Mbele ya Waziri Mkuu, Mzazi afikisha malalamiko ya mwanae kutekwa na Waliojitambulisha kuwa ni Polisi

Mbele ya Waziri Mkuu, Mzazi afikisha malalamiko ya mwanae kutekwa na Waliojitambulisha kuwa ni Polisi

Mbabani

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2022
Posts
2,464
Reaction score
7,043
Ni huzuni kwa kweli, mwanamke mmoja huko Itigi - Singida ameeleza kwa uchungu mtoto wake alivyokamatwa na polisi wakamfunga pingu kisha kutokomea nae, mzazi wa mtoto huyo alifatilia kituo cha polisi bila mafanikio ya kumuona mwanae, ni siku 40 zimepita hajui mtoto wake alipo.

Ameyaeleza hayo mbele ya waziri mkuu Mwigulu Nchemba 31/05/2026.

Nchemba amemtaka RPC achukue maelezo ya yule mama, sasa je ni maelezo gani mapya atawapa polisi ili hali alishafatilia sana huko polisi bila mafanikio yoyote?

Watekaji wanatoa wapi pingu?

======

Bibi: Mimi kwa majina naitwa Joyce Abel, nimetoka Manyoni. Tangu tarehe 21 mwezi wa nne walikuja watu wengine wawili...

Waziri Mkuu: Wapi?

Bibi: Nyumbani kwangu majengo Manyoni.

Waziri Mkuu: Ehe.

Bibi: Wakaniambia wao ni maaskari.

Waziri Mkuu: Ehe.

Bibi: Wakamchukua mtoto wangu, kijana wangu ambaye ana miaka 32 tangu tarehe 21 mwezi wa nne. Hiyo hiyo siku ya tarehe 21 mwezi wa nne, nikaondoka nikafuatia kwanza nikawauliza, amekosa nini? Wakaniambia wewe mama rudi ndani. Jamani amefanyaje? Tulikuta tumekaa sebuleni, tuko wote na baba yake na mke wake na mimi, tumekaa tu mchana saa 9 mchana. Wakasema, "Sisi ni maaskari."

Wakawa wamemshika mabegani na kuanza kumtoa. Nikawaambia jamani anakosa gani? Wakasema, wakanisukuma "Mama nenda ndani." Walikuwa vijana wawili. Kuja kuchungulia nje hivi, nje kwa uwanjani kwangu nikaona askari amesimama, amevaa sare (uniform), amebeba na bunduki. Nikasogea, nikasema, "Jamani amekosa nini mwanangu?" Yule askari akanisukuma, "Mama ludi... ludi ndani." Nitarudije ndani bila kujua hatima ya mwanangu na amekosa nini? Si mniambie? Hawakusema.

Hawakunijibu, niliuliza mpaka mara tatu, wanaendelea kuniambia, "Mama rudi ndani." Basi, kuja kuangalia gari lilikuwa limepaki nyumbani kwenye mlango wa fensi (fence) yangu ya nyumba, wakafika hapo kwenye mlango wamemshika hivi, wanamvuta, wanampeleka kwenye gari. Wakafika wakamfunga pingu, wakamsukumiza kwenye gari, gari yenyewe ilikuwa ya kuluzu (cruise) nyeupe, wakamgongesha mlango wa nyuma, wakafunga mlango, wakaanza kuwaita wale wenzao ambao walikuwepo ndani, ambao walitangulia kama wanauza mashuka.

Na mashuka nilinunua. Walifanya kama hao wamachinga wanauza nguo, nikanunua mashuka matatu. Basi, wakaitana wote, "Twendeni twendeni!" Wakaingia kwenye gari, wakawasha gari, wakakimbia wakaenda. Mimi nikafuata...

Waziri Mkuu: Na taarifa hizo umezifikisha wapi?

Bibi: Kituoni polisi Manyoni. Nilipoenda kituoni, wakasema sisi hakuna mtu aliyeletwa hapa. Nikarudi. Kesho yake tena nikaenda, wakasema, "Mama, tunakwambia hakuna, hebu twende tukupeleke mahabusu." Wakanipeleka kuita watu jina la mwanangu, hakuna mwanangu hakuitika hapo. Wakanipeleka juu ghorofani kuita jina la mwanangu, hakuna hakaitika.

