Taratibu jamii ya Watanzania inaanza kuinyanyapaa elimu ya mtaala wa NECTA. Unaweza kuamini msomi kama Carol Ndosi anaweza kuandika kitu kama hiki

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,121
27,128
Wewe Mtanzania ambae bado haujajuwa kwamba sasa hivi tunaishi kwenye zama za internet na kwa sasa dunia umebadili uelekeo wake utakuja kustuka ukiwa umechoka sana.

Unyanyapaa dhidi ya elimu.

1. Wasomi wana nyanyapaliwa.

2. Elimu ina nyanya paliwa.

3. Mifano inatolewa mingi kwamba ambao hawajaenda shule ndio wanafanikiwa zaidi kuliko walioenda shule...

Kuna muda utafika kusoma itaonekana ushamba na kupoteza muda.

Zamani kupiga 5 n.a. 6 ilikuwa big deal siku hizi madogo wanapata division one form four wanaenda chuo kusomea skills ( na kiuhalisia huo ndio uamuzi mzuri kwa sababu kuwa na skills ni bora kuliko degree. )

Ona kwa mfano huu msemo unao wakejeli wanafunzi waliokuwa wnakuwa wa kwanza darasani kwamba now hawana maisha yoyote.

Mbaya zaidi kauli kama inatolewa na wasomi na watu wanao heshimika katika jamii.

Mtoto anaesoma akikutana na comments zinazo waponda watu ambao walikuwaga wanashika namba za juu shuleni anaweza kuwa disappointed. Anaweza kuona kumbe kusoma ni ujinga.

Nilifanya uamuzi mzuri sana kuwatoa wanangu kwenye shule za mamilioni na kuwaleta Kayumba kwa sababu tunakoelekea elimu hii ya mtaala wa Necta itakuwa haina tena vigezo cha kuitwa elimu na haitokuwa na thamani ya kulipiwa mamilioni.
Ninasema tunakoelekea as if bado hatujafika.

Screenshot_20230929-165107.png
 
Primary nilikua mtoro sugu zali la mentali likaniangukia nikachaguliwa Second selection shule ya Serikali, Form 1 nikaburuzwa sana na watoto waliotoka English medium, kuanzia kidato cha pili hadi 4 nilikua namba 1 shule nzima, Baada ya kuingia form 5 PCM nikaona hapa nimekuja kupoteza muda ila hamna namna nikasema 6 nitatoboa tu, nikawa siendi darasani kutwa nashinda bwenini then mchana baada ya Lunch naingia kijijini na wadau wangu tunaenda kupiga stori na wanakijiji + kunywa pombe za kienyeji, mock ya form 6 nikapiga ZERO (0) Saafi, ila kwakuwa tayari nilikua na plan yangu kichwani wala matokeo hayo hayakunishtua kabisa, miezi 5 kabla ya necta nikaanza kula msuli yatima, lengo ikiwa kupata division two au three ya mwanzo, bahati nzuri NECTA nikapata div 3.13, chuo nlichokua nataka kwenda na Course tayari nilikua nishachagua tangu niko Advance. Kweli chuo nikaenda nilichokichagua na course yangu ile ile. Kufika chuo semister ya pili nikaona hapa pia mbona kama napoteza muda??!! Lecturer anafundisha database na networking kwenye ubao na chaki nikaona huu ni ujinga, nikachagua kuzama kwenye Programming kwa mbinu zile zile za msuli yatima, it paid off, nilikua najitahidi tu niwe na Gentlemen GPA. All in all kama unauwezo wa kufaulu wewe faulu tu, maisha hayana formula.
 
Back
Top Bottom