TANZIA: Mh. Salim Hemed Khamis (CUF) afariki dunia

TANZIA: Mh. Salim Hemed Khamis (CUF) afariki dunia

Mbunge wa Chambani Salim Hemed Khamis,amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .Taratibu za kuusafirisha mwili kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanyika.

chanzo ITV
 
Ukitazama kiundani kwa marefu na mapana, haya maisha si chochote ila ni mtihani kwa asiyezindukana!
 
RIP mheshimiwa mbunge, mungu awape moyo wa subir wanafamilia, wana CUF, wabunge wote, watanzania na kila alieguswa na msiba huu
 
Pole kwa familia yake, kwa jimbo lake la chambani, kwa chama chake cha cuf na watanzania wote kwa msiba huu.
 
Mbunge wa Jimbo la Chambani, Salim Hemed Khamis (CUF), aliyeugua ghafla wakati akihudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jana amefariki dunia leo mchana kwa shinikizo la damu. Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahala pema, AMEN.
 
Mbunge wa Jimbo la Chambani, Salim Hemed Khamis (CUF), aliyeugua ghafla wakati akihudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jana amefariki dunia leo mchana kwa shinikizo la damu. Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahala pema peponi, AMEN.
 
Mungu amlaze mahali anapostahili kutokana na matendo yake aliyotenda siku za uhai wake.
 
Inasikitisha sana. Apumzike kwa amani. Lakini ilikuwaje akanywa dawa kabla ya kula!? Alikosa mpishi, alipolala hakuna hoteli inayouza aina ya vyakula alivyokuwa anapendelea kula, hakuwa fedha, alitingwa na kazi, au alikuwa ana mazoea ya kunywa dawa hizo bila ya kula?
 
Duh kifo cha ghafla hata usia inawezekana hakuacha
 
Back
Top Bottom