Tanzia: Mama yangu mzazi ameaga dunia

Tanzia: Mama yangu mzazi ameaga dunia

Pole sana na mwenyezi Mungu akutie nguvu katika kipind hiki kigumu!
 
pole sana kaka kwa kufikwa na hayo mazito. Mungu akutie nguvu, ila kaka kwa tamaduni zetu za africa kidogo nashangaa uko online unafanya nini muda huu mtu uliyefiwa na mzazi. kwangu mimi naona ajabu.
 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi......pole ndugu....ila kuwa na furaha, ameenda kutana na mpenzi wake aliyetengana naye miaka miwili iliyopita....na siku zijazo, nanyi mtaenda na kukutana nao..na mtakuwa familia moja kwa mara nyingine....Mungu awafariji sana katika kipindi hiki kigumu cha kukubali safari ya mama yako...ila muwe na furaha...Mungu anasema, "kila jambo lina wakati wake, na makusudi yake chini ya mbingu"...hivyo kuwa na amani ya moyo..na ukauhifadhi mwili wa mama sehemu nzuri na kwa amani.....
 
Mungu awape faraja na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu...RIP Mama
 
Umefiwa na mama yako mzazi muda wa kuingia JF unautoa wapi wewe?
Ukitaka kujua tabia za mtu usihangaike, mpe jukwaa aongee, umemaliza!
Wanaosema huu ni utani hakuna kitu cha aina hiyo!...hatujui kabila la mfiwa, so automatically issue ya utani inajiondoa.
JF ni namna ya kuwasiliana just like tutumiavyo midomo yetu, how could somebody pass into this kind of temptation without a word to his/her fellows?
Ngabu's post is sickening.
Poler sana mfiwa, tuko pamoja na wewe!
Mungu amlaze Mama yetu mahala pema!
 
umefiwa na mama yako mzazi muda wa kuingia jf unautoa wapi wewe?

sikujua na wew uko kwenye list ya wale watoto wa kjike wa jangwan wanaojaza ----- humu ndani;polen wafiwa mungu awapenguvu wakati huu mgumu nimepitia hilo na auelezeki uchungu wake ispokuwa mfiwa mwenyewe mungu awapeleke salama na kuwafikisha salama mkuu
 
pole sana kaka kwa kufikwa na hayo mazito. Mungu akutie nguvu, ila kaka kwa tamaduni zetu za africa kidogo nashangaa uko online unafanya nini muda huu mtu uliyefiwa na mzazi. kwangu mimi naona ajabu.

queeny Mkuu:JF NI SEHEMU YA RAHA NA SHIDA SAMAHAMANI KUKWAMBIA HILI NIMEKUTANGULIA KIHESHMA NAJUA JF IN N OUT;NAKUPA HILI NA WEWE HATA UKIFIWA MAOMBI YA WANA JF WACHACHE YATAKUSAIDIA KUMALIZA MSIBA KWA AMANI KULIKO UNAVYOFIKIRIA 2.UNAPOONA MATANGAZO YA MSIBA SMAHAN KWA HILI VYEMA UKAWA MSTAARABU KAMA NYANI NGABU;NAHISI UMEELEWA NAMAANISHA NINI;3:uONAPO MWENZIO AMEKUJA NA HUZUNI ANAITAJI FARAJA NA NDIO MAANA AJAANDIKA BENKI ACCOUNT KAMA WAJIOMBA ZAKO NA SHANGAZ ZAKO WANAPOHUBIRI NENO LAMUNGU NA KUPITISHA ACC ZAO
 
