupenda kusema kwamba ukame wa miaka ya 70's ulichangia kudorora kwa uchumi, lakini husahau kwamba nchi kama Ethiopia ilikuwa na janga kubwa kuliko letu ila leo wametupita uchumi.

============================================================
Ndugu zangu simkashifu Mzee Nyerere, wala watanzania ila ukweli mchungu ni kwamba kuna namna alitawala ndivyo sivyo. Ukitoa ufisadi na tamaa za mali, ambavyo Mzee hakuwa navyo kabisa, tabia nyingine mbaya ambazo CCM wanazo leo walizitoa kwa Mzee Nyerere. Mfano, kupenda kufanya siasa kwenye utaalamu, tabia za umwinyi usio na mantiki, kutokukubali kwamba umekosea na kukosolewa, n.k

Niwape mfano kuhusu Dikteta Mengitsu wa Ethiopia, alivyolijenga shirika la ndege ambalo ni moja ya mashirika bora kabisa barani Afrika. Mengitsu alikuwa ni mkomunisti kwelikweli, basi Shirika la ndege la Ethiopia wakataka kununua ndege. Wajamaa kama kawaida yao, wakashauri aende akanunue ndege za Mrusi, Antonov na Tupolev kwa wajamaa wenzake. Ila wataalamu walimkatalia wakamshauri asifanye hivyo maana kuchanganya ndege kutazua matatizo kiutalaamu.

Mengitsu alikubaliana na ushauri wa wataalamu, japo kishingo upande na kununua ndege za Marekani ambazo mainjinia wengi walikuwa na utaalamu nazo. Ila kubwa zaidi, alishauriwa kabisa asiruhusu wanasiasa hasahasa wale wajamaa waingilie utendaji kazi wa shirika la ndege. Hivyo Ethiopian Airlines likawa shirika linalojitegemea lenyewe (Fully Autonomous), bila kuingiliwa na wanasiasa.

Kuna waziri akajichanganya kusema anataka kuingilia utendaji wa shirika. Mengitsu alichokifanya ni kumchukua na kwenda kumpiga risasi hadharani. Tokea pale, wanasiasa hasahasa wajamaa wapenda porojo hawakuwahi kusogelea kabisa lile shirika na ndiyo ikawa ponapona yake hadi leo. Nigeria aliwahi kuwa na ndege nyingi na za kisasa kuliko Ethiopia, lakini shirika lake halifanya vizuri. Tatizo ni porojo na siasa, halafu utaalamu pembeni.

Tanzania tulifuta taasisi zenye nguvu za kilimo, (Cooperatives) kwa kigezo cha kuondoa ukabila na ukanda na mwishowe tukaua kilimo. Leo hii Tanzania, sheria inampa waziri mwanasiasa, asiye na utaalamu wowote ule, nguvu ya kuiamulia (Giving Directives) bodi ya wataalamu, pamoja na kuchagua wanabodi anapotaka yeye. Mambo yakienda kombo tunalalamika. Mfumo wa hii nchi umekaa vibaya mno, kuwapa nguvu wanasiasa kuliko wataalamu, hili alilitengeneza Mzee Nyerere, lakini halikuwa sahihi kabisa.
 
Tanzania 🇹🇿 hakuna watu, kuna mijitu ya hovyo.
Tukumbushane tu, ili tuendelee tunahitaji ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora.

Taasisi watu hamna, hivyo kamwe hatuwezi kupata siasa safi wala uongozi bora na milele hatutaendelea.

Soma Isaya 50:11
 
Nakubaliana kabisa na wewe. Kuna siku huwa najiuliza, hivi inakuwaje watanzania kuvumilia aina hii ya ujinga bila hata kustuka akili kidogo ?
 
Kinachosikitisha maji ya mvua yanatiririka baharini,mkulima anasubiri kudra za mwenyezi mungu.
FB_IMG_1654103401853.jpg
 
N
Watanzania huwa tunapenda majibu marahisi kwenye maswali magumu.

Huwa tunapenda kusingizia haya yafuatayo kwenye umasikini wetu, hasahasa anguko na mdororo wa uchumi wa miaka ya 80's hadi 90's:

1. VITA VYA KAGERA,
2. UJAMAA,
3. HUJUMA ZA KIBEPARI,
4. ANGUKO LA UCHUMI WA DUNIA MIAKA YA 70's
5. UKAME WA MIAKA YA 70'S.

