Tanzia: Mama yangu mzazi ameaga dunia

Tanzia: Mama yangu mzazi ameaga dunia

pole sana kaka kwa kufikwa na hayo mazito. Mungu akutie nguvu, ila kaka kwa tamaduni zetu za africa kidogo nashangaa uko online unafanya nini muda huu mtu uliyefiwa na mzazi. kwangu mimi naona ajabu.

kwahiyo ulitaka apige mayowe na kugaragara chini kwenye basi ili watu wajue kuwa anamajonzi?
Wakati mwingine tuweni wastaarabu katika mambo kama haya ijoz anahaki kabisa kuingia mtandaoni na kutujuza sisi kama rafiki zake ilituweze kumfariji katika kipindi hiki kigumu na si kumvunja moyo kama wewe na nyani ngabu mlivyofanya.
 
Wadau,kwa huzuni na majonzi makubwa nasikitika kuwajulisha kuwa mama yangu mzazi ameaga dunia majira ya saa tatu na nusu usiku wa tar. 29/04/2013
Ikumbukwe kuwa mnamo tar. 17/03/ mwaka huu niliandika post ya kumbukumbu ya miaka miwili ya kifo cha baba yangu mpendwa.
Leo tena naanza safari nyingine ya maisha ya kumkosa mama.
Huzuni niliyonayo moyoni haielezeki wapendwa.
Kinachoniumiza zaidi ni kuwa alilazwa J'pili ya tar 28/4,siku ya pili nikaweza kuzungumza naye kwa kupitia simu,akanieleza yupo kwenye drip ya pili kati ya tatu,na anakula vizuri,isipokuwa anajisikia uchovu wa homa.
Ilinipa faraja kuwa ndani ya siku mbili atarejea kuendelea na shughuli zake. Mida ya saa tatu nikajulishwa pia kuwa anaendelea vyema.
Lakini ndo hivyo tena,baadae nikajulishwa taarifa hii iliyonifanya nishindwe kuvumilia kulia.
Hapa najiandaa nisafiri asubh hii kwenda mkoani kuzika.
Nimejitahidi kuwaandikia,mshirikiane nami kwa maombi.
Nashindwa kupata neno zuri kuelezea huzuni yangu wapendwa. Inauma kupoteza wazazi,inauma zaidi kupoteza katika mazingira usiyotarajia.
pole ndugu yangu kipenzi pole sana niilimpoteza mama yangu 1999 ila naona ni sawa na jana aisee wacheni tu.mpaka leo sijaweza mthamini mwanamke mwingine yyte na kumfananisha na mamayangu.nakumbuka nilikuwa mdogo niliacha kuingia form1 special school niliyochaguliwa nikaenda soma day school ili niwe namwona nakumuuguza mama yangu aisee nilimpenda sana ila mungu alimpenda zaidi ,ila tr 05/09/1999 saa 09.08 na sekunde 43 alinifia mikononi aisee nilibaki namwamsha hata kelele hatukupiga mpaka asubuhi lol wacheni pole sana mkuu najua unapopitia .babab/mama wa mtu huwezi mfananisha na kitu chochote!!
 
pole sana mkuu, je haya maelezo ulikuwa umeyaandaa kabisa umefanya kupaste tu maana wengine huwa tunaishiwa maneno lakini wewe ulivyo pangingilia kwa uzuri..
 
Pole sana! Kua na subira ndo hali ya dunia


Sent from my EyePhone
 
Akili timamu ndiyo haswa niliyoitumia katika kuhoji kwangu.

Mimi nilifiwa na mdingi miezi kadhaa iliyopita na JF haikuwepo hata kwenye mawazo yangu!

Siku hiyo nilikuwa mwenye simanzi nyingi, purukushani za maandalizi ya mazishi, pamoja na shughuli zingine zihusuzo msiba.

