Tanzania's Foreign Policy

Katibu Tarafa

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2007
Messages
980
Points
1,225

Katibu Tarafa

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2007
980 1,225
kulikoni,
serikali yetu imejaa mazumbukuku,badala ya kuutangaza utali kwa kutumia njia mwafaka sasa wao ndio wanegeuka watali.ile wizara ya mambo ya nje wakati mweshimiwa anaiongoza aliwarudisha mabalozi wangapi nyumbani kwa kushindwa kuleta watalii.muungwana na wapagazi wake hawana jipya.
 

Mkandara

Verified Member
Joined
Mar 3, 2006
Messages
15,472
Points
1,250

Mkandara

Verified Member
Joined Mar 3, 2006
15,472 1,250
Kulikoni,
1.
1. Kunapokuwa na habari mbaya katika image ya nchi ni jukumu la ubalozi, wizara ya mambo ya nje na hata idara nyingine mbali mbali kujaribu kubadili hilo, njia zipo nyingi na kazi kubwa ya ubalozi ni ku-redress the negative image. Hivi ndio vipimo vinavyotumika kuangalia effectiveness ya balozi husika, in fact who knows kwa kuweka ukweli bayana unaweza vutia watalii na wawekezaji....precisely Membe's point!!
Nitazidi kusisitiza kuwa zinapotoka habari za image mbaya ni muhimu kutazama image zenyewe... na sio kujitetea wakati ukweli umebakia pale pale. Mwanamke malaya mwenye HIV kuficha maradhi yake kwa kutumia mdomo ama vyeti feki ni ujinga mkubwa sana. By the way hao wazungu wanajua kabisa hali ya TZ ndio maana wanazo balozi zao ndani nchini.

2.
2. Ziara za muungwana ni ku-capitalise jitihada za balozi, hivi jamani mnadhani Mheshimiwa Rais ataibuka tu aende ziarani, it all begins with proper co-ordination ya ubalozi, idara za itifaki, ikulu na respective departments on the host governments, akiondoka rais wanaofuatia ndio wanacapitalize on the promises, pledges nk....Wawekezaji wakisikia from the horses mouth na ubalozi ukiwa effective kufuatilia ndio matunda yanaokana... UbAlozi mzuri ndio utafuatilia vizuri...Precisely Membe's point ''Tutawapima kwa kuleta wawekezaji''
Tatizo letu sio hizo ziara isipokuwa ni ziara ambazo zinatangaza Umalaya wetu kwa malengo ya kuuza mwili. Mwanamke mzuri mwenye sifa zote hawezi kumtafuta mume kwa njia hiyo... Yes nitakubaliana na wewe tu ikiwa sisi sote tunazungumzia Umalaya.

3. '' Tengeza nyumba wapangaji watakuja tu'' sounds nice Mkandara lakini I am afraid though it is a true statement but incomplete, wakati mwingine you need wapangaji ili uweze kujikwamua upate fedha ndio ukarabati, they need to go hand in hand... Tuna uwezekano wa kupata mafuta as dalili zipo, uwezo wa ku-explore hatuna hivi tusiombe misaada nje kuwaalika wawekezaji kwa vile bara bara ni mbovu? Tuna gesi nyingi sana, utaalam wa kui-convert into usable energy hatuna hivi tusitangaze tender ya kampuni za kigeni kuja kuredress this kwa vile kuna matatizo ya umeme?! Waziri akisema mabalozi watapimwa kwa kuvutia wawekezaji kuna kosa gani? Kukarabati nyumba YES mkandara lakini wapangaji tunawahitaji as well...
Kulikoni, Maelezo yako ni mazuri sana kwa Malaya anayeanza kumwambia mteja wake matatizo yaliyomfikia hadi kufikiia maamuzi yake ya kuwa Malaya. Do you think hao wazungu mnao wafuata wanajali?..Unafikiria mzungu haelewi kuwa uzuri ulionao ni faki unatumia mapoda na kuvaa paruka (wig) ili ufafanane nao...Mteja wa malaya siku zote anachotazama yeye ni kukidhi nyege zake, He care less matatizo yako na urembo wa make up zako, hayo mapoda.
Tatizo lako unalitazama swala hili kama Malaya wakati mimi nalitazama swala hili kama uwezo wa mwanamke kuweza kujitegemea na kupata mume kwa sababu ya mapenzi. Hito theory yako ya kusema kuna wakati unahitaji mpangaji kabla hujajenga ni theory inayotumiwa na Malaya. wala huwezi kusema kwamba wanaume hakuna ama hakuna hakika ya kuolewa ukiwa na elimu na kujitunza vizuri. haya ni mawazo ya mwanamke aliyekwisha kata tamaa kabisa.
Pamoja na kuwepo na nafasi ndogo ya ushiriki wa mwanamke, mwanamke anakiwa zaidi kuwa na elimu, Kuutunza mwili wake hasa unapojaliwa mwili kama mama yetu Tanzania. Kuuanika mwili wa mama yetu tanzania ktk magazeti ya Uchi sio sifa hata kidogo.

