teac kapex
JF-Expert Member
- Jan 23, 2011
- 470
- 136
Habari za leo wadau wa jukwaa hili, leo kwa bahati mbaya nimechanganya mafuta, nina gari aina ya hiace ambayo inatumia Petroli, nimekwenda kituo cha mafuta muuzaji bila kuuliza akashindilia diesel kama lita 4 hivi na ndani ya tank kulikuwa kama na lita 7 za petroli nilipoondoka tu umbali usiozidi mita 50 gari ikaanza kuwa na miss na kwa kweli imenigharimu sana maana nimelazimika kutumia mafuta mengi kwa umbali mfupi, na hadi sasa miss ni kubwa sana, sasa naomba ushauri wenu nifanye nini kuiondoa? Nb kumbuka kwa nimejitahidi kuongeza mafuta mengine kama ya sh 40,000 lakini hakuna mafanikio. MSAADA TAFADHALI