Tatizo la kununua Umeme wa LUKU: Waziri Kalemani amsimamisha kazi kwa siku 10 Meneja wa TEHAMA wa TANESCO

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Waziri wa Nishati, Medard Kalemani amewasimamisha kazi kwa siku 10 Meneja wa TEHAMA na Huduma za Biashara wa TANESCO, Lonus Feruzi na wasaidizi wake Frank Mushi na Idda Nja.

Ametaka watoe maelezo ya tatizo la mifumo ya LUKU, na kuagiza maelezo yao yasipojitosheleza waondolewe kazini.

==
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amemsimamisha kazi kwa siku kumi Meneja wa Tehama na huduma za biashara wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Lonus Feruzi na wasaidizi wake Frank Mushi na Idda Njau, ili watoe maelezo kufuatia kuwepo kwa tatizo katika huduma ya manunuzi ya LUKU kupitia njia za Kielekroniki.

Dkt. Kalemani amewaambia Waandishi wa habari mkoani Dar es salaam kuwa, endapo maelezo yao hayatajitosheleza Watumishi hao waondolewe kazini.

Kwa muda wa takribani siku tatu, wateja wa TANESCO wameshindwa kununua umeme wa LUKU kwa njia.ya Kielekroniki, na hivyo kulilazimu shirika hilo kuwaelekeza Wateja wake kununua umeme kwenye ofisi zake za mikoa na wilaya katika maeneo mbalimbali nchini.
 
Wafanyakazi watatu wamesimamishwa kazi kwa kushindwa kutatua tatizo la LUKU na waziri mwenye dhamana. Waziri amemuagiza Mkurugenzi Mkuu kuutangazia umma kurejea kwa huduma ya LUKU saa 8 mchana leo
Mbona umekimbia Sana mkuu lete picha tuone
 
Wafanyakazi watatu wamesimamishwa kazi kwa kushindwa kutatua tatizo la LUKU na waziri mwenye dhamana. Waziri amemuagiza Mkurugenzi Mkuu kuutangazia umma kurejea kwa huduma ya LUKU saa 8 mchana leo
Sasa Ni saa nane na dkk saba
 
Waziri wa Nishati, Medard Kalemani amewasimamisha kazi kwa siku 10 Meneja wa ICT na Huduma za Biashara wa TANESCO, Lonus Feruzi na wasaidizi wake Frank Mushi na Idda Njau ili watoe maelezo ya tatizo la mifumo ya LUKU, na kuagiza maelezo yao yasipojitosheleza waondolewe kazini. https://t.co/BefGpxaVpI
20210519_140832.jpg
 
Back
Top Bottom