TANZIA: Afisa wa TAKUKURU auawa

TANZIA: Afisa wa TAKUKURU auawa

Inasikitisha sana.
Ila naomba niulize kuna mtu anajua majukumu ya hawa USALAMA WA TAIFA kimuundo serikali ?
USALAMA WA TAIFA is a very broad concept.I think some people are preoccupied with "usalama wa watawala." kama mikataba feki, bidhaa feki, ufisadi, mauaji, elimu duni n.k vinazidi kuzidi lakini watawala wako safi sasa usalama ni wa taifa au ....
 
Takukuru nyie ni watoto tu hata mjipendekeze vp hamuwezi pewa jukumu la usala wa taifa, hamliwezi. Bhoke ndo nani so far!?

kama kitu hukifahamu kiache...maafisa wote wa takukuru hupata mafunzo ya kijeshi na yale ya usalama wa taifa.
 
Hizi kazi nyingine nazo utata mtupu kwenye Tanzania ya leo hii
 
Nisiwe mshabiki ila kichwaa cha habari na maudhui havina mahusiano ya moja kwa moja, narudia tena mahusiano ya moja kwa moja.

Watu wamechangia saana huu uzi kwa sababu ya utendaji mbovu wa TISS kitu ambacho kingeweza kuanzishiwa uzi wake tofauti.

Ukifuatilia vyanzo vingi vya habari, kuna tofauti nnazoziona zinazingira tukio la haya mauaji,

Kwanza
Kuna utata wa muda wa tukio kutokea, wengine wanasema saa tisa usiku wengine wanasema kati ya saa :30 hadi saa2

Pili
Habari ya mara ya kwanza ilikua inasema walikua kwenye tafrija ya kuwaaga wenzao waiohamishwa vituo vya kazi, wengine wanasema kuuaga mwaka 2012, wengine wanasema haikua tafrija ya kikazi. Na walitumia gari binafsi ambalo namba zake za usajili hazijapatikana.

Kwa nini pawe na mknganyiko huu, na kwa kumbukumbu ya watu wengi matukio ya aina hii yamekua yakiishia kimyakimya.
Nadhani hapo ndio watu wanapoleta suala la ueledi na utendaji kazi wa TISS.
 
Watakuwa walidhulumiana deal hao! Kwa hiyo jamaa kalipiza kisasi.

Bahati mbaya gani hiyo jamani? Yaani ukoki silaha yako, ubonyeze kipigio ndo risasi itoke bado tunakubali kuwa ilikuwa bahati mbaya? Hapana uchunguzi wa kina unahitajika hapo.

Wangekuwa Policcm ningefungua kizibo cha champaigne sasa hivi!!

R.I.P Bhoke Ryoba
 
OFISA TAKUKURU AUA MWENZAKE KWA RISASI

OFISA wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) Makao Makuu Dar es Salaam, Musa John (34), amemuua mfanyakazi mwenzake kwa bunduki wakiwa ufukweni eneo la Kigamboni, Dar es Salaam.

John anadaiwa kumuua mfanyakazi mwenzake, Bhoke Rioba saa tisa usiku wa kuamkia jana katika ufukwe wa Kigamboni katika eneo la Southern Sun wilayani Temeke wakiwa katika sherehe ya kuaga wenzao waliopata uhamisho kwenda mikoani. Wote ni maofisa uchunguzi.

Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa John alimfyatulia risasi ya kichwa Bhoke
ambaye alifia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokimbizwa kwa matibabu.
Kwa sasa kwa mujibu wa taarifa hiyo, John anashikiliwa na Polisi Chang'ombe baada ya kufanya mauaji hayo na mwili wa Bhoke umehifadhiwa Muhimbili.

Akisimulia kisa cha mauaji hayo, mtoa habari wetu alidai kuwa wafanyakazi hao wakiwa katika ufukwe huo usiku saa tisa; baadhi wamelala na wengine wamekaa katika kusherehekea, walivamiwa na vibaka. Mtoa taarifa huyo alidai baada ya kuvamiwa na vibaka, John alitoa bastola yake kwa nia ya kupiga juu ili kuwatawanya vibaka hao ambao haikufafanuliwa walikuwa wangapi, lakini kwa bahati mbaya Bhoke aliyekuwa amelala, aliamka ghafla na risasi ikampata kichwani.

Ofisa Habari wa Takukuru, Doreen Kapwani alithibitisha kutokea kwa kifo hicho cha Bhoke jana kwa kupigwa risasi na John na kueleza kwamba ilikuwa kati ya saa 1:00 na saa 2:00 usiku, tofauti na taarifa za awali kwamba ilikuwa si saa tisa.
"Ni kweli imetokea jana (juzi) usiku kati ya saa moja na saa mbili huko beach (ufukweni) Kigamboni na wote wawili (Bhoke na Musa) ni watumishi wa Takukuru, Makao Makuu, Dar es Salaam," alisema Kapwani.

Huku akigoma kueleza kwa undani kuhusu tukio hilo kwa madai kuwa Polisi inafanya uchunguzi, Kapwani alisema utaratibu wa mazishi ya Bhoke unafanywa na familia yake inayoishi Kigamboni.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo akizungumzia tukio hilo alisema, "Taarifa ya tukio hilo tunayo na mtuhumiwa wa mauaji alijisalimisha mwenyewe Polisi na bado tunamshikilia kwa uchunguzi."

