Tanzia: Mama yangu mzazi ameaga dunia

Tanzia: Mama yangu mzazi ameaga dunia

Umefiwa na mama yako mzazi muda wa kuingia JF unautoa wapi wewe?

Nyani, jaribu kuwa mstaarabu kidogo sio kila kitu unaleta ubishani wa kitoto. Kwani kuingia JF inachukua week nzima???
Jaribu kumpa support mwenzio, mpaka amefikiria kuja humu ina maana anajua atapata msaada either wa maombi hata faraja, hizihizi pole unazoona hazina maana zinampa nguvu mfiwa.
Pole sana Ijoz.

R.I.P Mama wa member mwenzetu.
 
Ndio mila zetu mkuu. unapaswa kuzidumisha.

Ndugu yangu, umefika wakati wa kuachana na mila zisizo na maana. Mwenzio amefiwa wewe unamwagia maji, unacheza ngoma, unatania matendo aliyokuwa anafanya marehemu! unazuia jeneza eti upewe pesa!! mmmmm hii mila hovyo kabisa
 
Mungu awajaze moyo wa subira katika hili, pole sana mdau tumuombee mama yetu apumzishwe kwa amani.
 
Ndugu yangu, umefika wakati wa kuachana na mila zisizo na maana. Mwenzio amefiwa wewe unamwagia maji, unacheza ngoma, unatania matendo aliyokuwa anafanya marehemu! unazuia jeneza eti upewe pesa!! mmmmm hii mila hovyo kabisa

Kuna mama moja alikuwa anawanyima amani sana watu kwenye misiba kwa utani wake unaoelekea kwenye ukweli, sijui nguo za marehemu alikuwa anazipata vipi anavaa na kumuigiza, kuna siku mfiwa mmoja alimzaba vibao vya maana tu watu walimlaumu sana lakini ilisaidia sana kumbadili yule mama siku hiizi ametulia sana.
 
Umefiwa na mama yako mzazi muda wa kuingia JF unautoa wapi wewe?
Ukifiwa Nyani Ngabu unafarijika ukiwasiliana na marafiki. Kuna marafiki wa simu na marafiki wa kioo cha Computer. Ukiona vile ujue ni mpenzi wa JF na anaona JF kama nyumbani na mimi na wewe tunakuwa marafiki zake wakuu. Pole ndugu mwenyezi mungu akupe nguvu na jasiri hasa wakati huu mgumu si kwako tu bali hata kwetu maswahiba wako wa JF
 
Kuna mama moja alikuwa anawanyima amani sana watu kwenye misiba kwa utani wake unaoelekea kwenye ukweli, sijui nguo za marehemu alikuwa anazipata vipi anavaa na kumuigiza, kuna siku mfiwa mmoja alimzaba vibao vya maana tu watu walimlaumu sana lakini ilisaidia sana kumbadili yule mama siku hiizi ametulia sana.

Utani umekuwa ukitumika kuumiza zaidi wafiwa na si kufariji. Hauna maana ufutwe!
 
Pole mkuu, Mwenyezi Mungu awape wepesi katika wakati huu mgumu....
 
R.I.P. mama ijozi.!
 
Last edited by a moderator:
Inavyoonesha huyu mfiwa yuko dar thts why anasema anajiandaa kusafiri kwenda mkoani kuzika, sion ubaya wa yeye kutoa taarifa ya msiba thr jf, sidhani kama anaweza kufanya utani kwa jambo kama hili.

Pole kwa kufiwa mpendwa
R.I.P our mummy

Akili timamu ndiyo haswa niliyoitumia katika kuhoji kwangu.

Mimi nilifiwa na mdingi miezi kadhaa iliyopita na JF haikuwepo hata kwenye mawazo yangu!

Siku hiyo nilikuwa mwenye simanzi nyingi, purukushani za maandalizi ya mazishi, pamoja na shughuli zingine zihusuzo msiba.

Ndiyo niifikirie JF? SMFH.
 
Ni wazi kifo hakizoeleki pole sana mungu wa mbinguni akujaalie nguvu uweze kushiriki maziko salama pole sana ndugu
 
Pole sana kwa kuondokewa na mzazi wako. yote ni mapito.
 
Back
Top Bottom