Kifupi ndugu yangu jaribu kuzungumza lugha moja. Kila hoja yako inalenga sana utetezi wa maisha ya mwanamke Malaya. Ili Malaya aweze kufanikiwa ni vitu gani muhimu anatakiwa kuvifanya!

Akina mama mtanisamehe kwa kutumia lugha hii lakini nakuombeni mtazme zaidi sifa niliyoipa nchi yetu Tanzania kama Mama yetu sote.
 

mTz

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2006
Messages
283
Points
0

mTz

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2006
283 0
Mkandara,

I like your metaphoric language, it says all, blank truth, its time we/they get back to senses and put things in order. Lets stop denial of facts, the direction in which our leaders are taking the country is not going to lead us into sustainable development, its only a handful of cronies who are going to enjoy!
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
8,854
Points
1,250

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
8,854 1,250
Mkandara
Nimekusikia mkuu maneno mazito ujumbe sahihi JK asitufanye isis wajinga na wapambe wake . Wote hawana lolote wanalilia ukuu tu . Acheni wizi wa mali zetu tumikieni Watanzania.
 

Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2006
Messages
1,220
Points
1,250

Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2006
1,220 1,250
Wanabodi,
Mimi hapa mtu wa kale na elimu yangu ni ya madrasa lakini nitasema yanayonisumbua.
Hakuna cha digrii ya MA wala Phd ikiwa digrii hiyo hifanyii kazi kulingana na mazingira yako. Hizo digrii zenu za International relations mnazo zipatia nje zinatazama mazingira ya uhusiano wa Uingereza ama Marekani nje na sio kutoka nje kuingia nchi hizo. Hizi ni Academic na lazima kuzifanyia majaribio ndani mwako ambayo unayatazama kwa mtazamo wa kutoka Tanzania kwenda nje ili ziweze kufanya kazi vizuri na sio kutazama nje ili uibadilishe Tanzania kukidhi nchi hizo.

Nitakwambieni kitu kimoja walichokifanya nchi kama China, Maleysia, India na hata Ireland kwa kipindi kifupi sana. Hawa jamaa zetu wametazama nchi zao mapungufu yake ya ndani wakayafanyia kazi kuyaweza katika mazingira bora. Mazingira ambayo ni pamoja na kuelemisha wananchi wake ktk sekta ambazo wameziwekea mikakati ya muda mfupi na mrefu, badala ya wao kutumia muda mrefu kunadi nchi zao.
Hujasikia hata siku moja viongozi wa nchi hizi wakikimbia huku na kule kutafuta soko kwa sababu walikuwa wakifagia kumbi zao kuondoa taka kwanza kwa zaidi ya miaka kumi na ushee. Na hadi kesho huwezi kuona viongozi wao wakijipendekeza ktk nchi za Magharibi isipokuwa hushusha nyanga zao mezani na kusema:- This is what my county can offer! Wakiweka imani kwamba kizuri siku zote hujiuza na kibaya hujitemmbeza!...
Ukiwa na elimu na uwezo wa kufanya kazi siku zote CV (resume) yako itasema, kinachofuata ni interview na pengine kuiapata kazi sio kuzunguka na resume mkononi kila bar kuongea na wajomba wakutafutie ajira. Something is wrong!
Tunachofanya Tanzania ni biashara ya Umalaya kusimama pale Joly na kuhamia viwanja vya Maggot, Skyway, Kwa macheni na Kinondoni Block... kwa hiyo hata kama una digrii gani ukiwa malaya wewe malaya tuu!...na hiyo digrii ittakusaidia zaidi ktk kutafuta soko la Umalaya, sana sana advantage yako kubwa itakuwa lugha. usichokifahamu ni kwamba huyo mzungu mtalii anachotaka sii lugha yako ila mwili wako ambao hauna tofauti na mwanamke mwingine yeyote isipokuwa wewe ni kati ya wanawake rahisi kupatikana.

