Tanzia: Mwana JF Straton Mushi aaga dunia

Mrs Bishanga

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,002
2,272
Kwa masikitiko makubwa ninapenda kuwataarifu msiba wa mwana JF mwenzetu bwana Straton Mushi aliyefariki mapema wiki hii baada ya kuugua muda mfupi.

Mwili wa marehemu uliagwa Jana nyumbani kwake Salasala Dar Es salaam na badae kusafirishwa kuelekea Moshi- Uru Mawela kanisani kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho jumamosi hapo hapo Mawela.

Marehemu atakumbukwa kwa upendo wake na harakati za kupigania haki bila kuogopa.

Poleni wana JF, wafanyakazi wote wa Airtel na wanafamilia.

Kwa watakaoweza kwenda msibani Kama upo Moshi mjini Nenda stendi kuu panda magari yanaoenda uru halafu Shuka mawela kanisani hapo hapo kushoto kwako Ndio penye msiba. Kama unatumia usafiri binafsi basi ukifika Mawela kanisani ukiulizia kwenye msiba utaoneshwa bila wasiwasi.

Bwana alitoa na Bwana alitwaa jina lake lihimidiwe.

IMG_0533.JPG
 
"COMRADE" apumzike salama, ameumaliza mwendo. Wafikishie salamu kina "Mw. Nyerere" na "Baba Karume" yale waliotukataza ya kuchagua vingozi wasiofaa ndio imekua mila/ibada ya CCM. Ila tutaendelea kusukuma bendera JF mpaka tutakapofikia kilele cha demokrasia.

Swali fikirishi, sisi tusiojulikana kwa ndugu/jamaa/marafiki kama tunatumia JamiiForums, siku tukivuta taarifa za vifo sijui vipi itawafikia humu wana harakati wa JF.
 
Back
Top Bottom