Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 19,093
- 9,261
HABARI KWA KINA kutoka kwenye magazeti ya:
Mtanzania
Tukio hilo lilitokea wakati wafanyakazi hao pamoja na wenzao, walipokuwa katika sherehe za kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2013.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo, alisema mauaji hayo yalitokea juzi saa 1.30 usiku, katika ufukwe wa Hoteli ya Sourthen Beach iliyopo Kigamboni, Temeke Dar es Salaam.
"Watumishi hao walikodi gari ndogo na kwenda kwenye ufukwe huo, kwa ajili ya kupata vinywaji na chakula. Wakati walipokuwa wakifurahia, ghafla inasemekana John alichukua bastola kisha akampiga Bhoke kwa risasi iliyompata jichoni. Tukio hilo lilisababisha Bhoke atokwe damu nyingi na wenzake walipoona hivyo, wakaanza kutimua mbio huku na kule. Baadaye walimchukua majeruhi na kumkimbiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, akiwa katika hali mbaya na alifariki dunia usiku wa kumkia jana, wakati akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo. Kutokana na tukio hilo, mtuhumiwa John alijisalimisha mwenyewe katika Kituo cha Polisi Chang'ombe Temeke, ambako bado anashikiliwa huku uchunguzi zaidi wa tukio hilo ukiendelea. Mwili wa marehemu umehifadhiwa hapo hapo Muhimbili. Bado tunaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hili, ili tuweze kujiridhisha na mazingira halisi ya tukio zima kwani wakati linatokea, hapakuwa na ugomvi wowote. Kwa hiyo, tukio linahitaji uchunguzi wa kina tujue namna bastola hiyo ilivyotumika kumpiga marehemu na sherehe hizo zilikuwa zinahusu nini kwani waliohusika ni baadhi tu ya watumishi waTAKUKURU," alisema Kamanda Kiondo.
My TAKE:
Ya kuambiwa changanya na za kwako,
hawa kwanini wakimbie?
alitaka kua na wengine au?