TANZIA: Mh. Salim Hemed Khamis (CUF) afariki dunia

Nyakageni

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2011
Posts
15,044
Reaction score
5,115
Aliyekuwa mbunge wa Chambani visiwani Zanzibar, Mheshimiwa Salim Hemed Khamis amefariki dunia. Taarifa zisizo rasimi ni kuwa amefariki hospitali alikopelekwa baada ya kuanguka. Marehemu amefariki na umri wa miaka 62.

Salamu za pole kwa wana CUF, Wana Chambani na wafiwa wote pamoja na ndugu na jamaa.

Mungu amlaze mahala pema peponi.
hon-hemed-khamis-salim-chambani.jpg

​
Confirmed na nina mtu nimetuma hapo ofisi za Bunge kuna press conference...

======================================================
Taarifa juu ya kuugua kwake Mh. Salim Hemed Khamis
======================================================

​
Mbunge wa Jimbo la Chambani, Salim Hemed Khamis (CUF), ameugua ghafla wakati akihudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Mbunge huyo alikutwa na masahibu hayo jana na alikimbizwa hospitalini kwa matibabu ambako alilazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU).
Wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Edward Lowassa, na Makamu Mwenyekiti, Mussa Hassan Zungu na baadhi ya wajumbe walimtoa nje ya ukumbi na kumpepea kwa kutumia magazeti na majarida.

Hata hivyo, hali yake ilizidi kuwa mbaya huku akizungumza kwa tabu kuwa alikunywa dawa za shinikizo la damu (BP) kabla hajala chochote na hivyo kuzidiwa.

Wabunge hao na maofisa wa Bunge, waliendelea kumpepea ili apate ahueni, lakini hali ilizidi kuwa mbaya na kushindwa kuongea kila alipoulizwa jambo.

Walimbeba na baada ya muda waliomba msaada kwa wanahabari waliokuwapo eneo hilo huku wakiwazuia wasipige picha za tukio hilo kwa maelezo kuwa si kila kitu ni habari.

Waandishi watano walisaidiana na wabunge hao kumbeba kwa kupitia mlango wa dharura na alipakizwa kwenye gari la ofisi ya Bunge lenye namba za usajili STK 2178 likiongozwa na pikipiki ya polisi yenye namba za usajili PT 2591.

Gari iliyombeba Mbunge huyo iliondoka kwenye ofisi hizo saa 5:15 asubuhi na habari zilizopatikana baadaye zilieleza kuwa alipelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Baadhi ya wabunge walisema kuwa Khamis akiwa amekaa, ghafla alianza kutapika huku akilalamika kuwa hajisikii vizuri baada ya kunywa dawa za BP na hali yake kubadilika na walisaidiana kumtoa nje ya chumba cha mkutano.

Pamoja na wabunge hao pia, alikuwapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Waliomsindikiza hospitalini ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Amour Arfi (Chadema) na Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF).

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kurejea kutoka Muhimbili, Khalifa alisema Khamis alipokewa na alikuwa anaendelea kupatiwa matibabu.

Khalifa alifafanua kuwa Khamis anasumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Edward Lowassa, alisema hali yake ilikuwa inaendelea vizuri na kuthibitisha kuwa amelazwa ICU. Lowassa alisema kuwa miezi mitatu iliyopita Khamis alikuwa India kwa matibabu. Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Aminiel Eligaesha, alipoulizwa kwa njia ya simu, alithibitisha kuwa mbunge huyo kupokewa hospitalini hapo na kuongeza kuwa alipatiwa matibabu na anaendelea vizuri. Hata hivyo, alisema taarifa kamili itatolewa na ofisi za Bunge.

Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, alisema hadi jana jioni mbunge huyo alikuwa bado ICU chini ya uangalizi wa madaktari. "Bado yuko ICU. Wanamwangalia. Presure (shinikizo la damu) iko juu, tunampumzisha kidogo," alisema Joel akijibu swali la NIPASHE kuhusu maendeleo ya afya ya mbunge huyo. Akijibu swali iwapo kuna mpango wowote wa kumpeleka mbunge huyo kupatiwa matibabu zaidi nje ya nchi, alisema: "Tunasubiri ushauri wa madaktari."

