Watanzania wamepiga kelele we mara wakateuliwa maprofesa kushika Wizara ya Elimu na wakatueleza tutulie mabadiliko yako yanafanyiwa kazi.
Niseme kitu kimoja " Sijawahi kuwaamini maprofesa wetu", nahisi watastup[iga na kitu kizito.
Nimefuatilia michango ya maprofesa wetu mpaka juzijuzi hapa wametufanyia utafiti wa chanzo cha uchafuzi mto mara na kuzua taharuki.
Natabiri watajifungia na wakiibuka wataibuka na kuingiza elimu ya kushona, ujenzi, ufundi umeme, ufundi magari, kilimo kwenye mitaala ya elimu ya msingi.
To be honest only a layman asiyestahili hata kuongoza familia yake ndiye anayeweza kuibuka na mapendekezo ya kuingiza elimu ya ufundi au skills kwenye mitaala kama utatuzi wa changamoto zetu.
Msomi yoyote aliyeelimika ataanzia kujiuliza hivi changamoto za wastanzania ni nini?
1. Je, Jamii inakosa vijana wenye skills ----- Hapana vijana wapo wengi tu wanaofundishwa mitaani, wanaotoka vyuo vya veta, SIDO = hivyo skills siyo tatizo
2. Nini Changamoto ya vijana wenye skills ----- wengi wanalamikia ajira, kijana mmoja anajifunza kuchomelea anakosa ajira, anajifunza kushona anakosa ajira, anajifunza ujenzi na bado unakuta anaishi kwa kubaingaiza akiwa na taaluma zaidi ya mbili = Tatizo ni maarifa ya kuwawezesha kujiajiri
3. Je, Jamii inakosa wasomi wenye elimu ya juu ---- hapana vyuo vikuu na vya kati vinavyotoa vyeti, shahada na astashahada vimekuwa vingi
4. Je, nini changamoto kwa hawa wasomi wa elimu ya juu ---- Wengi changamoto kwao ni ukosefu wa ajira na umakini katika kutekeleza majukumu ya taaluma zao
Kwa kifupi chgangamoto kubwa kwa jamii nzima
1. ukosefu wa ajira baada ya kuhitimu taaluma zao
2. Ukosefu wa umakini
3. Ukosefu wa maadili hasa kwenye eneo la uaminifu
4. ..............
Mabadiliko katika mitaala yalenge kutatua changamoto zetu. Kama shida ya watanzania wengi ni kukosa ajira na kushindwa kujiajiri basi elimu muhimu kwa ajili ya ujasiliasmali iingizwe.
Watu wafundishwe kubaini fursa zilizowazunguka, watu wafundishwe nidhamu za ujasiliamali kama kujizuia vitu vya anasa kudunduliza mtaji, kumtumikia mtu ili upate ujuzi na mtaji, jinsi ya kufanya kazi na taasisi za mikopo, namna ya kutafuta masoko na bidhaa au huduma, uaminifu katika kutoa huduma, jinsi ya kubuni wazo la biashara kama ni kuzalisha kwa kubuni, kukopi au kuuza bidhaa za wengine.
Jamii ifundishwe namna ya kuingia Joint venture, miiko ya venture, majukumu ya pande zote. hapa nitoe ufafanuzi kwamba unakuta mtu yuko ofisini na anatamani kufanya kilimo hana mda lakini anaweza kupata mtaji.
Kuna kijana amekosa ajira ana mda wa kulima lakini hawa hawaji pamoja na kukubaliana kuingia ubia ili walime kwa pamoja.
Mwenye mtaji anatamani ampate kijana wa kumtumikia bure na kijana hayuko tayari kubeba maono ya wengine.
wanabaki kuogopana na wote kushindwa kuingia ubia wenye tija kwa wote.
Tunataka jamii ya kesho kila mwana jamii aone ubia kama fursa, ajue akihitaji mbia siyo kwa ajili ya kumnyonya au kumwibia.
Hawa wote wajue namna ya kufuatilia shughuli zao na wajue kuna changamoto na wawekwe tayari kuzitatua.
Wote wajue namna gani wanaweza kutumnia taasisi za mikopo kuendeleza shughuli zao.
Ila wasije kutwambia kutatua changamoto zetu ni kwamba kila mtanzania akimaliza darasa la saba ajue taaluma ya ushonaji, this will be nonsense, kujua kushona kutamsaidiaje mhitimu aliyemaliza chuo kikuu akakosa ajira?
Nani kawaambia ufundi cherehani ni taaluma ambayo kila mwenye ujuzi atapata ajira na apate ujira. ni vijana wangapi wako mtaani leo wamesoma cherehani na hawana ajira.
Mabadiliko ya elimu yanatakiwa ku add value kwenye elimu yetu ili kila mmoja kile alichojifunza kifanye kazi na siyo kuongeza ujuzi wa kipuuzi ambao hauna guarantee ya ajira.
Tunahitaji watu wetu wawe creative, wawe na focus ya kuona fursa kwenye jamii, wawe na nidhamu za kikazi na kijasiliamali n.k
Waache kujifungia na kufanya mambo mpaka yaishe alafu ndiyop waibuke na mambo ambayo hata kama wamebuni ugoro watakaa kuyatetea ili waonekane wamefanya bora.
Walete mjadala jamii ijadili ni kitu wanakitaka katika mabadiliko ya elimu, wao wapendekeze baadhi na mjadala wa jamii utasaidia kuongeza na kupunguza.