Viongozi wetu na hasa JK pleeease tengeneza kwanza nyumba yako ili upate wapangaji, watakuja tu kama walivyoweza kufanya wenzetu. Nitanukuu msemo mmoja wa rais wa maleysia akiwaambia raia wake kuwa

"Huu ni wakati mgumu sana kwenu kwa haya nitakayo waeleza!..Kuna wengi hamtaweza kunielewa lakini nakuombeni uvumilivu wenu na kesho mtakuja kunikumbuka.
Leo ni siku ambayo Maleysia imefikia Uamuzi wa kutupa magongo na wananchi kujaribu kutembea bila magongo. Malesia sio taifa lemavu lenye kilema cha uchumi ila tulipata ajari mbaya ya kiuchumi tukavunjika miguu yetu.
Kwa muda mrefu sana tumeyatumia magongo hayo, na sasa hivi ni wakati wa kujaribu kutembea wenyewe bila msaada wa magongo!..
Ukizoea kutembea kwa magongo ni rahisi kujenga imani kwamba hujapona vizuri na hautaweza kuelewa kama kweli umepona ikiwa hutajaribu kutembea bila magongo!.."

Maneno hayo ni mazuri sana na amsho kubwa kwa mataifa kama yetu kutoendelea kutegemea IMF na misaada ya nchi za magharibi ambayo ndiyo kiini cha safari zote hizi. Kuendeleza imani hizi za kuwa taifa tegemezi hata siku moja hatuwezi kwenda kokote.
Sijui kama mnalifahamu hili kuwa nafasi ya Afrika leo hii katika soko la dunia imeshuka hadi asilimia 2 kutoka aslimia 8 ambayo ilikuwa imesimama miaka ya bara hiri kupata Uhuru. sasa hii habari ya Utandawazi inatupa picha gani ikiwa nafasi yetu imepungua zaidi ktk soko hilo kuliko zamani?...

Ina maana moja tu! - Hatuwezi kushindana! na utaweza vipi kushindana ikiwa wewe mwenyewe umesha kubali huwezi kuzalisha kisha unamwita mgeni ambaye anachukua mali yako na kuiweka ktk soko la dunia kwa jina lake!..

Kisha tazameni ni vitu gani nchi kama marekani inaagiza kutoka tanzania kiasi kwamba wanadai leo kuwepo na mahusiano mazuri ya kibiashara kati yetu na wao!...Nini hasa watu hawa wananunua kutoka kwetu? Utaona ni sahani, vinyago, mbachao, mananazi, fulana za t-shrit na sijui maua, hali vitu vyote vikubwa ambavyo vinaweza kujenga uchumi wetu wanavitaka wao kuvikamata kwa kutumia majina yao.
Leo mnakimbilia Ulaya kuitangaza TZ ili ipate kukamatwa zaidi ktk vitu ambavyo vinapatikana tanzania. Why hao wawekeshaji wasije jenga viwanda vya uzalishaji wa vitu ambavyo sisi hatuna i.e magari? Electonic parts na hata mazao yetu kuwa ktk finished product ndani ya nchi?
Mkandara!
Hawa watu wanaelewa kwamba huko kuomba kwao si suluhisho la matatizo ya mtanzani bali ni suluhisho la matatizo yao Binafsi, kwani misaada mingi na mikopo mingi inawanufaisha wao zaidi kama viongozi wetu na si watanzania wote, ndiyo maana wanaweka pamba masikioni.Huoni Njaa wanavyoivalia kibwebwe hata muekezaji fake anapokewa na utitiri wa viongozi na anapewa tiketi ya kuingia ikulu kuonana na Mtu anayeitwa nasi Rais!
 

