Msaada kuhusu kupata leseni ya kampuni

Msaada kuhusu kupata leseni ya kampuni

Ed edd n eddy

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2016
Posts
251
Reaction score
324
Habari ndugu zangu, naomba msaada kidogo.

Nimesajili kampuni na sasa nataka kupata leseni ya biashara kwa jina la kampuni. Tatizo ni kwamba nikitumia portal ya TAUSI, naona option ya kuomba leseni ya biashara kwa jina langu binafsi, lakini sioni sehemu ya kuomba leseni kwa jina la kampuni.

Nataka leseni iwe chini ya jina la kampuni, ili niweze pia kufungua akaunti ya benki ya kampuni kwa kutumia jina hilo.

Kama kuna mtu mwenye uzoefu na mchakato huu au anayejua jinsi ya kutumia TAUSI kupata leseni kwa kampuni iliyosajiliwa, naomba msaada wa kuelekezwa hatua kwa hatua.

Kama kuna agent, accountant au mtu anayefanya huduma hii naweza pia kuwasiliana naye.

Naomba msaada wa mtu yeyote anayejua namna ya ku-navigate hii process. Asanteni sana.
 
Kama kampuni imesajiliwa tayari, kwa kawaida leseni ya biashara inapaswa kuombwa kwa taarifa za kampuni, siyo jina lako binafsi. Kwenye TAUSI, hakikisha umeingia/ume-link taarifa za kampuni husika na una nyaraka zake kama Certificate of Incorporation, TIN na taarifa za biashara.

Kama option ya kampuni haionekani, inaweza kuwa suala la profile/account au aina ya huduma unayoomba. Ni bora usiombe kwa jina lako binafsi halafu baadaye ujaribu kubadilisha.

Ushauri wangu: fika kwenye ofisi ya mamlaka inayotoa leseni eneo ambalo biashara ipo, waonyeshe Certificate of Incorporation na TIN ya kampuni, waombe wakuelekeze namna ya ku-link kampuni kwenye TAUSI. Ukishapata leseni kwa jina la kampuni, ndipo mambo ya akaunti ya benki ya kampuni yatakuwa straightforward zaidi.
 
So niende wilayani au sio?
 
Back
Top Bottom