Nikashuka. Wakaniambiaje? "Rudi mama, ngoja tufanye upelelezi." Sasa nikawa tu nikikaa nikienda, "Jamani mwanangu vipi upelelezi umefanyika?" Wananambia, "Bado." Siku zingine nawakuta hawako, siku zingine wananiambia, "Mama rudi bado." Basi, mpaka hivi sasa leo ni siku ya 40, sijui mwanangu aliko na yuko hai na yuko wapi, hata sijiui. Nalia kila siku mimi... nalia mwanangu... mwanangu sijui yuko wapi...

Waziri Mkuu: Haya nimekusikia. Kamanda wa Polisi... Kamanda wa Polisi hebu sogea hapa mchukue huyu mama, alafu pata hizo dondoo (details) alafu... hebu akueleze hizo taarifa zake. Ili tujue ni... ni mmefuatilia mmejua ni nini hicho.

Pia soma: PostGE2025 - CCM Hatimaye yachukizwa na utekaji! Yaumizwa na yaliyotokea Oktoba 29, Balozi Migiro ateta na Kikeke
 
Ni huzuni kwa kweli, mwanamke mmoja huko Itigi - Singida ameeleza kwa uchungu mtoto wake alivyokamatwa na polisi wakamfunga pingu kisha kutokomea nae, mzazi wa mtoto huyo alifatilia kituo cha polisi bila mafanikio ya kumuona mwanae, ni siku 40 zimepita hajui mtoto wake alipo.

Ameyaeleza hayo mbele ya waziri mkuu Mwigulu Nchemba 31/05/2026.

Nchemba amemtaka RPC achukue maelezo ya yule mama, sasa je ni maelezo gani mapya atawapa polisi ili hali alishafatilia sana huko polisi bila mafanikio yoyote?

Watekaji wanatoa wapi pingu?
Huyo dogo atakuwa ana issue ya mgogoro wa mapenzi au betting.
cc:RPC Singida aione kwenye jalada ili kutowachosha askari wake na mambo ya kujitekateka.
 
Ni huzuni kwa kweli, mwanamke mmoja huko Itigi - Singida ameeleza kwa uchungu mtoto wake alivyokamatwa na polisi wakamfunga pingu kisha kutokomea nae, mzazi wa mtoto huyo alifatilia kituo cha polisi bila mafanikio ya kumuona mwanae, ni siku 40 zimepita hajui mtoto wake alipo.

Ameyaeleza hayo mbele ya waziri mkuu Mwigulu Nchemba 31/05/2026.

Nchemba amemtaka RPC achukue maelezo ya yule mama, sasa je ni maelezo gani mapya atawapa polisi ili hali alishafatilia sana huko polisi bila mafanikio yoyote?

Watekaji wanatoa wapi pingu?
Kuna miaka itigi ilitisha kwa majambazi/
No more talks!...
 
Ni huzuni kwa kweli, mwanamke mmoja huko Itigi - Singida ameeleza kwa uchungu mtoto wake alivyokamatwa na polisi wakamfunga pingu kisha kutokomea nae, mzazi wa mtoto huyo alifatilia kituo cha polisi bila mafanikio ya kumuona mwanae, ni siku 40 zimepita hajui mtoto wake alipo.

Ameyaeleza hayo mbele ya waziri mkuu Mwigulu Nchemba 31/05/2026.

Nchemba amemtaka RPC achukue maelezo ya yule mama, sasa je ni maelezo gani mapya atawapa polisi ili hali alishafatilia sana huko polisi bila mafanikio yoyote?

Watekaji wanatoa wapi pingu?

Kesi ya nyani
 
Hayo ndo maarifa mliyobakiwa nayo nyie Millennials.
Kwanza hata wewe mwenyewe wa hovyoo!!!!

Bisha!
Sawa nyie chadema wajuzi, but can't leaves our country to 🐕get know this,and shut ya 😺
 
Back
Top Bottom