TANZIA: Afisa wa TAKUKURU auawa

TANZIA: Afisa wa TAKUKURU auawa

Kwamba sasa afisa wa TAKUKURU Bhoke Ryoba ameuawa na "watu wasiojulikana" mbele ya kadamnasi ya watu inaendeleza kile ambacho wengine tumekisema kwa miaka sita sasa - kuna tatizo la msingi la muundo na utendaji katika Usalama wa Taifa.

Ninakumbushia tu.

Kama wajua y? Kauwawa tudadavulie usilete majungu utajishushia hadhi yako?
 
Hili imebekia kuwa taasisi ya kupeleka umbea chama Tawala na kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu. Yeyote atakayeenda kinyume na kujifanya kufata maadili ya kikazi katika UWT basi huyo lazima ashughulikiwe.
 
Kwamba sasa afisa wa TAKUKURU Bhoke Ryoba ameuawa na "watu wasiojulikana" mbele ya kadamnasi ya watu inaendeleza kile ambacho wengine tumekisema kwa miaka sita sasa - kuna tatizo la msingi la muundo na utendaji katika Usalama wa Taifa.

Ninakumbushia tu.
Mkuu Mzee Mwanakijiji,
Kuna "Usalama wa Taifa" chini ya TISS, "Usalama wa Nchi" chini ya JWTZ na "Usalama wa Raia" chini ya Polisi!. As far as usalama wa taifa is concerned, hakuna tatizo lolote!. Taifa ni salama!, nchi pia ni salama!, tatizo kidogo kwenye usalama wa raia!.

Hili tukio la kifo cha ofisa wa Takukuru, hii incident ni "one of" isolated event kama ilivyotokea kwenye kifo cha "Kombe"!, "Prof. Jwan Mwaikusa", "Advocate Kapinga" and many more, that have nothing to do with Usalama wa Taifa, but an individual incidents to silence then just in case!.

Mkuu, nanii, usiwe na wasiwasi, taarifa hii isije kukudisturb katika mapumziko yako hapo "Bilila", hata Othman na Mwamunyange, wote wamejipumzikia, vijana wa Shemaji Mwema wapo bize kazini kuhakikisha kuwa sikukuu hizi za X-mass na Mwaka mpya zinapita salama u salmini na kwa amani, bila kitisho chochote! just relax and enjoy your holiday!.

P.
 
hebu nyamaza!!! Si lazimu kuchangia kila thread wajua?! We unadhani mwandishi wa habari mkongwe kama huyu mzee mwanakijiji hajui majukumu ya usalama wa taifa. Miaka yote aliyokaa daily news bado asijue tu. Kwanza tanzania hakuna usalama wa taifa. Wapo tu mafuska kadhaa pale walevi wakubwa wakijivunia vitambulisho bila ujuzi wowote wa taaluma hiyo nyeti... Intelligence ni taaluma ya accurate data collection for timely decision making. Wanashindwa ku collect data hata zilizo barabarani. Kazi yao kuwaza hela, matiti na pombe tu. Na kama wewe ni mmoja wao achana na mzee mwanakijiji. Kachukue tu allowance yako ya leo kalewe....

Usalama wa taifa ulikufa na nyerere

kuwa mwandishi wa siku nyingi ndo hawezi kuandika maji taka
 
Hakuna tatizo lolote wasi wasi wako tu mbona kumetulia sasa enzi za mzee wa masasi ndio ilikuwa mshike mshike
Mkuu wa idara ya usalama wa taifa kapigwa risasi na kuuwawa na polisi
Kifo cha utata cha baba yetu wa kule butiama
Kifo cha utata cha dr omali ali juma
 
Vyombo vingine vinasema ameuawa na mwenzake. Je, mwenzake hana jina?Wengine muuaji hajulikani. UWT katika mazingira kama haya ni feki. Hapa kuna elementi ya kulindana kama kawaida yenu,hosea, fareshi,na ccm yote.
Hakika hakuna UWT, ila kuna walevi, wazinzi, mafisadi, walinda ufisadi, na waiba kura nyakati za uchaguzi.
 
