Tanzia: Mama yangu mzazi ameaga dunia

Tanzia: Mama yangu mzazi ameaga dunia

Wadau,kwa huzuni na majonzi
makubwa nasikitika kuwajulisha kuwa mama yangu mzazi ameaga dunia majira
ya saa tatu na nusu usiku wa tar. 29/04/2013
Ikumbukwe kuwa mnamo tar. 17/03/ mwaka huu niliandika post ya kumbukumbu
ya miaka miwili ya kifo cha baba yangu mpendwa.
Leo tena naanza safari nyingine ya maisha ya kumkosa mama.
Huzuni niliyonayo moyoni haielezeki wapendwa.
Kinachoniumiza zaidi ni kuwa alilazwa J'pili ya tar 28/4,siku ya pili
nikaweza kuzungumza naye kwa kupitia simu,akanieleza yupo kwenye drip ya
pili kati ya tatu,na anakula vizuri,isipokuwa anajisikia uchovu wa
homa.
Ilinipa faraja kuwa ndani ya siku mbili atarejea kuendelea na shughuli
zake. Mida ya saa tatu nikajulishwa pia kuwa anaendelea vyema.
Lakini ndo hivyo tena,baadae nikajulishwa taarifa hii iliyonifanya
nishindwe kuvumilia kulia.
Hapa najiandaa nisafiri asubh hii kwenda mkoani kuzika.
Nimejitahidi kuwaandikia,mshirikiane nami kwa maombi.
Nashindwa kupata neno zuri kuelezea huzuni yangu wapendwa. Inauma
kupoteza wazazi,inauma zaidi kupoteza katika mazingira
usiyotarajia.
R.I.P mama pole ijoz
 
Mwenyezi Mungu mwingi rehema awatangulie katika kumpumzisha mama yetu mpendwa aliyetangulia mbele ya haki na yeye mwenyewe aliyemuita ampe pumziko la milele, Amina.
 
pole sana mkuu mungu amlaze mahali pema mama na pia akupe wewe na familia faraja
 
kazi yake Mola haina makosa. Pole sana mkuu Mungu akulinde na kukuongoza katika kipindi hiki kigumu.
 
Pole sana kwa kipindi kigumu...Mungu akutie nguvu na ujasiri na pia akupe faraja.
Sisi sote ni udongo na mavumbini tutarudi. Amen
 
pole sana ndugu yetu kwa kupoteza mtu muhimu. RIP mama
 
Mungu akupe faraja na akuinulie watu ambao watakusaidia kuzoea yaliyotokea!!Msalaba mbele,Dunia nyuma..Mungu ampe pumziko jema la milele

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
mwenyezi mungu akutulize, akulinde na kukuongoza katika kipindi hiki kigumu, tupo pamoja
 
pole sana Ijoz
jipe nguvu kama ilivo avatar yako
cha kujiuliza sisi tutafika miaka yake?
 
Mkuu pole sana!Mwenyezi Mungu akupe moyo wa uvumilivu ktk kipindi hiki kigumu, tuko pamoja ktk sala mkuu! R.I.P mama!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Akili timamu ndiyo haswa niliyoitumia katika kuhoji kwangu.

Mimi nilifiwa na mdingi miezi kadhaa iliyopita na JF haikuwepo hata kwenye mawazo yangu!

Siku hiyo nilikuwa mwenye simanzi nyingi, purukushani za maandalizi ya mazishi, pamoja na shughuli zingine zihusuzo msiba.

Ndiyo niifikirie JF? SMFH.

Binadamu tunatofautiana
 
Mwache apumzike maana matendo yake yamefuatana naye. Asubuhi ile atakapokuja mwana wa Adam atafufuliwa kwa ajiri ya hukumu, kama alitenda mema atavuna ktk wema na kama alitenda mabaya atavuna katika hayo aliyoyatenda.
Ni MUDA WAKO KUTENDA MEMA KWAKO WEWE UNAYEJIANDAA KUFA SIKU MOJA.
 
Pole sana mkuu. Pole kwa familia yote. Mungu atawapigania katika kipindi hiki cha majaribu.
Mungu awape nguvu ili muwe na uwezo wa kumzika mama mpendwa.

Nyani Ngabu umesikitisha na kushangaza umma. Ila inawezekana huo mtazamo wako binafsi kwa hiyo sina nafasi ya kukufikiria vinginevyo.
 
Mungu Mwenyezi akupe faraja iliyo kuu katika kipindi hiki kigumu!! Pole sana sana
 
Wadau,kwa huzuni na majonzi makubwa nasikitika kuwajulisha kuwa mama yangu mzazi ameaga dunia majira ya saa tatu na nusu usiku wa tar. 29/04/2013
Ikumbukwe kuwa mnamo tar. 17/03/ mwaka huu niliandika post ya kumbukumbu ya miaka miwili ya kifo cha baba yangu mpendwa.
Leo tena naanza safari nyingine ya maisha ya kumkosa mama.
Huzuni niliyonayo moyoni haielezeki wapendwa.
Kinachoniumiza zaidi ni kuwa alilazwa J'pili ya tar 28/4,siku ya pili nikaweza kuzungumza naye kwa kupitia simu,akanieleza yupo kwenye drip ya pili kati ya tatu,na anakula vizuri,isipokuwa anajisikia uchovu wa homa.
Ilinipa faraja kuwa ndani ya siku mbili atarejea kuendelea na shughuli zake. Mida ya saa tatu nikajulishwa pia kuwa anaendelea vyema.
Lakini ndo hivyo tena,baadae nikajulishwa taarifa hii iliyonifanya nishindwe kuvumilia kulia.
Hapa najiandaa nisafiri asubh hii kwenda mkoani kuzika.
Nimejitahidi kuwaandikia,mshirikiane nami kwa maombi.
Nashindwa kupata neno zuri kuelezea huzuni yangu wapendwa. Inauma kupoteza wazazi,inauma zaidi kupoteza katika mazingira usiyotarajia.

Pole mjf mungu akupe nguvu za kukabiliana na kipindi kigumu kama hiki.
 
Back
Top Bottom