Askari JWTZ Arusha amuua mfugaji kwa risasi

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia askari wa jeshi la wananchi Tanzania, (JWTZ), wilayani Monduli kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi mfugaji, Laisi Lemomo(26)Mkazi wa Kijiji Cha Lashaine wilayani Humo.

Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake kamanda wa jeshi la polisi Mkoani hapa, Justine Masejo alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi Julai 12 mwaka huu majira ya saa 10 jioni katika Kijiji hicho.

Alisema kuwa chanzo Cha tukio hilo bado kinachunguzwa baada kikosi Cha askari wa upelelezi kutoka makao makuu ya jeshi hilo Mkoani Arusha kutumwa eneo la tukio na kwamba taarifa zaidi juu ya tukio hilo zitatolewa hapo baadaye.

Wakati huo huo jeshi la polisi Mkoani hapa linamshikilia mganga wa kienyeji, (jina lina hifadhiwa) Mkazi wa Sombetini jijini Arusha anayedaiwa kumshawishi mtuhumiwa wa mauji ya Mtoto mwenye umri was miaka minne ambaye Julai Sita mwaka huu mwili wa Mtoto huyo ulikutwa kwenye shamba la Mikahawa eneo Burka jijini hapa ukiwa umetelekezwa.

Kamanda Masejo, alifafanua kwamba mwili wa marehemu wenye jinsia ya kiume ulikutwa na majeraha ya kipigo na kuzibwa mdomo na majani ya miti huku mtuhumiwa wa ukatili huo (jina linahifadhiwa) akidaiwa ni baba wa kufikia wa marehemu ambaye alikuwa akiishi naye.

Alisema kwamba mtuhumiwa huyo Mara baada ya kukamatwa na kuhojiwa alikiri kutenda unyama huo na kumtaja mganga huyo wa kienyeji kuwa ndiye aliyemshawishi kutenda tukio hilo kwa lengo la kumaliza kesi zake zinazomkabili mahakamani pamoja na kunyosha mambo yake ya kibiashara.

Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani Mara baada ya upelelezi was jeshi la polisi kukamilika.

Ends...
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia askari wa jeshi la wananchi Tanzania,(JWTZ),wilayani Monduli kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi mfugaji ,Laisi Lemomo(26)Mkazi wa Kijiji Cha Lashaine wilayani Humo .
Haya ni masikitiko makubwa. Kweli tunahitaji elimu elimu elimu. Ninauliza tu. Hakuna jinsi Serikali au jamii itafute njia ya kukataza huu utapeli wa hawa waganga maana ni chanzo cha migogoro katika jamii.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia askari wa jeshi la wananchi Tanzania,(JWTZ),wilayani Monduli kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi mfugaji ,Laisi Lemomo(26)Mkazi wa Kijiji Cha Lashaine wilayani Humo .
Mfumo wa Elimu umeoza, Daktari anatoa dozi ambayo sio ya ugonjwa, unatumia, siku unarudi hospital kucheki afya, unaambiwa kwanza mbona vipimo vyako havikuonyesha ugonjwa wowote, Wala hukutakiwa kutumia dozi, wakati huo umeishabwia madawa kibao.

Wanaofeli ndio wanaopelekwa jeshini, polisi, uhamiaji, mtu amedesa tangu sekondari mpaka chuo, unampa Idara aongoze,
Waziri wa Elimu "Profesa"Ndalichako, alishindwa kumudu majukumu balaza la mitiani, leo kapewa wizara, ukisikia anaongea au anachambua mada, unajiuliza huyu ndio Profesa, sasa kama mtu kwa miaka yote hiyo hakuweza hata kuwa na command ya lugha ya kigeni, aliyojifunza tangu darasa la tatu! Hataweza kweli kuwa na upeo wa kutatua mambo mazito ya Elimu.
 
Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) kwa tuhuma za mauaji ya mfugaji aliyefahamika kwa jina la Lais Lemomo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema leo Julai 14, 2021 kuwa mwanajeshi huyo anadaiwa kumpiga risasi Lemomo akiwa anachunga mifugo.

"Tukio hili lilitokea mnamo tarehe 12 mwezi huu majira ya jioni, timu ya makachero ipo katika eneo la tukio na uchunguzi utakapokamilika taarifa zaidi zitatolewa," amesema.

Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na pindi utakapokamilika taarifa kamili zitatolewa.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumbe na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Isack Joseph wamefika eneo la mauaji hayo, ambapo kumekuwa na mgogoro baina ya wafugaji na jeshi.

Mwaisumbe alitoa pole kwa familia ya marehemu na ameahidi kufanyika kwa uchunguzi wa tukio hilo na mtuhumiwa kufikishwa mahakamani.

Advertisement
Katika tukio lingine Kamanda Masejo amesema jeshi hilo linaendelea kumhoji mganga mmoja wa kienyeji mkazi wa Sombetini jijini Arusha kwa tuhuma za kumshawishi baba mmoja amfanyie ukatilii mtoto wake wa kufikia.

"Julai 8 mwaka huu tulitoa taarifa kuwa mtoto mwenye umri wa miaka minne alifanyiwa ukatili wa kipigo na kuwekewa majani mdomoni na baba yake wa kufikia, kisha akatelekezwa," aliongeza.

Masejo amesema baada ya kumkamata na kumhoji mganga huyo alikubali kuwa alimshawishi baba huyo afanye hivyo ili apate utajiri katika shughuli zake.
 
Hawa jamaa wamechanganyikiwa wanadhani hii nchi ni yao peke yao ujinga wa hali ya juu unapata mafunzo ya kuua unakuja kuua mfugaji hiyo karma yake ni ya vizazi kwa vizazi mpaka iishe...
 
