Maneno ya Mwanakijiji ni haya hapa chini:Mi sikuona maji taka hapa.
"Kwamba sasa afisa wa TAKUKURU Bhoke Ryoba ameuawa na "watu wasiojulikana" mbele ya kadamnasi ya watu inaendeleza kile ambacho wengine tumekisema kwa miaka sita sasa - kuna tatizo la msingi la muundo na utendaji katika Usalama wa Taifa. Ninakumbushia tu."
Sasa tafakari maneno yaliyo katika Blu na ujiulize ni mara ngapi matukio makubwa yamefanywa hapa Tanzania na yakawa yamefanywa na "watu wasiojulikana." Kesi inayoongelewa inahusu tukio kubwa ambalo limefanywa na watendaji katika Serikali, kuleta maana kuwa kuna criminals wapo ndani ya Serikali ya nchi yetu.
Criminals huwa hawaruhusiwi kufanya kazi katika serikali, na zuwio hili hufanywa na serikali makini kwa kufanya Vetting ya watendaji. Jukumu la Vetting ni jukumu la taasisi ya Data collection kuhusu watu wataofanya kazi zoooote katika serikali. Hata wafagizi lazima wawe vetted kwa sababu unaweza kusababisha shida kubwa sana katika serikali kutokana na kuweka criminal kwenye nafasi ya mfagizi kwenye ofisi ya serikali. Accurate Data Collection for Decision Making ni kazi ya Intelligence. Hapa Tanzania watu wa aina hiyo hatuna kwa sasa, and that should explain why very stupid decisions are made on occassions hapa nchini.
Hawa watu wasiojulikana walifikaje hapo kumuua afisa wa Takukuru bila kujulikana? Wewe unaona kuna maji taka katika hii hoja hapo? na unapata sababu kushangaa "sijui kama unafahamu majukumu ya usalama wa taifa? Si lazima kuchangia kila thread mkuu. Kama kitu hukielewi soma tu uelimishwe na wengine katika michango yao.