Tatizo la pikipiki kutumia mafuta mengi kuliko kawaida

Udochi

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
761
1,006
Wataalam,
Pikipiki yangu ni ndogo aina ya Sinoray 110, Full tank mafuta ni Lita tatu (3) tu.

Nilipoinunua ikiwa mpya nilikuwa naitumia hadi siku 6 kwa mizunguko yangu ya kwenda kazini na kurudi nyumbani.

Ni miaka miwili imepita sasa, ila kwa Sasa Lita zilezile 3, nazitumia siku 3 tu kwa mizunguko ileile.

Tatizo linaweza kuwa ni nini hapa wataalam?
 
Kagua spark plug kama inachoma vizuri, Ignition wire hakikisha umeifunika na supressor hapo kwenye plug.

Air cleaner umewahi kubadili au unasafisha kila muda gani, pia mkague carburetor kama ipo sawa na kuisafisha.
 
Kagua air cleqner , bearings , na uangalie tryre rolling resistance , kuna uwezekano unatumia matairi mazito
 
Kama umewahi badili piston rings, fundi wako alitakiwa akague na valve ya outlet na inlet hata kama akikuta zipo vizuri asifunge kabla ya kuzigrind(kusaga) tena.

Pia adjustmest ya tarpet inaweza ikawa sababu, kama zimelegea sana au kukaza sana maana zinahusika kwenye ufunguaji wa inlet& outlet valve
 
  • Thanks
Reactions: PYD
Back
Top Bottom