Huwa hatuzingatii kwamba aina ya uongozi ambao ulikuwepo Tanzania ndiyo umechangia na unazidi kuchangia nchi kudidimia. Hebu tuilinganishe Tanzania na Ethiopia, nchi ambazo zote zimewahi kutawaliwa na Wajamaa, zimewahi kupigana Vita za uvamizi, na zimewahi kukumbwa na ukame na njaa. Ukimaliza utafahamu kwamba mbali na matatizo yote, Ethiopia wametuacha sisi mbali sana (In terms of GDP) na kuwakuta inahitaji hatua za ziada.

Hebu tuzingatia haya yafuatayo:

Mosi, kama tatizo ni Ujamaa, nchi kama Ethiopia walikuwa wajamaa na wakomunisti kuliko sisi, lakini leo hii wametupita mbali sana kiuchumi. Wenzetu walitawaliwa na Military Junta, The Derg chini ya Waziri Mkuu Mengitsu ambaye aliingia madarakani kwa fujo na kutawala kwa mkono wa chuma. Aliaua maelfu ya raia, huku akiiga ukatili wa wasovieti na wachina, ambao walitumia kampeni za RED TERROR kuhakikisha ukomunisti unaendelea kutawala. Huku Tanzania haya mambo hayakuwepo, ila wenzetu wakatuacha.

Pili, kama tatizo ni Vita, nchi ya Ethiopia imepigana vita kubwa na za muda mrefu zilizoua maelfu ya watu kuliko. Vita ya Ogaden, ambayo Ethiopia alipambana na Somalia, ilikuwa ni kubwa kuliko ile ya Kagera. Jumla ya vifaru vilivyotumika na Ethiopia vilikuwa siyo chini ya 300, pamoja na mizinga ya kisasa, huku wakisaidiwa na maelfu ya wanajeshi wa Cuba ambao ilibidi wale, wavae na wapewe silaha. Makadario yanasema kwamba Ethiopia alitumia zaidi ya trilioni saba za kitanzania. Kule Kagera makadirio yanasema kwamba ilitumika Trilioni moja hadi Mbili. Nachoshangaa mpaka sasa, mbali na gharama kubwa ya vita, Ethiopia wako mbele yetu kiuchumi.

Mbali na hapo, Ethiopia ni nchi ambayo haijawahi kuwa na Amani na Utulivu kama Tanzania. Nchi imejaa ukabila mkali mno. Wao wamekuwa kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe tokea mwaka 1974 hadi 1971. (The Ethiopian Civil War), lakini mbali na hayo yote walishika madaraka kina Meres Zenawi, nchi ilipiga hatua zisizo za kawaida.

Tatu, kama tatizo ni Ukame, nchi ya Ethiopia ilikumbwa na ukame uliopelekea baa kubwa la njaa tokea mwaka 1983-1985 ambapo, watu zaidi ya milioni saba wa Ethiopia waliathirika. UN wanasema kwamba, njaa ile ilitengeneza mayatima laki mbili, huku mamilioni wakigeuka wakimbizi. Wataalamu wa kitanzania hupenda kusema kwamba ukame wa miaka ya 70's ulichangia kudorora kwa uchumi, lakini husahau kwamba nchi kama Ethiopia ilikuwa na janga kubwa kuliko letu ila leo wametupita uchumi.

============================================================
Ndugu zangu simkashifu Mzee Nyerere, wala watanzania ila ukweli mchungu ni kwamba kuna namna alitawala ndivyo sivyo. Ukitoa ufisadi na tamaa za mali, ambavyo Mzee hakuwa navyo kabisa, tabia nyingine mbaya ambazo CCM wanazo leo walizitoa kwa Mzee Nyerere. Mfano, kupenda kufanya siasa kwenye utaalamu, tabia za umwinyi usio na mantiki, kutokukubali kwamba umekosea na kukosolewa, n.k

Niwape mfano kuhusu Dikteta Mengitsu wa Ethiopia, alivyolijenga shirika la ndege ambalo ni moja ya mashirika bora kabisa barani Afrika. Mengitsu alikuwa ni mkomunisti kwelikweli, basi Shirika la ndege la Ethiopia wakataka kununua ndege. Wajamaa kama kawaida yao, wakashauri aende akanunue ndege za Mrusi, Antonov na Tupolev kwa wajamaa wenzake. Ila wataalamu walimkatalia wakamshauri asifanye hivyo maana kuchanganya ndege kutazua matatizo kiutalaamu.

Mengitsu alikubaliana na ushauri wa wataalamu, japo kishingo upande na kununua ndege za Marekani ambazo mainjinia wengi walikuwa na utaalamu nazo. Ila kubwa zaidi, alishauriwa kabisa asiruhusu wanasiasa hasahasa wale wajamaa waingilie utendaji kazi wa shirika la ndege. Hivyo Ethiopian Airlines likawa shirika linalojitegemea lenyewe (Fully Autonomous), bila kuingiliwa na wanasiasa.