Mkandara

Verified Member
Joined
Mar 3, 2006
Messages
15,472
Points
1,250

Mkandara

Verified Member
Joined Mar 3, 2006
15,472 1,250
KNKU,
Nakuelewa sana mkuu na naielewa vizuri kazi ya PIMP!, tupo mjini.... hao mapimp kibao wamejaa.
Hata siku moja Pimp hawezi kuelewa tunachozungumza ikiwa mwanamke mwenyewe anazidi kupendeza na viatu vya mchuchumio (Twin tower). Maendeleo ya mdanganyika yanapimwa kwa uwezo wa huyu mama yetu Tanzania kuwa na ma Gucci, Range rover na Pamba za Bugatchi,Varsace,Armani hali makazi yale Kinondoni makaburini, watoto wananunuliwa nepi za mitambara ya kaki!.. chakula mzungu (Ugali wa sembe) wakitoezea na vyama vingi (maharage). Watoto wakipiga kelele tunaambia bila huo Umalaya mtaweza kula hata hayo maharage?...
Kulikoni, Tanzania ina option nyingi, Umalaya sii last option kabisa wala hatujafikia nafasi ya kukata tamaa. JK yuko desperate kama alivyokuwa Mkapa na matokeo yake ndio wanazidi kututokomeza ktk Umalaya bila kujua kuwa Umalaya una muda wake. Ukisha zeeka tu hakuna bwana atakaye kupenda na wala hizo make up hazitaongopa tena!
Hata siku moja, thamani ya nchi haitazamwi kwa wingi wa Range na hayo magorofa ama mzungu gani mwenye fedha kalala na mama yetu Bongo.
 
B

Brutus

Guest
B

Brutus

Guest
Bw. Kulikoni!
ECONOMIC DIPLOMACY haiwezi kufanikiwa bila kutumbulia macho COMPETITIVE INTELLIGENCE!
I think you know better than that.. na Hon. Membe kama Intelligence officer na mwanadiplomasia anaweza kufanya zaidi ya hapo!
Sorry to say this, lakini alichoongea ni ' Cheap-talk' for an Intelligence officer and a long time diplomat!

haya mambo ya Mr. President na timu yake yana-sound kama mbwembwe za Chiluba na Zambia!
Mr. Kulikoni... hivi hawa jamaa zako unaowatetea huwa wanafuatilia na kujifunza kutokana na yanayoendelea kwa jirani zetu??

Mzee mkandara anaongea lugha rahisi sana... UMALAYA!
Hiki sio kitu kizuri kabisa!
Tanzania inajiuza ikiwa na too much make-ups... jamaa wanatimiza nyege zao wanatimua.. mwisho wa siku "Tanzania" anarudi kwenye kibanda chake na bafu la passport-size!
Ikulu na wizara ya mambo ya Nje inabidi ifanye reforms ya utendaji wake ili hizi habari za Economic Diplomacy ziweze kufanya kazi vizuri!
Uswahili-swahili umezidi!
 

Game Theory

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2006
Messages
8,570
Points
0

Game Theory

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2006
8,570 0
Kulikoni
usione kimya

bado niko archives nakusanya data na sources...so far niko pazuri lakini niliona bora nichukue na kule John Hopkins ambako natumai by next week nitakuwa na kitu kamili


vile vile kuna data nazikusanya 1977-1990

sasa kama unavyojua sipendi kufanya mambo ya character assassinations au witch hunts lakini the bottom line i expected alot toka kwa Membe na still sijakata tamaa..ila naona matamshi yake yalinifanye nione kama kuna strategy za kumharibia au he is the fall guy. na kilichonitisha ni yeye kujoin katika bandwagoning ya ALTIMUTUMS kam PM na sidhani kuwa kama its the best approach hata katika kutoa directives.

but time will tell

in the mean time nipe muda bado nakusanya mambo
 

mikuki

Senior Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
101
Points
0

mikuki

Senior Member
Joined Mar 10, 2007
101 0
Naomba nitoe mchango wangu kidogo hapa. Mimi nadhani Tanzania tatizo letu kubwa ni kwamba tunayajua matatizo yetu lakini hatujajua njia sahihi za kuyakabili au hatujui matatizo yetu ni yapi na ndo maana we have failed to do right things!!. Huwezi kuja US au Europe kutafuta investors au watalii wakati wakija Tanzania hata maji ya kunywa siyo salama na kwanza hayapatikani! Basic social infrastructure zimetushinda. Dar Es Salaam yetu bado kipindupindu ni threat KM mbili toka ikulu kwa JK.

