Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mtumishi mwenzake kwa bahati mbaya walipokuwa katika sherehe za kumuaga mwenzao katika hotel ya South Beach iliyopo Kigamboni jijini hapa Dar es salaam. Risasi hiyo ilimpata mhanga huyo katika kichwa na kumuua hapohapo.
Innalillah wayna ilahy rajiun
Innalillah wayna ilahy rajiun
Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Bhoke Ryoba, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na ofisa mwenzake wakati wakisherekea ufukweni mwa Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Afisa Uhusiano wa Takukuru, Ryoba alifariki dunia juzi baada ya kupigwa risasi.
"Tumekuwa tukipokea simu nyingi kutoka kwa watu wakihitaji kufahamu ukweli wa tukio la kupigwa risasi kwa mtumishi Bhoke Ryoba, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, anapenda kutoa ufafanuzi kuhusu tukio hili kwamba ni kweli alifariki dunia Jumamosi (juzi) usiku baada ya kupigwa risasi," ilieleza kwa kifupi taarifa hiyo