Tathmini ya siasa za CHADEMA mara baada ya kuruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa

system hacker

JF-Expert Member
Mar 13, 2022
426
706
Kwa kifupi bado wapo hai sana tofauti na ilivyotegemewa.

Ila wanachama wao wamechoka sana. Wengine wamekata tamaa kabisa na kuachana na siasa, lakini moyoni bado ni wanachadema.

Ingizo jipya? Lipo. Linatoka CCM. CCM inawanyoosha sana wananchi right, left and centre. Hata wale wabishi nao wamenyooka sasa wanaelewa CCM haina ishu tena imefeli.

Utayari wa CHADEMA kupewa nchi? Bado sana. Hii nasema bado sana.

Bado chadema ipo vulnerable mno kushika nchi nazungumzia urais. Hawana 'Presidential Presentations' yaani sio presentable ki urais. Dizain wame pose ki uharakati zaidi.

Of coz mtu kama Mbowe ni Presidential material lkn hana watu presentable. Wengi wanaomzunguka wapo presentable kiunaharakati. Lkn wana akili sana tena sana.

Wana nguvu wapi?

Kwenye majimbo na Kata na Serikali za mitaa. Kule wapo very powerful. Na wana energy sana. Kigingi kikubwa ni polisi na mitutu yao. Isingekuwa Polisi tusingekuwa tunaongea mengine.

Nini kifanyike?

Hata sijui. Lkn waendelee kuombea hali mbaya kwa wananchi ili chuki izidi kuongezeka kwa CCM chama tawala.

One point to remember:

Siasa ni biashara kama zilivyo biashara zingine tu. Wanasiasa ni wajasiriamali wa siasa. Elewa hivyo.

Kwa maneno haya chadema inatazamwa kama kampuni fulani hv inayo trade publicly hivyo hivyo kwa CCM na vyama vingine.

Wenye akili zao lazima waangalie portfolio zao na ku check returns.

So, chadema inapaswa kuendelea kujijenga zaidi. Adui yao mkubwa kwa sasa ni 'POLISI' wala sio CCM.

Polisi ama vyombo vya dola kwa ujumla inafanya stock ya chadema isikue kwa kasi inayotakiwa.

Polisi inafanya watu wa maana kushindwa kuwekeza chadema publicly. Lkn wana inhale na exhale chadema. Heart beats zina pumb chadema blood lkn hawatoki front.

Pindi kundi hili watakapopata uhakika wa returns zao ndani ya chadema ndio siku hiyo chadema inachukua nchi mchana kweupe.

Nasisitiza: Adui wa chadema sio CCM bali ni Polisi. Polisi wanatumwa na CCM. Vyombo vya dola vinatumwa na CCM. Na CCM kamwe hawataacha kuwatuma.

Maana CCM kuwatuma wao itafanya ionekane sio wao bali ni masuala ya kiusalama ya nchi. CCM kila leo watakana kutumia polisi kujilinda.

Unataka kuelewa zaidi nje ya siasa za CHADEMA?

System ya nchi kama nchi haionekani kuwa stable sana. Taasisi almost karibu zote zipo very politicised. Hazina competence. Ni taasisi za vitisho zaidi kuliko kupokea challenges na kuzikabili ama kuzi address in a competence manner.

Sometimes ni kama wananchi wapo ahead of time kuliko system ya nchi. Jaribu kuangia mifumo ya elimu, afya na mengine mengi. Na hapa ndipo worry ilipo ikiwa vyama vya siasa vitashika dola huku taasisi nyeti zikiwa za kisiasa zaidi.

Tunaelekea wapi 20 years later? Sijui, lakini nina hofu km trend itaendelea kuwa hv.

Kuna muda unawaza au viongozi wetu sio wananchi wenzetu? Vile watoto wao wana uraia kwingine na hata pesa wameweka nje ya nchi. So huku wanavuna shamba la bibi na kutuachia maskini kila kitu kimeisha? Najiulizaga tu.

Ndivyo navyoona mimi.

Niite system hacker
 
Back
Top Bottom