Siku hizi wamejazana wajomba na watoto wa nyumba ndogo maadili yatatoka wapi? Watu wajinga kabisa ambao tumesoma nao tunawajua eti leo hii na wao ni usalama wakati shuleni walikuwa na tabia mbaya achilia mbali kupata zero. Academic inaweza kuwa sio hoja lakini tabia zao duuuuuuu. Zamani mtu anafuatiliwa tabia toka primary, anakuja sekondary wanamfuatilia.

A level wanaweza mchukua rasmi kama ni exceptional ila kama bado wanataka data zake wanasubiri amalize form six then muda wa jeshini pale ndoo ilikuwa entry point. Na hasa muda wa kuhama kutoka kambi moja kwenda nyingine.

KIBE, Hiyo arrogance imewafanya mfike mlipofika. Mwanakijiji hata kama hajui chochote kuhusu usalama, wewe kama mtu wa usalama unatakiwa kuchukua hoja kama hiyo serious, kwamba inakuwaje watu wa kawaida wanatuhusisha na mauaji? Something must be wrong some where.

Then unatakiwa usome uzi huu wote na ukiwa serious utaokota mawili ili mkikaa myafanyie kazi. Unless mnakuwa serious na mabadiliko jamii inazidi kutokuwaelewa na mnakuewa irrelevant mingoni mwa wanajamii.

Kuhusu majukumu yenu kwataarifa yako zaidi ya asilimia 60 ya wanaJF wanajua kwani jina lenu tu linaweka wazi nini majukumu yenu. Labda nikumbushie jukumu moja ambalo mmelifuta kiaina siku hizi.

Ni kututetea sisi tunaosingiziwa kesi na kufungwa kwasababu hatujui sheria japo makosa hatukufunya. Mkitimiza jukumu hili tu siku ya muungano inatakiwa Kikwete asamehe wafungwa zaidi ya 5000.
 
Kwenye sherehe? na ulifungua usalama risasi iende chemba?

Nilikuwa natoa maelekezo bahati mbaya mwanafunzi aliikoroga usalama ukakwama wakati risasi ipo chemba, hata kuielekeza chini ilikuwa makusudi kuwa endapo itasaidia basi nikatifue vumbi
 
Yule ni sikio la kufa, hata useme namna gani atasikia lakini hawezi kuelewa au kutekeleza lolote!!!!
 
..mshenzi mkubwa huyo!! umewahi kuona bunduki inajipiga!!??? lazima iwekewe risasi, risasi iwekwe kwenye chemba, ifunguliwe usalama na trigger itikiswe ndo risasi ipigwe...uchunguzi wa kina tena wa Polisi na Tiss uhusike hapo!!!!! kuna hujuma...labda jamaa anazuia ulaji wa watu flan flana.:A S angry:
 
Mzee
Mwanakijiji
umeandika too short as if sote tunaelewa hiyo
issue.

Hebu dadavua kidogo kisha tuone Usalama wa Taifa wanahusikaje??? Mbona
hujawalaumu Polisi kwa suala hilo kwa kushindwa kuwakamata hao wahalifu.

Jamaa alikuwa na interest zipi mpaka auwae????

Hayo kwangu nadhani ni maswali ya msingi ninayoyataka mjibu
yake.

mkuu you are a great thinker, JF sasa ivi wamebaki mamburula,
hawataki kujua huyo Bhoke kauwawaje? Alikuwa na nani? Sehemu gani?
Uchunguzi umefikia wapi? Wao wanachojua ni either kulaumu au kusifia kwa kuzingatia mrengo wao wa kisiasa
 
Last edited by a moderator:
kuwa mwandishi wa siku nyingi ndo hawezi kuandika maji taka


Maneno ya Mwanakijiji ni haya hapa chini:Mi sikuona maji taka hapa.

"Kwamba sasa afisa wa TAKUKURU Bhoke Ryoba ameuawa na "watu wasiojulikana" mbele ya kadamnasi ya watu inaendeleza kile ambacho wengine tumekisema kwa miaka sita sasa - kuna tatizo la msingi la muundo na utendaji katika Usalama wa Taifa. Ninakumbushia tu."