Kwa mujibu wa Kiondo, mauaji hayo yalitokea kati ya saa moja na saa mbili usiku ufukwe wa Kigamboni ambako mtuhumiwa na marehemu walishiriki na wenzao kwenye masuala ya kijamii.
"Walikuwa kwenye kufurahi kijamii, si shughuli ya kiofisi, walikwenda kwa gari ndogo binafsi ambayo bado namba za usajili hatujazipata, katika kufurahi huko ndipo John alipiga risasi na kumpata Bhoke katika jicho la kushoto," alisema.

Kamanda Kiondo alisema Bhoke alipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili usiku huo kwa matibabu, lakini baadaye alifariki akiwa hospitalini hapo na mwili umehifadhiwa hapo.
Kiondo alisema Polisi inachunguza sababu za John kupiga risasi kutokana na tukio hilo kutawaliwa na utata. Takukuru na Polisi wamekanusha kuhusu kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi baina ya wahusika hao wawili.
 
Hatukatai. Ila kwa bahati mbaya ya aina yako ina maana marehemu angekuwa amelala sakafuni au sijui amechuchumaa!
Au 'mwana bahati mbaya' alikuwa anacheza mduara sasa baadala ya kuweka kidole juu akaweka machine ya kutoa vitu vyenye ncha kali juu!
 
Hivi ukiwa katika sherehe wanaruhusiwa kubebea silaha!!!? walikuwa kazini au katika starehe? Sheria za silaha nchi hii tafadhali tusije tukafikia Marekani!
 
Hili imebekia kuwa taasisi ya kupeleka umbea chama Tawala na kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu. Yeyote atakayeenda kinyume na kujifanya kufata maadili ya kikazi katika UWT basi huyo lazima ashughulikiwe.

Hahahhah! Hii nimeikubali mkuu.Usalama wa Taifa kazi yake kupambana na Upinzani tu. Yani siku hizi raia wanaona ni taasisi fulani ya kupuuza! Hawaichukulii seriouz kama miaka ya nyuma.
 
R.I.P afisa. Poleni familia ya afisa, na wafiwa wote. Lakini silaha, bahati mbaya, how? Haiingii kichwani, nasubiri wanaojua hizo silaha waje waeleze zinavyolipuka bahati mbaya
 
Ni kweli itakuwa ni bahati mbaya tuu!, hata Kombe alipouliwa uliwa, si ni ilikuwa ni bahati mbaya tuu!, hata juzi polisi walipomuua Mwangosi, maelezo yameandikishwa, bomu la machozi lilifyatuka kwa bahati mbaya tuu!.

Ni bahati mbaya jamani!.

NB. Hata Takukuru wafiche vipi, ukweli utajulikana tuu!, shooting ifanyike saa 2:00 usiku Southern Beach watu wasijue?!, ati walikuwa wamelala na kuvamiwa na vibaka, katika kupiga risaji juu ikampata jichoni?!. Mind well marehemu ni mwanamke na muuaji ni mwanaume na sio wapenzi!. There are more questions than answers!.

RIP Bhoke Ryoba!.

Pasco.
 
Hakuna bahati mbaya kwenye matumizi ya silaha za moto,nasisitiza HAKUNA BAHATI MBAYA!huyo mtu achukuliwe hatua za kisheria,wafiwa poleni sana
 
USALAMA WA TAIFA is a very broad concept.I think some people are preoccupied with "usalama wa watawala." kama mikataba feki, bidhaa feki, ufisadi, mauaji, elimu duni n.k vinazidi kuzidi lakini watawala wako safi sasa usalama ni wa taifa au ....

Hapo sawa ,ni dhahiri kuwa watu wengi wana assume hawa TISS hawana majukumu yao yaliyoainishwa . Laiti watu wangejua tusingewalaumu . Mtu unapokuwa na uelewa kuhusu CIA ,KGB ,FBI Ukataka kulazimisha kufikiri hawa usalama wa taifa bongo wanamajukumu kama hayo,huko ni kupotoka .

Hawa jamaa ukielezwa wanachofanya utastaajabu ,ndio maana wanaonekana na kubandikwa jina USALAMA WA VIONGOZI hata kama Jamii haiwataki wa maovu yao .
 
Hapo sawa ,ni dhahiri kuwa watu wengi wana assume hawa TISS hawana majukumu yao yaliyoainishwa . Laiti watu wangejua tusingewalaumu . Mtu unapokuwa na uelewa kuhusu CIA ,KGB ,FBI Ukataka kulazimisha kufikiri hawa usalama wa taifa bongo wanamajukumu kama hayo,huko ni kupotoka .

Hawa jamaa ukielezwa wanachofanya utastaajabu ,ndio maana wanaonekana na kubandikwa jina USALAMA WA VIONGOZI hata kama Jamii haiwataki wa maovu yao .
Asante mkuu. Ni kweli maana kila wanapoenda wakubwa wao hutangulia kwanza, tena kwa maposho manene. kwenye misafara na mikusanyiiko ya wakubwa huko kuna ufanisi wa hali ya juu. huku kwingine wakiwa hivo usalama oh! utafana hata wagonjwa hawatalishwa dawa feki, barabara hazitapewa watu feki, elimu hatakuwa feki n.k. n.k.
 
Back
Top Bottom