RESOLVED KERO Uhamiaji Arusha wanasema maombi yetu ya Passport hayaonekani kwenye mfumo, wanasema tulipie tena

RESOLVED KERO Uhamiaji Arusha wanasema maombi yetu ya Passport hayaonekani kwenye mfumo, wanasema tulipie tena

Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
491
Reaction score
781
Nilifanya maombi yangu mwezi Februari 2026 na nikalipia gharama zote zinazohitajika kwa mujibu wa taratibu. Baada ya kusubiri kwa muda mrefu bila kupata mrejesho, nilipofika kufuatilia niliambiwa kuwa maombi yangu hayaonekani kwenye mfumo.

Jambo lililonishangaza zaidi ni kwamba niliambiwa nifanye upya maombi na nilipie tena ada, bila kupewa maelezo ya kina kuhusu nini kilitokea kwa maombi yangu ya awali pamoja na fedha niliyolipa.

Kinachoumiza zaidi ni kwamba hakuna taarifa rasmi niliyopewa kwa maandishi, bali naambiwa kwa mdomo tu, hali inayoniacha katika sintofahamu kubwa na hofu ya kupoteza fedha zangu bila haki.

Ninaomba sana mamlaka husika ziingilie kati ili kupata ufafanuzi wa kina kuhusu tatizo hili, na kuhakikisha haki zetu kama waombaji zinazingatiwa bila kulazimika kulipia huduma mara mbili bila sababu ya msingi.

Ufafanuzi: Uhamiaji: Mfumo ulisumbua na sasa umekaa sawa, taarifa za walioomba Passport zipo, hawatakiwi kulipa mara 2
 
Hauna kithibitisho chochote kinachoonesha kama ulilipia? Mkuu
 
kila sehemu wizi mliyemkuta alichukua hela akaenda kunywa pombe
 
Back
Top Bottom