CHANZO: Nipashe
 
Niliona mahali picha ya mbunge kutolewa ukumbini baada ya kudondoka. Sikumbuki nilisoma wapi.
 
bwana amekupenda zaidi upumzike kwa Amani.
 
kama ni kweli R.I.P.
kila mtu ataonja mauti,hata hao wanaotungoa meno na kucha ipo siku nao hii dunia hawataiona na wanaowaagiza watakufa pia!!
 
Nimeiona facebook pia kwenye wall ya mwananchi kaandika hiyo taarifa lakini nae akitaka wazidi kufuatilia kujua ukweli wake.
 
Mbunge wa Jimbo la Chambani, Salim Hemed Khamis (CUF), ameugua ghafla wakati akihudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Mbunge huyo alikutwa na masahibu hayo jana na alikimbizwa hospitalini kwa matibabu ambako alilazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU).
Wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Edward Lowassa, na Makamu Mwenyekiti, Mussa Hassan Zungu na baadhi ya wajumbe walimtoa nje ya ukumbi na kumpepea kwa kutumia magazeti na majarida.

Hata hivyo, hali yake ilizidi kuwa mbaya huku akizungumza kwa tabu kuwa alikunywa dawa za shinikizo la damu (BP) kabla hajala chochote na hivyo kuzidiwa.

Wabunge hao na maofisa wa Bunge, waliendelea kumpepea ili apate ahueni, lakini hali ilizidi kuwa mbaya na kushindwa kuongea kila alipoulizwa jambo.

Walimbeba na baada ya muda waliomba msaada kwa wanahabari waliokuwapo eneo hilo huku wakiwazuia wasipige picha za tukio hilo kwa maelezo kuwa si kila kitu ni habari.

Waandishi watano walisaidiana na wabunge hao kumbeba kwa kupitia mlango wa dharura na alipakizwa kwenye gari la ofisi ya Bunge lenye namba za usajili STK 2178 likiongozwa na pikipiki ya polisi yenye namba za usajili PT 2591.

Gari iliyombeba Mbunge huyo iliondoka kwenye ofisi hizo saa 5:15 asubuhi na habari zilizopatikana baadaye zilieleza kuwa alipelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Baadhi ya wabunge walisema kuwa Khamis akiwa amekaa, ghafla alianza kutapika huku akilalamika kuwa hajisikii vizuri baada ya kunywa dawa za BP na hali yake kubadilika na walisaidiana kumtoa nje ya chumba cha mkutano.

Pamoja na wabunge hao pia, alikuwapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Waliomsindikiza hospitalini ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Amour Arfi (Chadema) na Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF).

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kurejea kutoka Muhimbili, Khalifa alisema Khamis alipokewa na alikuwa anaendelea kupatiwa matibabu.

Khalifa alifafanua kuwa Khamis anasumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Edward Lowassa, alisema hali yake ilikuwa inaendelea vizuri na kuthibitisha kuwa amelazwa ICU. Lowassa alisema kuwa miezi mitatu iliyopita Khamis alikuwa India kwa matibabu. Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Aminiel Eligaesha, alipoulizwa kwa njia ya simu, alithibitisha kuwa mbunge huyo kupokewa hospitalini hapo na kuongeza kuwa alipatiwa matibabu na anaendelea vizuri. Hata hivyo, alisema taarifa kamili itatolewa na ofisi za Bunge.

Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, alisema hadi jana jioni mbunge huyo alikuwa bado ICU chini ya uangalizi wa madaktari. "Bado yuko ICU. Wanamwangalia. Presure (shinikizo la damu) iko juu, tunampumzisha kidogo," alisema Joel akijibu swali la NIPASHE kuhusu maendeleo ya afya ya mbunge huyo. Akijibu swali iwapo kuna mpango wowote wa kumpeleka mbunge huyo kupatiwa matibabu zaidi nje ya nchi, alisema: "Tunasubiri ushauri wa madaktari."

CHANZO: Nipashe
 
Mungu amlaze mahala pema , nawaomba wanandugu na wengine wawe na subira katika kipindi hiki kigumu.
 
Pole kwa familia, pole wabunge na watanzania kwa ujumla, mungu amlaze panapostahili, amen!
 
Ndg wana Jf,nimepata taarifa zisizo rasmi kuxa mbunge aliyeanguka jana kwenye ofisi ndogo za bunge na kukimbizwa hospitali ya rufaa Mhimbili amefariki dunia...
 
Kama taarifa sio rasmi nadhani hakuna haja ya kuharakisha kuzileta humu haswa unapokuwa unazunguzia KIFO.
 
Back
Top Bottom