Huyo kamanda hajui protocol mwanajeshi hawekwi kwenye selo moja na raia inabidi akafungwe kwenye selo zao
 
Pale pana shida sana, Wamasai wanaongezeka na Kambini ndio sehemu Yao ya Malisho, sasa unamkuta Masai ana Smart phone ana pinpoint maeneo au atapiga picha vifaru mazoezi ya kijeshi unamuachaje?
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia askari wa jeshi la wananchi Tanzania, (JWTZ), wilayani Monduli kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi mfugaji, Laisi Lemomo(26)Mkazi wa Kijiji Cha Lashaine wilayani Humo.

Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake kamanda wa jeshi la polisi Mkoani hapa, Justine Masejo alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi Julai 12 mwaka huu majira ya saa 10 jioni katika Kijiji hicho.

Alisema kuwa chanzo Cha tukio hilo bado kinachunguzwa baada kikosi Cha askari wa upelelezi kutoka makao makuu ya jeshi hilo Mkoani Arusha kutumwa eneo la tukio na kwamba taarifa zaidi juu ya tukio hilo zitatolewa hapo baadaye.

Wakati huo huo jeshi la polisi Mkoani hapa linamshikilia mganga wa kienyeji, (jina lina hifadhiwa) Mkazi wa Sombetini jijini Arusha anayedaiwa kumshawishi mtuhumiwa wa mauji ya Mtoto mwenye umri was miaka minne ambaye Julai Sita mwaka huu mwili wa Mtoto huyo ulikutwa kwenye shamba la Mikahawa eneo Burka jijini hapa ukiwa umetelekezwa.

Kamanda Masejo, alifafanua kwamba mwili wa marehemu wenye jinsia ya kiume ulikutwa na majeraha ya kipigo na kuzibwa mdomo na majani ya miti huku mtuhumiwa wa ukatili huo (jina linahifadhiwa) akidaiwa ni baba wa kufikia wa marehemu ambaye alikuwa akiishi naye.

Alisema kwamba mtuhumiwa huyo Mara baada ya kukamatwa na kuhojiwa alikiri kutenda unyama huo na kumtaja mganga huyo wa kienyeji kuwa ndiye aliyemshawishi kutenda tukio hilo kwa lengo la kumaliza kesi zake zinazomkabili mahakamani pamoja na kunyosha mambo yake ya kibiashara.

Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani Mara baada ya upelelezi was jeshi la polisi kukamilika.

Ends...
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amina. Tunaomba muhusika ashukuliwe hatua kali za kisheria tumechoka na haya matukio sahivi.
 
Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) kwa tuhuma za mauaji ya mfugaji aliyefahamika kwa jina la Lais Lemomo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema leo Julai 14, 2021 kuwa mwanajeshi huyo anadaiwa kumpiga risasi Lemomo akiwa anachunga mifugo.

"Tukio hili lilitokea mnamo tarehe 12 mwezi huu majira ya jioni, timu ya makachero ipo katika eneo la tukio na uchunguzi utakapokamilika taarifa zaidi zitatolewa," amesema.

Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na pindi utakapokamilika taarifa kamili zitatolewa.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumbe na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Isack Joseph wamefika eneo la mauaji hayo, ambapo kumekuwa na mgogoro baina ya wafugaji na jeshi.

Mwaisumbe alitoa pole kwa familia ya marehemu na ameahidi kufanyika kwa uchunguzi wa tukio hilo na mtuhumiwa kufikishwa mahakamani.

Advertisement
Katika tukio lingine Kamanda Masejo amesema jeshi hilo linaendelea kumhoji mganga mmoja wa kienyeji mkazi wa Sombetini jijini Arusha kwa tuhuma za kumshawishi baba mmoja amfanyie ukatilii mtoto wake wa kufikia.

"Julai 8 mwaka huu tulitoa taarifa kuwa mtoto mwenye umri wa miaka minne alifanyiwa ukatili wa kipigo na kuwekewa majani mdomoni na baba yake wa kufikia, kisha akatelekezwa," aliongeza.

Masejo amesema baada ya kumkamata na kumhoji mganga huyo alikubali kuwa alimshawishi baba huyo afanye hivyo ili apate utajiri katika shughuli zake.
Arusha nako kuna mambo mambo yao fulani siyaelewagi....
 
kwa niwazavyo ,huyo mwanajeshi ataachiwa kwasababu zifuatazo. 1. kama eneo lilikuwa na mgogoro baina ya wafugaji na jeshi ,ina maanisha huyo mfugaji kama ninavyowafahamu tena wa kimasai alitaka kumshambulia huyo mjeshi na katika kujihami mjeshi akafyatua risasi kujihami ila halikuwa lengo kuua ,so hiyo ni ajali kama ajari zingine, 2.kuna mazingira ya huyo mfugaji kukataa amri halali ya askari huyo wa JWTZ, maana wafugaji huwa na morare sana tena wakati wa kuwalisha wanyama wao huwa wanakuwa wanyama pia ikitokea kunakitu kinatishia maslahi ya wanyama wao.
 
Huyo kamanda hajui protocol mwanajeshi hawekwi kwenye selo moja na raia inabidi akafungwe kwenye selo zao
Wewe unayejua protocol una heri. Unajua wanajeshi wangapi wako mahabusu magerezani wakisubiri kesi zao za mauaji ya raia?
 
Sifahamu mkuu ila military protocol mwanajeshi yeyote ambaye bado analitumikia jeshi hapaswi fungwa wa shitakiwa na mahakama za kiraia mpaka atakapo vuliwa uanajeshi ndio maana wana mahakama zao na police wao na cell zao
 
Back
Top Bottom