Tanzia: Mama yangu mzazi ameaga dunia

Tanzia: Mama yangu mzazi ameaga dunia

Duh what a loss jamani can only imagine what u r going through..kama mwanaume jipe moyo ndo ivo maisha yalivy o...Mungu amlaze mahali pema Amen..
 
Mkuu ijoz pole sana,
Maandiko matakatifu yanasema "Hapa hatuna mji udumuo bali twautumainia ule ujao" mama yako amelala tu, kuna siku ataamka, fanya kama vile kuna mahali amekwenda kuna siku atarudi, hata hivyo mmeachana kwa muda tu, kuna siku mtakutana tena! Mungu ampe Pumziko la milele, na mwanga wa amani amwangazie, pole sana mkuu.
‪Fanuel Sedekia - Nishike Mkono‬‏ - YouTube
NB: UNGEWEKA WAZI LOCATION YA MSIBA INGEKUWA POA SANA KUNA WANA-JF WENZAKO WANGEKU-JOIN KWENYE KUMSINDIKIZA MAMA KATIKA SAFARI YAKE YA MWISHO.
 
Mkuu pole sana, ila jipe moyo...tumeumbiwa binadamu. Na mauti hayana dawa ndo'maana hufikia hatua kizuri uaharibika/kufa na kupotea. Mwenyezi Mungu akupe nguvu na faraja hasa kipindi hiki.
MAY HER SOUL REST IN PEACE AND PERPETUAL ETENAL LIGHTH SHINES UPON HER.
 
Pole sana mkuu, MUNGU akutie nguvu na ujasiri wa kuikubali hali hii ngumu..
 
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe. Ndugu jipe moyo mkuu hayo ni mapenzi ya Mungu ambayo hakuna binadamu mwenye kuyazuia. Sote tutapita njia hiyo kwa kila mtu kwa zamu yake. Pole sana!
 
Pole sana Mungu ni mwema hata Sasa ni mwema songa mbele ndugu yangu
 
Pole sana mkuu!
Mungu awape nguvu katika wakati huu mgumu...
Kilichobaki ni sisi pia kujiandaa coz we are at the same journey..
R. I. P mama ijoz
 
Last edited by a moderator:
Wadau,kwa huzuni na majonzi
makubwa nasikitika kuwajulisha kuwa mama yangu mzazi ameaga dunia majira
ya saa tatu na nusu usiku wa tar. 29/04/2013
Ikumbukwe kuwa mnamo tar. 17/03/ mwaka huu niliandika post ya kumbukumbu
ya miaka miwili ya kifo cha baba yangu mpendwa.
Leo tena naanza safari nyingine ya maisha ya kumkosa mama.
Huzuni niliyonayo moyoni haielezeki wapendwa.
Kinachoniumiza zaidi ni kuwa alilazwa J'pili ya tar 28/4,siku ya pili
nikaweza kuzungumza naye kwa kupitia simu,akanieleza yupo kwenye drip ya
pili kati ya tatu,na anakula vizuri,isipokuwa anajisikia uchovu wa
homa.
Ilinipa faraja kuwa ndani ya siku mbili atarejea kuendelea na shughuli
zake. Mida ya saa tatu nikajulishwa pia kuwa anaendelea vyema.
Lakini ndo hivyo tena,baadae nikajulishwa taarifa hii iliyonifanya
nishindwe kuvumilia kulia.
Hapa najiandaa nisafiri asubh hii kwenda mkoani kuzika.
Nimejitahidi kuwaandikia,mshirikiane nami kwa maombi.
Nashindwa kupata neno zuri kuelezea huzuni yangu wapendwa. Inauma
kupoteza wazazi,inauma zaidi kupoteza katika mazingira
usiyotarajia.

Pole sana manafamilia mwenzetu, Mungu akupe nguvu na ujasiri ukipite hiki kipindi kigumu. R.I.P mama mpendwa:
 
Pole sana mkuu. Kweli ni majonzi na huzuni kubwa. Lakini kwa uwezo wa Mungu utayashinda

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Akili timamu ndiyo haswa niliyoitumia katika kuhoji kwangu.

Mimi nilifiwa na mdingi miezi kadhaa iliyopita na JF haikuwepo hata kwenye mawazo yangu!

Siku hiyo nilikuwa mwenye simanzi nyingi, purukushani za maandalizi ya mazishi, pamoja na shughuli zingine zihusuzo msiba.

Ndiyo niifikirie JF? SMFH.


Pole sana kwa msiba mkubwa uliokufika. Mungu aware moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na mama mzazi.

Nyani Ngabu, Binadamu tunatofautiana sana kwa majina mpaka matendo na jinsi ya kukabiliana na majanga.
 
Mungu awatie nguvu na kuwafariji katika kipindi hiki cha majonzi.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mungu ailaze roho ya marehemu
mahala pema peponi. Ni safari katika maisha. Shukuru kwa kupata hiyo
nafasi ya kumsindikiza kwenye malalo ya milele. Amen.

pole sana rip ur mum!!
 
Back
Top Bottom