Wengi mko huku ughaibuni: Hivi mkiangalia maisha ya huku yalivyo, unategemea kweli mtu akawekeze au akatalii sehemu kama Dar au Tanzania? Sio kwamba hatuna cha kuonyesha la hasha! mazingira ni mabovu. Hata watalii wanasave sana kusudi waweze kusafiri. Kwa nini asiende mfano Belize au Eastern Asia anakojua atatumia pesa yake vizuri na atafurahia? Hata usafi unatushinda? Shame on us! Afrika umaskini wetu uko rooted kwenye fikra na kupanga. Viongozi wetu ndo wanatusaliti.

JK na mabalozi wetu waache longo longo wakae wafanye kazi..hizi porojo hazitufikishi popote! Anakuja UK au US na delegation ya watu hamsini...hivi hawajifunzi hata kitu kimoja? au wanakuja kufanya shopping tuu? Angalia jiji la Dar mpaka leo mitaa yote ni michafu, sewarage system ni mbovu ya mwaka sitini kabla ya uhuru! hakuna reliable public or private transport, Dala dala mpaka ugombanie..huyo mtalii unataka atembee kwa mguu? hakuna reliable public law enforcement organs, polisi ni public enemy, very corrupt... fukwe za bahari ni chafu wameamua kuweka uzio. Imagine! Hawa hawa akina meya ndo wanashinda huku ulaya kwa "ziara za kujifunza".

Harafu tunataka tulete watalii? mnacheza! Mimi I love my country, lakini huwezi kuniambia kwamba Tanzania we are doing much to attract serious investors! because we are not serious! Wengi tukipewa nafasi..(wengi tunapokea madaraka tukiwa na interests ya kubadili system..sadly, system inatubadilisha!!)we think of our stomach, family, tukizidi hapo ni ukoo na kabila kwa mbaaaaaaaali sana!! Thats all!.

Mpaka tuwe serious, tugundue hao Asian tigers tunaowaongelea kila siku..walifanikiwa kwa vitendo na sacrifices na si porojo! As long as we continue on this paths, lets be assured of being perpertual embarrasment to the international community while condemning our people on permanent deprivation of their dignity! Mi nafikiri Bush akipokea maraisi wa Afrika White Hose..anajua kabisa niko na mijambazi hapa!! Maana ni mijitu isiyofikiria watu wao at all!!

Hivyo basi tuache ndoto za alinacha (jamaa anasema investors wajenge hata production plants kama magari)! Fanya takwimu, ni watanzania wangapi tunanunua magari mapya? mazingira ya kuwekeza hayaruhusu! Investment climate TZ bado!! we need to ADRESS THE BASICS KWANZA!! TZ tuna hotuba nyingi sana, ila utekelezaji ndo sifuri. Hawa mabalozi walioko njee what they care ni $$..Tutengeneze mazingira..investors watakuja tuu. They need resources and we HAVE THEM!

Mpaka tujue kuprioritize maslahi ya wengi badala ya parochial self serving interests za wachache ndo tutasonga mbele.
 

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
8,636
Points
2,000

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
8,636 2,000
Maneno yamesemwa na Mikuki, Brutus, Mkandara n.k kuwa Tanzania tubadilishe tabia ya kubembeleza watalii na wawekezaji; badala yake tujenge mazingira ya kuwafanya watamani kuja kwetu. Uchafu, miundombinu mibovu na umaskini wa raia wetu ni vitu ambavyo vinawatisha watalii. Kwa mfano kama mtoto wa rais au waziri wetu anakwenda Ujerumani kutibiwa mafua je, je mtalii akiumwa na nge au nyoka pale kwetu atatibiwa wapi? Hii ina maana kuwa tunatakiwa kuwa hospitali za kuaminika ili pia kuwavuta kwetu hasa ukizingatia kuwa mazingira yetu yana magonjwa mengi. Kuwa na umma wa maskini huwa kunajenga uhalifu ambao pia unachangia kwa kiasi kikuu kuwafanya watalii wasije. Mwaka 1991 nilikutana na jamaa mmoja Australia aliyekua na hamu sana ya kupanda mlima Kilimnajaro; hivyo alikuwa anaplani kwenda Kenya ili apate nafasi ya kuupanda. Nikamwambia kuwa mlima ule uko Tanzania na hivyo akiingia Kenya bado atatakiwa apitie uhamiaji kabla hajaingia Tanzania kuupanda mlima ule. Nikamshauri aje Dar es Salaama moja kwa moja, jambo ambalo alilifanya. Kitu cha aibu kilichotokea ni kwamba wakati anachukua basi la kutoka Dar kwenda Arusha, makonda wakamgonga sana nauli kuliko hata ile ya ndege. Jamaa alikasirika sana alipogundua nauli halisi kutoka Dar hadi Arusha baada ya kumwuliza jirani yake ndani ya basi. Nilichukulia tabia hii kama ya kimaskini.
 

