Taratibu za kupata passport ya kusafiri zipoje?

soma hapo mkuu
Mahitaji;
1. Kitambulisho cha taifa
2. Barua ya mwajiri/
3. Leseni ya biashara kama umejiri/kampuni
4. Andika/andikiwa barua ya maombi ukieleza sababu za safari zako/nchi utakazozitembelea
5. Cheti cha kuzaliwa/hati ya kiapo
6. Cheti cha kuzaliwa cha mzazi mmoja/hati ya kiapo
Maombi ya awali yanaanzia kwenye tovuti ya uhamiaji na utalipia 20k
Jumla ya gharama ni 150k
wengine waongezee
Kupata pasipoti kwa sasa ni rahisi mno,
1. Cha muhimu uwe na
2. Cheti cha kuzaliwa
3. Kitambulisho cha utaifa
4. "Safari"
5. Uthibitisho wa uraia wa mmoja wa wazazi wako.

Maximum inapatikana ndani ya week mbili,

Process zinaanzia online

Total cost ni 150,000.
Kama yapi mkuu?
 
Kupata PASSPORT siyo jambo rahisi kama wadau wanavyoeleza hapo juu, Hata kama unavyo vielelezo vyote Kitambulisho cha Taifa, Kitambulisho cha Kazi, Cheti cha Kuzaliwa n.k utasumbuka tuu.Mimi nimeamua kuachana na habari za kuomba Passport baada ya kukatishwa tamaa kwamba siwezi pata kisa Natumia Majina ya Ukoo wa Mama. Kama unatumia majina ya Ukoo wa Mama au kwa wale walioolewa na kubadilisha majina shughuli yake siyo ndogo wazee.
 
Habari wakuu naomba msaada kujua gharama za kupata passport ya kusafiria ya miaka kumi pia... process zake za kupata zikoje
 
Walikuona mpumbavu utatumia vipi majina ya ukoo wa mama?ila pole mkuu maafisa uhamiaji wa kichaga ama kaskazini hawataki kabisa kusikia ujinga huo wa majina toka ukoo wa mama ni fedhea kubwa
 
niwe mkweli tu zilinitoka japo najua ni haki yangu lkn niligonga mwamba hadi nilipojiongeza, anayesema hakuna rushwa anajidanganya, awamu hii rushwa ni nzito zaidi ama utoe au ukose huduma.
Huwezi amini niliojiandikisha nao oktoba 2017 hadi leo hawana kitambulisho
Ukiona mtu anakuambia hakuna rushwa au utendaji umeboreka sana basi fahamu huyo anaongea kwa kuwasikia wanasiasa na hajawahi kuwa na issue inayohotaji mkono wa watendaji wa serikali, na idara zake!!! Mi mwenyewe ni majuzi tu tumekaa bila umeme kwa siku 9, na kabla ya hapo wahusika waliongea bila aibu kwamba inachukua wiki 2-3 lakini kama nataka fasta, basi nitoe rushwa!!
 
Kiukweli rushwa ipo na huo ndio mfumo uliotengenezwa kwenye kila kitengo kwa miaka mingi sana.
Kwa hiyo sio kazi rahisi kuitokomeza hii hali.
Na watu wapenda rushwa wanakupata wakati unapokuwa na haraka sana na huduma na ndio mwanya unapatikana.
Mimi nashukuru Niliomba passport wiki 4 zilizopita na majuzi nimeipata bila kutoa rushwa.
Lakini nilitumia nguvu ya ziada kubanana nao mguu kwa mguu,hadi kwenye maofisi ya mabosi wao ndio nikaipush kuipata, vinginevyo ingepita miezi hata miwili bila kuitia mkononi.
 
Walikuona mpumbavu utatumia vipi majina ya ukoo wa mama?ila pole mkuu maafisa uhamiaji wa kichaga ama kaskazini hawataki kabisa kusikia ujinga huo wa majina toka ukoo wa mama ni fedhea kubwa
Duuuuh! Sawa
 
Kiukweli rushwa ipo na huo ndio mfumo uliotengenezwa kwenye kila kitengo kwa miaka mingi sana.
Kwa hiyo sio kazi rahisi kuitokomeza hii hali.
Na watu wapenda rushwa wanakupata wakati unapokuwa na haraka sana na huduma na ndio mwanya unapatikana.
Mimi nashukuru Niliomba passport wiki 4 zilizopita na majuzi nimeipata bila kutoa rushwa.
Lakini nilitumia nguvu ya ziada kubanana nao mguu kwa mguu,hadi kwenye maofisi ya mabosi wao ndio nikaipush kuipata, vinginevyo ingepita miezi hata miwili bila kuitia mkononi.
Nimeipata kwa siku 12 tangu niwasilishe maombi
 
Attachments

  • IMG_20190916_074001.jpg
    IMG_20190916_074001.jpg
    203.4 KB · Views: 46
150k lakini kama huna cheti cha kuzaliwa na cha mzazi wako andaa 20k kila cheti
Habari wakuu naomba msaada kujua gharama za kupata passport ya kusafiria ya miaka kumi pia... process zake za kupata zikoje
 
Kweli kabisa
Ukiona mtu anakuambia hakuna rushwa au utendaji umeboreka sana basi fahamu huyo anaongea kwa kuwasikia wanasiasa na hajawahi kuwa na issue inayohotaji mkono wa watendaji wa serikali, na idara zake!!! Mi mwenyewe ni majuzi tu tumekaa bila umeme kwa siku 9, na kabla ya hapo wahusika waliongea bila aibu kwamba inachukua wiki 2-3 lakini kama nataka fasta, basi nitoe rushwa!!
 
Daah mambo yamebadilika sana Mimi nilipata kwa tsh elfu 50..sema nilifanya urafiki na jmaa mmoja wa migration mambo yakaenda vizur bila kutoa rushwa. Ndani ya wiki 3 nikawa nimepata..it was back 2014 those days
Pasi mpya gharama ni 150000. Hata kama unayo passport ya zamani ambayo bado haijaisha muda wake, ukitaka kusafiri utalazimika kubadili ili upate pasi ya kielektroniki, za zamani hazitumiki tena.
 
Back
Top Bottom