Ndiyo niifikirie JF? SMFH.
ulikumbuka kuwataarifu ndugu wengine!!au ulifanya kila kitu peke yako,sidhani kama kuwajulisha ndugu na marafiki walio karibu utasahau muda wote!!amekumbuka kuwa ana ndugu na marafiki Jfs ndo akatujulisha!!!!pole bwana uliyefiwa.
 
Pole sana mkuu na Mungu akupe wepes na faraja wewe na wafiwa wengine hii pia itufundishe kuwa dunia sote tuwaptaji tu hakuna atayebaki tuzdi kumjua Mungu wapendwa!!
(ila hili neno TANZIA si huwa linamaanisha habar zisizo rasmi/tetes? Wajuz wa lugha tafadhali natanguliza saman lkn)
 
wadau,kwa huzuni na majonzi makubwa nasikitika kuwajulisha kuwa mama yangu mzazi ameaga dunia majira ya saa tatu na nusu usiku wa tar. 29/04/2013
ikumbukwe kuwa mnamo tar. 17/03/ mwaka huu niliandika post ya kumbukumbu ya miaka miwili ya kifo cha baba yangu mpendwa.
Leo tena naanza safari nyingine ya maisha ya kumkosa mama.
Huzuni niliyonayo moyoni haielezeki wapendwa.
Kinachoniumiza zaidi ni kuwa alilazwa j'pili ya tar 28/4,siku ya pili nikaweza kuzungumza naye kwa kupitia simu,akanieleza yupo kwenye drip ya pili kati ya tatu,na anakula vizuri,isipokuwa anajisikia uchovu wa homa.
Ilinipa faraja kuwa ndani ya siku mbili atarejea kuendelea na shughuli zake. Mida ya saa tatu nikajulishwa pia kuwa anaendelea vyema.
Lakini ndo hivyo tena,baadae nikajulishwa taarifa hii iliyonifanya nishindwe kuvumilia kulia.
Hapa najiandaa nisafiri asubh hii kwenda mkoani kuzika.
Nimejitahidi kuwaandikia,mshirikiane nami kwa maombi.
Nashindwa kupata neno zuri kuelezea huzuni yangu wapendwa. Inauma kupoteza wazazi,inauma zaidi kupoteza katika mazingira usiyotarajia.

mungu akupiganie katika kipindi hiki kigumu.
 
Pole sana mkuu.Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu
 
I consider this ni utani wa kimakabila tulionao watanzania hasa mtu anapofiwa ili kumfanya angalau apunguze machungu.

Hakuna kitu ninachokichukia kama utani wakati wa msiba; sioni sababu ya maana ya utani. Watu wanadiriki hata kuwamwagia maji wafiwa eti utani loh!

Ijoz pole kwa msiba
 
Pole sana kwa kufiwa na mama yako kipenzi. Mungu amlaze mahali pema peponi na pia awape nguvu katika kipindi hiki kigumu sana. Amina
 
Akili timamu ndiyo haswa niliyoitumia katika kuhoji kwangu.

Mimi nilifiwa na mdingi miezi kadhaa iliyopita na JF haikuwepo hata kwenye mawazo yangu!

Siku hiyo nilikuwa mwenye simanzi nyingi, purukushani za maandalizi ya mazishi, pamoja na shughuli zingine zihusuzo msiba.

Ndiyo niifikirie JF? SMFH.

Nyani ngabu unatoa experience yako ambayo inatofautiana na watu wengine. Uwezo wa ku handle situation kama hizi zinatofautiana kati ya mtu na mtu hivyo usishangae wengine hata baa huwa wanakwenda. Ninavyoelewa mtoa mada anatueleza tumpe maneno ya faraja.
 
pole sana ndugu, tupo nawe pamoja katika kipindi hiki kigumu.
 
Hakuna kitu ninachokichukia kama utani wakati wa msiba; sioni sababu ya maana ya utani. Watu wanadiriki hata kuwamwagia maji wafiwa eti utani loh!

Ijoz pole kwa msiba
Ndio mila zetu mkuu. unapaswa kuzidumisha.
 
Back
Top Bottom