Wadau,kwa huzuni na majonzi makubwa nasikitika kuwajulisha kuwa mama yangu mzazi ameaga dunia majira ya saa tatu na nusu usiku wa tar. 29/04/2013
Ikumbukwe kuwa mnamo tar. 17/03/ mwaka huu niliandika post ya kumbukumbu ya miaka miwili ya kifo cha baba yangu mpendwa.
Leo tena naanza safari nyingine ya maisha ya kumkosa mama.
Huzuni niliyonayo moyoni haielezeki wapendwa.
Kinachoniumiza zaidi ni kuwa alilazwa J'pili ya tar 28/4,siku ya pili nikaweza kuzungumza naye kwa kupitia simu,akanieleza yupo kwenye drip ya pili kati ya tatu,na anakula vizuri,isipokuwa anajisikia uchovu wa homa.
Ilinipa faraja kuwa ndani ya siku mbili atarejea kuendelea na shughuli zake. Mida ya saa tatu nikajulishwa pia kuwa anaendelea vyema.
Lakini ndo hivyo tena,baadae nikajulishwa taarifa hii iliyonifanya nishindwe kuvumilia kulia.
Hapa najiandaa nisafiri asubh hii kwenda mkoani kuzika.
Nimejitahidi kuwaandikia,mshirikiane nami kwa maombi.
Nashindwa kupata neno zuri kuelezea huzuni yangu wapendwa. Inauma kupoteza wazazi,inauma zaidi kupoteza katika mazingira usiyotarajia.



Pole sana mkuu kwa msiba mkubwa uliokupata, MUNGU atawapa faraja yake iliyo kuu kuliko faraja zote za wanadamu.
 
Pole sana kwa msiba huu mzito, Mungu akutie nguvu wewe, familia yako na kila aliyeguswa na msiba huu katika kipindi hiki kigumu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
4:ajaandika mpesa wala tigopesa wala airtell mny means ajakuomba mchango wa kifedha ukiwa kama mwenye hekima ujiulize mfiwa kaweka hili ajaandika sehemu ya kutuma hela unahisi ameomba msaada gan zaidi ya maombi na faraja nasema hivi muwe makini siku nyingine kuacha kuandika utumbo kwenye majonzi hatakama ni watani zenu namshukuru mungu mmekutana na pdidy alieokombolewa na damu ya yesu mngekutana na didy 2yrs ago mngejuta kuandika huu ----- tena mungu awasamehe;mfiwa naomba msamaha kwa niaba ya ndugu zangu queeny na nyan ngabu zidi kuwaombea watakapofikwa nasi tutauliza kuna ngoma huko ama tuje na ngoma zetu msiban
 
Pole sana Mkuu kwa msiba mkubwa uliokufika. Mwenyezi Mungu akupe nguvu na faraja wewe na wafiwa wengine katika kipindi hiki kigumu kwenu
 
Wadau,kwa huzuni na majonzi makubwa nasikitika kuwajulisha kuwa mama yangu mzazi ameaga dunia majira ya saa tatu na nusu usiku wa tar. 29/04/2013Ikumbukwe kuwa mnamo tar. 17/03/ mwaka huu niliandika post ya kumbukumbu ya miaka miwili ya kifo cha baba yangu mpendwa.Leo tena naanza safari nyingine ya maisha ya kumkosa mama.Huzuni niliyonayo moyoni haielezeki wapendwa.Kinachoniumiza zaidi ni kuwa alilazwa J'pili ya tar 28/4,siku ya pili nikaweza kuzungumza naye kwa kupitia simu,akanieleza yupo kwenye drip ya pili kati ya tatu,na anakula vizuri,isipokuwa anajisikia uchovu wa homa.Ilinipa faraja kuwa ndani ya siku mbili atarejea kuendelea na shughuli zake. Mida ya saa tatu nikajulishwa pia kuwa anaendelea vyema.Lakini ndo hivyo tena,baadae nikajulishwa taarifa hii iliyonifanya nishindwe kuvumilia kulia.Hapa najiandaa nisafiri asubh hii kwenda mkoani kuzika.Nimejitahidi kuwaandikia,mshirikiane nami kwa maombi.Nashindwa kupata neno zuri kuelezea huzuni yangu wapendwa. Inauma kupoteza wazazi,inauma zaidi kupoteza katika mazingira usiyotarajia.
Mwenyezi Mungu akutie nguvu kwenye kipindi hiki kigumu, tupo pamoja nawe kwenye sala na maombi.
 
Back
Top Bottom