Kuna waziri akajichanganya kusema anataka kuingilia utendaji wa shirika. Mengitsu alichokifanya ni kumchukua na kwenda kumpiga risasi hadharani. Tokea pale, wanasiasa hasahasa wajamaa wapenda porojo hawakuwahi kusogelea kabisa lile shirika na ndiyo ikawa ponapona yake hadi leo. Nigeria aliwahi kuwa na ndege nyingi na za kisasa kuliko Ethiopia, lakini shirika lake halifanya vizuri. Tatizo ni porojo na siasa, halafu utaalamu pembeni.

Tanzania tulifuta taasisi zenye nguvu za kilimo, (Cooperative Union) kwa kigezo cha kuondoa ukabila na ukanda na mwishowe tukaua kilimo. Leo hii Tanzania, sheria inampa waziri mwanasiasa, asiye na utaalamu wowote ule, nguvu ya kuiamulia (Giving Directives) bodi ya wataalamu, pamoja na kuchagua wanabodi anapotaka yeye. Mambo yakienda kombo tunalalamika. Mfumo wa hii nchi umekaa vibaya mno, kuwapa nguvu wanasiasa kuliko wataalamu, hili alilitengeneza Mzee Nyerere, lakini halikuwa sahihi kabisa.
Nimependa ulivyomaliza.

Huwezi kuwapa nguvu wanasiasa kuliko wataalam alafu ukabaki salama. Shida ya hii nchi ni wanasiasa na tutakabyoweza kuwabana ndo itakuwa toka yetu kiuchumi
 
Ethiopia ni nchi Masikini kuliko Tanzania, bado inapewa msaada mkubwa wa chakula na West. GDP per capita yao ni ndogo sana, ndogo kuliko hata ya Tanzania.
 
Ukipewa madaraka unaanza kujaza mfuko wako, na ukijaa huridhika, unakula mpaka unajitapikia. Tutaendelea lini? Ukicheki kwa makini utagundua kuwa kuna sehemu ambayo akili ndogo inaongoza akili kubwa. Tuwe na uzalendo ila tujitahidi ili "akili kubwa (yenye uzalendo) iongoze akili ndogo.
 
Watanzania huwa tunapenda majibu marahisi kwenye maswali magumu.

Huwa tunapenda kusingizia haya yafuatayo kwenye umasikini wetu, hasahasa anguko na mdororo wa uchumi wa miaka ya 80's hadi 90's:

1. VITA VYA KAGERA,
2. UJAMAA,
3. HUJUMA ZA KIBEPARI,
4. ANGUKO LA UCHUMI WA DUNIA MIAKA YA 70's
5. UKAME WA MIAKA YA 70'S.

Huwa hatuzingatii kwamba aina ya uongozi ambao ulikuwepo Tanzania ndiyo umechangia na unazidi kuchangia nchi kudidimia. Hebu tuilinganishe Tanzania na Ethiopia, nchi ambazo zote zimewahi kutawaliwa na Wajamaa, zimewahi kupigana Vita za uvamizi, na zimewahi kukumbwa na ukame na njaa. Ukimaliza utafahamu kwamba mbali na matatizo yote, Ethiopia wametuacha sisi mbali sana (In terms of GDP) na kuwakuta inahitaji hatua za ziada.

Hebu tuzingatia haya yafuatayo:

Mosi, kama tatizo ni Ujamaa, nchi kama Ethiopia walikuwa wajamaa na wakomunisti kuliko sisi, lakini leo hii wametupita mbali sana kiuchumi. Wenzetu walitawaliwa na Military Junta, The Derg chini ya Waziri Mkuu Mengitsu ambaye aliingia madarakani kwa fujo na kutawala kwa mkono wa chuma. Aliaua maelfu ya raia, huku akiiga ukatili wa wasovieti na wachina, ambao walitumia kampeni za RED TERROR kuhakikisha ukomunisti unaendelea kutawala. Huku Tanzania haya mambo hayakuwepo, ila wenzetu wakatuacha.

