Tanzia: Mama yangu mzazi ameaga dunia

Tanzia: Mama yangu mzazi ameaga dunia

Pole sana Mungu akupe nguvu na awe faraja kwako katika kipindi kigumu ulichonacho. .Ila amini kuwa ni mpango wake na akishapanga hakuna wa kupangua,mshukuru kwa kila jambo. .BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE!
 
''Sisi Sote Ni Wa Allah Na Sote Tutarejea Kwake'', Allah Ailaze Roho Yake Mahali Pema Peponi. Amin. Pole sana ndugu...
 

Pole Sana. M.Mungu Awaongoze Katika Kipindi Hiki Kigumu. Amina.

Steve Dii

 
Wadau,kwa huzuni na majonzi makubwa nasikitika kuwajulisha kuwa mama yangu mzazi ameaga dunia majira ya saa tatu na nusu usiku wa tar. 29/04/2013
Ikumbukwe kuwa mnamo tar. 17/03/ mwaka huu niliandika post ya kumbukumbu ya miaka miwili ya kifo cha baba yangu mpendwa.
Leo tena naanza safari nyingine ya maisha ya kumkosa mama.
Huzuni niliyonayo moyoni haielezeki wapendwa.
Kinachoniumiza zaidi ni kuwa alilazwa J'pili ya tar 28/4,siku ya pili nikaweza kuzungumza naye kwa kupitia simu,akanieleza yupo kwenye drip ya pili kati ya tatu,na anakula vizuri,isipokuwa anajisikia uchovu wa homa.
Ilinipa faraja kuwa ndani ya siku mbili atarejea kuendelea na shughuli zake. Mida ya saa tatu nikajulishwa pia kuwa anaendelea vyema.
Lakini ndo hivyo tena,baadae nikajulishwa taarifa hii iliyonifanya nishindwe kuvumilia kulia.
Hapa najiandaa nisafiri asubh hii kwenda mkoani kuzika.
Nimejitahidi kuwaandikia,mshirikiane nami kwa maombi.
Nashindwa kupata neno zuri kuelezea huzuni yangu wapendwa. Inauma kupoteza wazazi,inauma zaidi kupoteza katika mazingira usiyotarajia.

pole mkuu
 
Pole sana ndugu yangu Najua uko kwenye wakati mgumu sana ktk maisha yako kuondokewa na wazazi si jambo rahisi,nakuombea faraja,mungu wa mbinguni akujalie faraja yake na akutie nguvu za kustahimili, pasipo yeye kukusaidia hutaweza ni kipindi kigumu mno,poleeeee saaaaana ndugu yangu
 
Pole sana ndugu na tuko pamoja katika kipindi hiki kigumu!tunamuombea apumzike mahala pema peponi.Amiin
 
Back
Top Bottom