Sasa tafakari maneno yaliyo katika Blu na ujiulize ni mara ngapi matukio makubwa yamefanywa hapa Tanzania na yakawa yamefanywa na "watu wasiojulikana." Kesi inayoongelewa inahusu tukio kubwa ambalo limefanywa na watendaji katika Serikali, kuleta maana kuwa kuna criminals wapo ndani ya Serikali ya nchi yetu.

Criminals huwa hawaruhusiwi kufanya kazi katika serikali, na zuwio hili hufanywa na serikali makini kwa kufanya Vetting ya watendaji. Jukumu la Vetting ni jukumu la taasisi ya Data collection kuhusu watu wataofanya kazi zoooote katika serikali. Hata wafagizi lazima wawe vetted kwa sababu unaweza kusababisha shida kubwa sana katika serikali kutokana na kuweka criminal kwenye nafasi ya mfagizi kwenye ofisi ya serikali. Accurate Data Collection for Decision Making ni kazi ya Intelligence. Hapa Tanzania watu wa aina hiyo hatuna kwa sasa, and that should explain why very stupid decisions are made on occassions hapa nchini.

Hawa watu wasiojulikana walifikaje hapo kumuua afisa wa Takukuru bila kujulikana? Wewe unaona kuna maji taka katika hii hoja hapo? na unapata sababu kushangaa "sijui kama unafahamu majukumu ya usalama wa taifa? Si lazima kuchangia kila thread mkuu. Kama kitu hukielewi soma tu uelimishwe na wengine katika michango yao.
 
Kauwawa na mfanyakazi mwenzake! Jina kapuni kwa sababu za kiu-salama!
 
The bullet never lie. Ukiwekewa target upige mti unakosa ila akiwekwa mtu it goes directly to the skull. Case kama hii US itachunguzwa na dept zaidi ya 5 afu ndo utatueleza how bad luck is bad luck.
 
Usalama wa CCM mke wa CH....JA ndio mwajiri siku hizi ni laki tano au saba vile anayefuatilia biashara hii ya yule mama atukumbushe .cku hizi utendaji sio ishu ila unapesa............niambie watoto wangapi wa makabwela baada ya nyerere kufa wamepata chance huko zaidi ya walewale na failure yao ya 4m 4,
 
Kwamba sasa afisa wa TAKUKURU Bhoke Ryoba ameuawa na "watu wasiojulikana" mbele ya kadamnasi ya watu inaendeleza kile ambacho wengine tumekisema kwa miaka sita sasa - kuna tatizo la msingi la muundo na utendaji katika Usalama wa Taifa.

Ninakumbushia tu.

Imran alipouawa tatizo lilikuwa la nani?
 
Kwamba sasa afisa wa TAKUKURU Bhoke Ryoba ameuawa na "watu wasiojulikana" mbele ya kadamnasi ya watu inaendeleza kile ambacho wengine tumekisema kwa miaka sita sasa - kuna tatizo la msingi la muundo na utendaji katika Usalama wa Taifa.

Ninakumbushia tu.

Wako bize na kuhakikisha Dr Slaa haingii ikulu!

Hayo mengine ya maana baadae....liwalo na liwe!
 
Kwamba sasa afisa wa TAKUKURU Bhoke Ryoba ameuawa na "watu wasiojulikana" mbele ya kadamnasi ya watu inaendeleza kile ambacho wengine tumekisema kwa miaka sita sasa - kuna tatizo la msingi la muundo na utendaji katika Usalama wa Taifa.

Ninakumbushia tu.
mkuu ni kama una mzio na usalama wa taifa! sidhani kama usalama wa taifa watakuwa behind kila raia kumlinda asidhuriwe. kwa hili la TAKUKURU umechemka kidogo. ila kuna ishu nyeti kama DOWANS au meremeta au kagoda hapo usalama wa taifa lazima waguswe maana hizo ni ishu kubwa na nyeti kuwahusu hao. siwatetei usalama but sometimes let us be logical when analyzing things!
:cheer2:
 
Kweli chuki mbaya.Hawa watu wa takukuru wameuana wenyewe kwa wenyewe kwenye pombe zao sasa mlitaka usalama wa taifa ukataze watu kunywa pombe.Mfumo kristo unawapunguzia watu uwezo wa kufikiri.Magufuli kaenda kwa Laila kenya kelele.Sasa mbowe kaenda kimyaaa.
 
Back
Top Bottom