Tanzia: Mama yangu mzazi ameaga dunia

Tanzia: Mama yangu mzazi ameaga dunia

ijoz

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
731
Reaction score
718
Wadau,kwa huzuni na majonzi makubwa nasikitika kuwajulisha kuwa mama yangu mzazi ameaga dunia majira ya saa tatu na nusu usiku wa tar. 29/04/2013. Ikumbukwe kuwa mnamo tar. 17/03/ mwaka huu niliandika post ya kumbukumbu ya miaka miwili ya kifo cha baba yangu mpendwa.

Leo tena naanza safari nyingine ya maisha ya kumkosa mama. Huzuni niliyonayo moyoni haielezeki wapendwa. Kinachoniumiza zaidi ni kuwa alilazwa J'pili ya tar 28/4,siku ya pili nikaweza kuzungumza naye kwa kupitia simu,akanieleza yupo kwenye drip ya pili kati ya tatu,na anakula vizuri,isipokuwa anajisikia uchovu wa homa.

Ilinipa faraja kuwa ndani ya siku mbili atarejea kuendelea na shughuli zake. Mida ya saa tatu nikajulishwa pia kuwa anaendelea vyema. Lakini ndo hivyo tena,baadae nikajulishwa taarifa hii iliyonifanya nishindwe kuvumilia kulia. Hapa najiandaa nisafiri asubh hii kwenda mkoani kuzika.

Nimejitahidi kuwaandikia,mshirikiane nami kwa maombi. Nashindwa kupata neno zuri kuelezea huzuni yangu wapendwa. Inauma kupoteza wazazi,inauma zaidi kupoteza katika mazingira usiyotarajia.
 
Pole sana Mkuu kwa msiba mkubwa uliokufika. Mwenyezi Mungu akupe nguvu na faraja wewe na wafiwa wengine katika kipindi hiki kigumu kwenu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN
 
Pole sana mkuu, Mungu akuongoze katika kipindi hiki kigumu.
 
Embu kuwa binadamu mwenye akili timamu
Kafiwa akufiwa yeye anatupasha yaliyo mfika muhimu kwetu kumpa pole hakuna la zaidi
Sasa mtu akifiwa atakiwi kuwaambia marafiki zake anaokutana nao kila wakati kwenye mitandao


(Mkuu pole sana ndio kazi ya mungu)

​

Akili timamu ndiyo haswa niliyoitumia katika kuhoji kwangu.

Mimi nilifiwa na mdingi miezi kadhaa iliyopita na JF haikuwepo hata kwenye mawazo yangu!

Siku hiyo nilikuwa mwenye simanzi nyingi, purukushani za maandalizi ya mazishi, pamoja na shughuli zingine zihusuzo msiba.

Ndiyo niifikirie JF? SMFH.
 
Pole sana mfiwa!

Nyani Ngabu tumpe maneno ya kumfariji mwenzetu na tumpe nguvu ayaweze maswahibu haya!Maneno kama hayo yako kumsimanga mfiwa kwa sababu tu katumia haki yake ya msingi tena ya kikatiba ya kipashana habari HAYANA NAFASI kwa sasa

Pole sana ndugu yetu!
 
Pole sana ndugu. Wanasema ndo ukubwa huo. Jipe moyo mkuu, kwa sababu ukivunjika moyo utashindwa kumsherehekea mama kwa safari yake ya mwisho. Maybthe good memories give you strength to go on.
 
Omayu, acha basi huo utani wa kinyantuzu. Ninajua hata huko shy watu wakifiwa hutoa taarifa kwa majirani, ndugu na jamaa. Sioni ubaya wowote yeye akitoa taarifa kwa jamaa zake wa jf.
Pole sana ndugu yetu kwa msiba uliokukuta. Bwana akufariji wewe pamoja na familia.
Nimekuombea.
 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Ni safari katika maisha. Shukuru kwa kupata hiyo nafasi ya kumsindikiza kwenye malalo ya milele. Amen.
 
ijoz

Pole sana Best wetu! Hakika ni wakati mgumu sana katika kipindi hiki ila jipe moyo kwani hakika tu MUNGU aliye hai na hata sasa!

Mwenyenzi MUNGU Baba wetu mwenye mamlaka Mbinguni na Duniani tunakuomba umpe Mama yetu pumziko la milele shambani mwako Bwana wetu! Amen!

Nyani Ngabu
Kwa kweli sijaipenda post yako No 3 na sikutegemea kauli kama hii toka kwa member kama wewe!

Angalia kauli yako!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana ijoz. Mungu akutie nguvu, faraja na utulivu katika kumsindikiza mama mpendwa. Hiyo ni njia yetu sote, mshukuru Mungu.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Mungu akutie nguvu kwenye kipindi hiki kigumu cha majonzi
 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Ni safari katika maisha. Shukuru kwa kupata hiyo nafasi ya kumsindikiza kwenye malalo yamilele. Amen

mahalapema huwawapikweli, na inapatikana ktk andikogani?. naulizatu
 
Pole sana kiongozi , Mungu awape faraja kipindi hichi kigumu .
 
Pole Sana Kwa Kufiwa Na Mama Yako Mzazi! Tuko Nawe Ktk Sala Kipindi Hiki Kigumu! RIP MAMA
 
pole sana mwenyezi awape faraja na nguvu katika kipindi kigumu roho ya marehemu mama yetu ipumzike kwa amani Amina
 
Back
Top Bottom