Tanzia: Mwana JF Straton Mushi aaga dunia

Tanzia: Mwana JF Straton Mushi aaga dunia

Kwa masikitiko makubwa ninapenda kuwataarifu msiba wa mwana JF mwenzetu bwana Straton Mushi aliyefariki mapema wiki hii baada ya kuugua muda mfupi. Mwili wa marehemu uliagwa Jana nyumbani kwake Salasala Dar Es salaam na badae kusafirishwa kuelekea Moshi- Uru Mawela kanisani kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho jumamosi hapo hapo Mawela.

Marehemu atakumbukwa kwa upendo wake na harakati za kupigania haki bila kuogopa.

Poleni wana JF, wafanyakazi wote wa airtel na wanafamilia.

Kwa watakaoweza kwenda msibani Kama upo Moshi mjini Nenda stendi kuu panda magari yanaoenda uru halafu Shuka mawela kanisani hapo hapo kushoto kwako Ndio penye msiba. Kama unatumia usafiri binafsi basi ukifika Mawela kanisani ukiulizia kwenye msiba utaoneshwa bila wasiwasi.

Bwana alitoa na Bwana alitwaa jina lake lihimidiwe.

View attachment 1269118
RIP Straton.
 
Hapo ndo nlipokosea. Ndo basi tena. We jua kwa uhakika kabisa alikuwa mmoja wetu. Ila ID yake sitataja kwa kuwa nshataja jina.
Lakini kipi bora?? Kujua mhogo mchungu (JF ID ) amekufa au kujua amina ramadhan ( jina real la mhogo mchungu) amekufa??
Yaani mfano ungesema ni Jon Stephano kafariki ingenigusa sana kuliko jina la kweli ambalo silijui
 
R.I.P our mate

Mimi pia naaza kufikiria kujenga urafiki wa kindugu na baadhi ya members wenzangu humu ili hata ikitokea nikafariki basi taarifa zangu zifikishwe mapema.
Yeyote atakayependa kuunga urafiki wa dhati na mimi naomba anipm tujuane
 
Unapenda kutangazwa umekufa?
Sasa ikusaidie nini, uombewe uende mbinguni??
 
Jamani nipate mchango Kwani me ni mama au mke wa marehemu?? Kuna mahali nimeomba hata Mia?? Kama marehemu mwenyewe akiwa hai hakupenda kuw verified why Mimi nifanye hivyo?? Asee ile familia ni tajiri haina shida hata na Mia ya mtu. Na Mimi Wala sio ndugu wa familia Bali ni rafiki tu.
NIKOME.
Sasa kama marehemu hakutaka kuwa verified kimbelembele na umbea imemletea nani humu tulikuomba habari zake? unavujisha siri wakati marehemu hakutaka kujulikana hata kwa kifo chake . mbea sana wewe.
 
R.I.P our mate

Mimi pia naaza kufikiria kujenga urafiki wa kindugu na baadhi ya members wenzangu humu ili hata ikitokea nikafariki basi taarifa zangu zifikishwe mapema.
Yeyote atakayependa kuunga urafiki wa dhati na mimi naomba anipm tujuane
Itakusaidia nini ukitangazwa mkuu?
 
Exactly. Na JF haina sababu ya kupata taarifa za kifo chake. Sema tu some random person died na sio mwanaJF mwenzetu as kinachotuunganisha huku ni ID ambayo hutaitaja.
Angebaki na taarifa yake kwa sababu huyo Mushi sisi hatumjui angetaja ID yake ya humu kidogo taarifa ingekuwa na umuhimu.
 
Aithee mushi mtani wangu amefariki kwa sababu gani?
RIP ila si katuachia mke?

Majonzi makubwa sana
By SI mpare by tribe
 
Humu kuna member anaitwa
@nleterewanganengo.
Tusipomwona basi huendo yeye maana hii lugha na kabila la marehemu ni tabaka moja
 
Hakuweka wazi ID yake ya JF hivyo ni vyema tuheshimu maamuzi yake.
Nimekupenda bure... Buuure. wala usinilipe chochote. Ni wachache wenye busara kama wewe. Hapa tumeshuhudia watu wajinga kabisa wakiweka ID za marehemu ambao wakati wa uhai wao wote walikuwa hawataki kujianika kwa kila mtu. Matokeo yake hata michango mingine waliyotoa kwa faragha inakuja kuonekana hadharani. Hapa kuna watu wenye watoto, wajukuu, wake waume, wazazi nk Na katika michango yetu tunaandika mengi kwa sababu tunatumia ID ambazo siyo halisi. Unapokuja kuweka jina la marehemu wazi watu wanaanza kupekenyua kuangalia alikuwa anaandika nini. Imagine mtoto anakuta marehemu mama yake alikuwa member wa ''lile Jukwaa'' na alitoa somo la ''kula koni.'' Once again thank you na nategemea member wengine watajifunza. RIP marehemu.
 
Mleta mada wewe ndiye umeharibu kwa maoni yangu. Wewe kama unamfahamu, ungemtaja humu kwa ID yake (na kuficha jina lake halisi) maana ndiyo ambayo tungeweza kuji associate nae. Nje ya hapo taarifa yako inakosa impact kwa hapa JF. Hujatutendea haki.

RIP MwanaJF
Mkuu kutaja ID sio busara ni kama kumvua nguo marehemu.
 
Nimekupenda bure... Buuure. wala usinilipe chochote. Ni wachache wenye busara kama wewe. Hapa tumeshuhudia watu wajinga kabisa wakiweka ID za marehemu ambao wakati wa uhai wao wote walikuwa hawataki kujianika kwa kila mtu. Matokeo yake hata michango mingine waliyotoa kwa faragha inakuja kuonekana hadharani. Hapa kuna watu wenye watoto, wajukuu, wake waume, wazazi nk Na katika michango yetu tunaandika mengi kwa sababu tunatumia ID ambazo siyo halisi. Unapokuja kuweka jina la marehemu wazi watu wanaanza kupekenyua kuangalia alikuwa anaandika nini. Imagine mtoto anakuta marehemu mama yake alikuwa member wa ''lile Jukwaa'' na alitoa somo la ''kula koni.'' Once again thank you na nategemea member wengine watajifunza. RIP marehemu.
May be upo sawa, lkn kama ndo hivyo basi hakukuwa na haja ya kutoa taarifa kwamba mwanajf kafariki wakati hatumjui. Ni mtazamo wangu
 
Back
Top Bottom