Tabasamu

Senior Member
Joined
Nov 27, 2006
Messages
136
Points
0

Tabasamu

Senior Member
Joined Nov 27, 2006
136 0
Tatizo letu bongo hatuna viongozi, tulionao ni watawala. Maneno ya Mkandara ndio yanayotakiwa kuwa yanatoka kwa viongozi na hayo ya KUlikoni ndio yatoke kwa waongozwa. Lakini hapa tunaona the opposite is true. Hivi nchi itafika wapi wakati kila wakiambiwa vitu vya maana wanakuja na utetezi wa ovyo ovyo?
 

Kulikoni

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2006
Messages
203
Points
195

Kulikoni

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2006
203 195
nakuamini DR WHO sio hawa wengine wanakurupuka na kuandika, fanya research kijana na uje hapa tuonyeshane hoja.


Maliza masomo tunahitaji critical minds kama wewe pale makao makuu Foreign na pia vituoni, kazi nzuri na i wish you good research...

wengine igeni mfano, arguments zenu hazina kichwa wala miguu labda MIKUKI na BRUTUS ambao nitawajibu eventually...

Mkandara unaboa majibu yangu nitakutumia kwenye PM manake umekosa nidhamu kabisa nchi yako unalinganisha na Kahaba? ama kweli wazaliwa kisutu mpo wengi....
 

Interested Observer

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2006
Messages
1,583
Points
2,000

Interested Observer

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2006
1,583 2,000
Kulikoni wewe kama sijakosea upo Canada, katika past introduction yako uliongelea kuwa unafanya research. Wewe unaweza kuwa na upeo mkubwa na global trends, kuhusu investors sentiments, immigration and natural human movements.
Mikuki na Mkandara wameongelea in details priorities ambazo viongozi wetu inabidi wawe wanazo. Vitu vingine vinakuja naturally; vijana wa Kimarekani na Ulaya, wakitaka mapumziko kutalii wanachagua Thailand, Hong Kong, China, Morocco, je kwa nini? Wewe kwa jibu la haraka unaweza kusema ni kwa sababu ya ubaguzi. Please rejea tena maneno ya Mikuki na Mkandara, then make a constructive contribution tuache mambo ya zidumu fikra za mwenyekiti!
 

Dr.Khamis

Member
Joined
Mar 5, 2007
Messages
44
Points
0

Dr.Khamis

Member
Joined Mar 5, 2007
44 0
Majadiliano yenu ni mazuri sana kama “viongozi” wetu watasoma na kufuatilia. Hivi leo tumesoma kwenye magazeti kwamba PM ametaka Dar isafishwe na kaipa manispaa ya Dar changamoto na “Ultimatum”. Lakini tena PM anaendelea katika barua yake na kutaka kuwe na “Tram System” hapo Dar.
1. Kweli matatizo yetu ni mengi na tunayafahamu wazi wazi. Lakini jinsi ya kuyatatua ndio kazi. Tuna tapatapa, mara hivi na mara vile.
2. Kama hiyo “Tram System” anayosema PM. Kwanza lazima tujenge reli katika jiji la Dar na vitongoji vyake. Na hiyo “tram” itatumia nini kama sio umeme?
3. Umeme wenyewe ndio huo wa matata.
4. Sehemu nyingine za jiji itabidi hiyo “tram” ipite chini ya ardhi. Je tumefanya utafiti wa kutosha.
5. Reli zetu za zamani zinatushinda na hivi sasa twazikodisha kwa kampuni kutoka India.
6. Maji ni kitu muhimu kwa binadamu yoyote. Sasa ni kitu gani ambacho kinatushinda kwani ujuzi wa kutafuta maji tunao toka zamani. Idara ya Maji ni ya kwanza nchini kupata wataalamu wa kitanzania ambao wamefundishwa kutoka nchi mbali mbali ulimwenguni.
7. Tunapeleka vijana wetu kusomea udaktari nchi kadhaa ulimwenguni. Lakini sasa hivi utaona tunapeleka wagonjwa India, UK, na Afrika kusini kutibiwa.Mtalii akiumwa na nyoka tutamrudisha kwao akatibiwe?