Pili, kama tatizo ni Vita, nchi ya Ethiopia imepigana vita kubwa na za muda mrefu zilizoua maelfu ya watu kuliko. Vita ya Ogaden, ambayo Ethiopia alipambana na Somalia, ilikuwa ni kubwa kuliko ile ya Kagera. Jumla ya vifaru vilivyotumika na Ethiopia vilikuwa siyo chini ya 300, pamoja na mizinga ya kisasa, huku wakisaidiwa na maelfu ya wanajeshi wa Cuba ambao ilibidi wale, wavae na wapewe silaha. Makadario yanasema kwamba Ethiopia alitumia zaidi ya trilioni saba za kitanzania. Kule Kagera makadirio yanasema kwamba ilitumika Trilioni moja hadi Mbili. Nachoshangaa mpaka sasa, mbali na gharama kubwa ya vita, Ethiopia wako mbele yetu kiuchumi.

Mbali na hapo, Ethiopia ni nchi ambayo haijawahi kuwa na Amani na Utulivu kama Tanzania. Nchi imejaa ukabila mkali mno. Wao wamekuwa kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe tokea mwaka 1974 hadi 1971. (The Ethiopian Civil War), lakini mbali na hayo yote walishika madaraka kina Meres Zenawi, nchi ilipiga hatua zisizo za kawaida.

Tatu, kama tatizo ni Ukame, nchi ya Ethiopia ilikumbwa na ukame uliopelekea baa kubwa la njaa tokea mwaka 1983-1985 ambapo, watu zaidi ya milioni saba wa Ethiopia waliathirika. UN wanasema kwamba, njaa ile ilitengeneza mayatima laki mbili, huku mamilioni wakigeuka wakimbizi. Wataalamu wa kitanzania hupenda kusema kwamba ukame wa miaka ya 70's ulichangia kudorora kwa uchumi, lakini husahau kwamba nchi kama Ethiopia ilikuwa na janga kubwa kuliko letu ila leo wametupita uchumi.

============================================================
Ndugu zangu simkashifu Mzee Nyerere, wala watanzania ila ukweli mchungu ni kwamba kuna namna alitawala ndivyo sivyo. Ukitoa ufisadi na tamaa za mali, ambavyo Mzee hakuwa navyo kabisa, tabia nyingine mbaya ambazo CCM wanazo leo walizitoa kwa Mzee Nyerere. Mfano, kupenda kufanya siasa kwenye utaalamu, tabia za umwinyi usio na mantiki, kutokukubali kwamba umekosea na kukosolewa, n.k

Niwape mfano kuhusu Dikteta Mengitsu wa Ethiopia, alivyolijenga shirika la ndege ambalo ni moja ya mashirika bora kabisa barani Afrika. Mengitsu alikuwa ni mkomunisti kwelikweli, basi Shirika la ndege la Ethiopia wakataka kununua ndege. Wajamaa kama kawaida yao, wakashauri aende akanunue ndege za Mrusi, Antonov na Tupolev kwa wajamaa wenzake. Ila wataalamu walimkatalia wakamshauri asifanye hivyo maana kuchanganya ndege kutazua matatizo kiutalaamu.

Mengitsu alikubaliana na ushauri wa wataalamu, japo kishingo upande na kununua ndege za Marekani ambazo mainjinia wengi walikuwa na utaalamu nazo. Ila kubwa zaidi, alishauriwa kabisa asiruhusu wanasiasa hasahasa wale wajamaa waingilie utendaji kazi wa shirika la ndege. Hivyo Ethiopian Airlines likawa shirika linalojitegemea lenyewe (Fully Autonomous), bila kuingiliwa na wanasiasa.

Kuna waziri akajichanganya kusema anataka kuingilia utendaji wa shirika. Mengitsu alichokifanya ni kumchukua na kwenda kumpiga risasi hadharani. Tokea pale, wanasiasa hasahasa wajamaa wapenda porojo hawakuwahi kusogelea kabisa lile shirika na ndiyo ikawa ponapona yake hadi leo. Nigeria aliwahi kuwa na ndege nyingi na za kisasa kuliko Ethiopia, lakini shirika lake halifanya vizuri. Tatizo ni porojo na siasa, halafu utaalamu pembeni.

Tanzania tulifuta taasisi zenye nguvu za kilimo, (Cooperatives) kwa kigezo cha kuondoa ukabila na ukanda na mwishowe tukaua kilimo. Leo hii Tanzania, sheria inampa waziri mwanasiasa, asiye na utaalamu wowote ule, nguvu ya kuiamulia (Giving Directives) bodi ya wataalamu, pamoja na kuchagua wanabodi anapotaka yeye. Mambo yakienda kombo tunalalamika. Mfumo wa hii nchi umekaa vibaya mno, kuwapa nguvu wanasiasa kuliko wataalamu, hili alilitengeneza Mzee Nyerere, lakini halikuwa sahihi kabisa.
Yeah! Huu ndio mfumo unaotugharimu hadi Sasa.
 
Back
Top Bottom