Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
- Thread starter
- #61
Nimeshapata muda na wiki hii nitajibu hoja zote zilizotolewa kwa mpangilio
Kikwete: Wekeni ukurasa wa Watanzania
wa nje katika tovuti.
Rais Jakaya Kikwete ameishauri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kufungua ukurasa katika tovuti yake kwa ajili ya vyama vya Watanzania wanaoishi�katika nchi mbalimbali.
Alisema hatua hiyo itatoa fursa kwa watanzania hao kuwasiliana kwa urahisi na wizara hiyo na wadau wengine pale wanapohitaji taarifa fulani au msaada kutoka serikalini.
``Hivi katika tovuti yenu mnao ukurasa ambao unaonyesha anuani za vyama vya Watanzania waoishi nje ya nchi, kama hakuna basi wekeni ukurasa huo, hii itakuwa njia nzuri kwao kuwasiliana nanyi lakini pia na wao kuwasiliana na wadau wengine ili pale wanapopata fursa za uwekezaji na biashara,`` alisema.
Alitoa ushauri huo mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa akisalimiana na Watanzania wanaoishi na kufanya shughuli mbalimbali nchini Ghana.
Rais Kikwete alikuwa akihudhuria mkutano wa tisa wa kawaida wa Wakuu wa Nchi na serikali wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika.
Alijibu hoja mbalimbali kutoka kwa Watanzania hao ikiwamo ile ya uraia wa nchi mbili, mchakato wa uanzishwaji wa Shirikisho la Afrika Mashariki na msimamo wa Tanzania kuhusu mjadala wa kuanzishwa kwa serikali ya Afrika.
Rais alisema, suala la uraia wa nchi mbili linafanyiwa kazi na Tume ya Kurekebisha Sheria na baada ya kutoa mapendekezo yake, suala hilo litafikishwa kwa wananchi ili walijadili.
Kuhusu mchakato wa Shirikisho la Afrika Mashariki, Rais alisema yeye kama Rais asingeweza kutoa maoni yake kwa sasa mpaka hapo wananchi watakapokamilisha kutoka maoni yao.
Alishauri masuala yanayotaka mjadala na mawazo ya wananchi si katika uanzishwaji wa shirikisho peke yake, bali hata katika mambo mengine kama vile soko la pamoja, ushuru wa forodha wa pamoja masuala aliyosema yanatakiwa kujadiliwa sambamba na uanzishwaji wa shirikisho la kisiasa.
Akijibu swali kuhusu maoni ya Tanzania juu ya kuanzishwa kwa serikali ya Afrika, Rais alisema kwamba wazo la kuanzishwa kwa serikali moja, si geni kwani liliasisiwa na Rais wa kwanza wa Ghana, Nkwame Nkrumah.
Alisema kuhusu hilo wapo wenye maoni tofauti juu ya kuanzishwa kwake, wapo wale wanaodhani suala hili lisiamuliwe kwa haraka na badala yake liende hatua kwa hatua.
``Lakini wapo pia wale ambao wanadhani kwamba huu ni wakati muafaka wa kuwa na serikali moja, lakini mtazamo wa viongozi kutoka nchi za SADC na EAC na wengine wengi ni kwamba twende hatua kwa hatua tukianzia na jumuia ya uchumi kwanza,`` akafafanua Rais. Akizungumzia kuhusu vita dhidi ya rushwa, Rais Kikwete alisema kwamba vita hivyo bado vinaendelea ingawa ni kazi nzito kwa kuwa kitendo chenyewe hufanyika kwa siri.
Kuhusu uwezeshwaji wa wananchi, Rais alisema serikali inaendelea na juhudi zake na kwamba anafurahi kwamba baadhi ya benki kama vile CRDB na NMB zimeanza kuutambua ukweli kwamba wajasiriamali wadogo wanakopesheka na wanarejesha mikopo yao.
Katika mazungumzo yao Watanzania hao, walimweleza Rais kwamba kuna fursa za biashara nchini Ghana, hasa katika mazao ya chakula, lakini walikuwa hawajui wawasiliane na nani ili kuwashawishi wafanyabiashara Watanzania kupeleka bidhaa hasa vyakula nchini humo. Nchi ya Ghana ambayo ni maarufu sana katika uzalishaji wa dhahabu na kokoa, asilimia kubwa ya vyakula vinavyoliwa nchi humo, vinaagizwa kutoka nchi jirani na kuuzwa kwa bei kubwa.
``Mheshimiwa Rais huwezi kuamini, unga wa ugali hapa tunanunua kwenye maduka makubwa (supermakert) na kwa bei ghali sana, tunadhani Watanzania wenzetu wanaweza kufanya biashara kubwa sana ya kuleta unga na vyakula vingine lakini hatujui tutawasilina nao vipi,`` alisema Bw. Sanyaj Rughani,Mtanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa Standard Chartered nchini Ghana.
Na siyo hilo tuuu,In short sijui hao ambao wanamkono katika kuformulate foreign policy yetu huwa wanafikiri nini. Hakuna updates zozote kuhusu ubalozi mpya Brazil, hatujui wanajeshi wetu kule Lebanon wanaendeleaje,na hata issue za Great Lakes region nazo hatujui serikali yetu inasema nini
In short serikali hii iko out of touch na kila Mtanzania aliyewapatia mandate ya kuongoza