Basic social infrastructures ndizo ambazo viongozi wetu wanatakiwa kuzitilia nguvu.

8. Hiyo “Sewage System” kwa kweli ni jambo la kustaajbisha.Watanzania walitolewa katika idara ya maji kwenda Holland kusomea jinsi ya kusafirisha maji machafu. Kukaundwa shirika la maji machafu! Lakini kipindupindu hakiondoki jijini.
9. Hapa serikali inaweza kutoa kazi kwa vijana wengi sana ambao sasa hivi wanazururua mitaani na kuwa majambazi. Ujenzi wa miraro mipya katika jiji zima na vitongoji vyake ni “project” ya muhimu sana.

Mara nyingi nasema matatizo twayafahamu lakini hatuna ile “priority” list. Ni lazima tuyatatuwe matatizo yetu “systematically”.
 

Sam

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2006
Messages
416
Points
0

Sam

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2006
416 0
nakuamini DR WHO sio hawa wengine wanakurupuka na kuandika, fanya research kijana na uje hapa tuonyeshane hoja.


Maliza masomo tunahitaji critical minds kama wewe pale makao makuu Foreign na pia vituoni, kazi nzuri na i wish you good research...

wengine igeni mfano, arguments zenu hazina kichwa wala miguu labda MIKUKI na BRUTUS ambao nitawajibu eventually...

Mkandara unaboa majibu yangu nitakutumia kwenye PM manake umekosa nidhamu kabisa nchi yako unalinganisha na Kahaba? ama kweli wazaliwa kisutu mpo wengi....


sam nimeedit maneno yako yamekuwa makali mno na ningependa kukuarifu kuwa ulivuka mpaka

humu hatutukanani ile tunakwenda na hoja

KAMA unalazaidi unaweza kuni contact through PM
DR WHO
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
8,854
Points
1,250

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
8,854 1,250
IO Kulikoni yuko London ni shushu Ubalozini wacha kupoteza muda wako . Last week nikiwa London I met him ila hawezi kuona ndani nma ushushu wake .
 

Mwawado

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2006
Messages
998
Points
195

Mwawado

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2006
998 195
Jamani Taratibu tusitupiane Matusi,Kwa mwendo huu hatutofika na tunapoteza Muelekeo!.Tafadhalini sana Waungwana tusitiane vidole vya macho!.Ikiwa hukubaliani na Hoja za mwenzio,bishana nae kistaarabu lakini sio matusi.
 

Nzokanhyilu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2007
Messages
1,087
Points
0

Nzokanhyilu

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2007
1,087 0
Mkandara, unapointi nzuri.
Kila siku nakaa naangalia Tourism marketing strategy, hata sielewi. Anyways, kuna tangazo la benki ya HSBC naliona kila siku atleast mara 5 hivi katika TV hapa UK. Tangazo hili linahusu Savings katika benki hii, na linaonyesha global outreach ya benki hii. Tangazo linapoanza tu, unaona mlima Kilimanjaro, but straight away inatajwa Kenya. I bet you this image is seen by millions in the UK, if not world wide. Whether Kenyans paid for that (which I doubt), but it shows, there is a strong belief worldwide in regards to Kilimanjaro being in Kenya. Everytime I see that image, najisikia siko sawa kama mtanzania.
Anyways, katika mambo yote kuhusu uwekezaji. Kinachoniuma sana ni kilimo, na kabla sijarudi kwenye Kilimo, ngoja niongelee resources zingine. Unajua, haya Oil/Gas/Coal, ni utajiri utakaoisha. And chances are, utajiri huo utaisha kabla hata hatujafaidika kimaana. Haya mambo (technology yake) najua, kwasababu nimesomea. I am pretty sure, viongozi katika energy sekta hapo Tanzania watakua wanajua (na kama hawajui, nitakuwa dissapointed sana, as its an open secret) kwamba USA (and most probably UK and other developed countries), wana tumia mafuta sana, pia wanastorage facilities kubwa ambapo wana store mafuta for the longer term. Na sehemu ambazo wamemaliza resources zao (au ni bei sana kuchimba), wameacha makusudi, na wanachimba mafuta nchi zingine. To these guys, kuanzisha vita na instability, ni cheaper, just to get to the oil in the longer run. Marekani kuongeza vituo vya majeshi afrika (who knows, even Tanzania from the sounds of it) ni longterm strategy yao. Its cheaper to buy Oil, then eventually you are going to buy from them (perhaps another technology of Energy source). Wanacontrol nuclear energy (wakati tayari technology wanayo), eventually you will buy from them. Wanapiga makelele kuhusu going 'green', wakati wenyewe walishapita. Which means, kwa vyovyote vile, hayo makaa yaliyo Tanzania, for the technology to develop it, you will need Western investment, at their conditions (and yes, there is Green technology for coal, unlike somewhere I read on Mjengwa's blog, which makes me question how many journalists know what they are talking about. No disrespect, just a little research is usefull).
Sasa Mkandara anapoongelea umalaya (though I wouldnt use that word, ingawa linapendezesha), ni kama vitu vya kununua technology. Jamaa wanakuja na technology zao, watafanya watakacho, wakiondoka wewe huna kitu. Ni kitu hicho hicho kinachotokea nchi za uarabuni. Pamoja na utajiri wote huo, hawasomeshi watu wao wabuni technologia. Machinery kubwa zote, wanakuja nazo wazungu. Middle East may look rich, lakini, longterm, watakua na matatizo sana.
Tanzania is filthy rich, even though wazungus say we are one of the poorest countries in the world.

Ok, kabla sijapotea mwelekeo, ngoja nirudi kwenye kilimo. Unajua, mtu ukiwa na ardhi/land, basi wewe sio masikini. Now, imagine, Tanzania isiwe na utajiri wa madini. Tutafanya nini na ardhi? Au tunaifanyia nini ardhi?
Hii topic interesting, na mimi nimeona jinsi Mh. JK anavyozunguka na entourage kutafuta wawekezaji. In theory, good idea. Mkandara unaposema watengeneze environment nyumbani. You are right on. We on the same wavelength. These guys are interested in getting investors for Kilimo among many other things.
First of all (if I look at the UK), the food products market, is controlled by Indians. The success of your product from your kilimo (in a developing country), can be looked at from a direction of how well you are selling your products in the supermarkets here in the UK. And I mean big supermarkets like Sainsbury, Tesco, Asda. Not corner shops selling unga wa Bhakressa (and I am not disrepecting at all). Sasa, I dont know how many of you are aware that, food products from Tanzania are diverted to India. They are then processed and repackaged as Indian products, then they are exported to the UK. And a quick estimate, say a kilo of cashew nuts is maybe a few pence (when bought in TZ), if that kilo is processed and sold at Tesco/Sainsbury, it will sell at anything between £10 to £20. Now this is a rough estimate. Sasa you ask yourself, if something aint wrong in Tanzania (and needs to be corrected), how do you expect an Investor to come to Tanzania, when it is convenient to buy from India. And probably, that Tanzania - India -UK route is held by some maffia. How do you break that? Isnt the problem in Tanzania?

On the same note, Tanzania's budget was less that 2% (correct if am wrong) for 2006/07 on agriculture. Agriculture is supposed to contribute 50% of the GDP. Are you telling, if I was an investor, how will I look at you if you read these figures to me?

So I think, cleaning needs to start home before asking for investors to come home. One of our major assets is land and water in abundance. And find ways, come with policies, to stop the post processing of Tanzania products in India. Only Tanzania can stop it. Kweli, kama mimi ni mhuni na napenda malaya, sitamwambia jinsi gani aache umalaya. Lakini mimi sitaki kuwa malaya, nina nia na uwezo wa kujiengua, kwanini nikuombe mhuni uniengue?? Aisee Mkandara (am scaring myself, am starting to copy your filthy language hahaaaaa)!!
 

Forum statistics

Threads 1,382,151
Members 526,283
Posts 33,820,807
Top