Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Pamoja na juhudi zetu kubwa za kuking'oa CCM, ukweli ni kuwa vyama vya Upinzani havijajiandaa vizuri kuliongoza Taifa letu.
Hili linatokana na ukweli kuwa havina watu wa kutosha ambao wanaweza kuwa Wabunge na kuendelea kwa migongano na kukosekana kwa watu wenye nguvu za kukubalika na jamii na hasa majimboni kuwa Wabunge.
Ni bahati mbaya sana Mzee Victor Kimesera mgombea uchaguzi wa CHADEMA Kiteto, yupo hoi bin taabani Dar kwa ajili ya matibabu. Wengi tumekimbilia "sumu" wengine watasema lwao. Lakini ukweli ni kuwa kama Mtoa uhai angemtwaa Malaika wake, je CHADEMA wangemsimamisha nani? Do opposition have a back up plan?
Kama sikosei, Mzee Kimesera anaweza kuwa na umri kati ya miaka 65-72. Hivyo basi CHADEMA wamekimbilia kumpa tunu hiii mtu mzee. Uzee si hoja au dhambi, bali jee hapakuwa na mtu mwingine yeyote ila Kimesera? Kumbukumbu zangu ni kuwa yeye Kimesera aligombea Kiteto 1995, hivyo miaka 12 baadaye, anaendelea kuwa mgombea pekee mwenye utashi na kukubalika kwa wananchi wa Kiteto?
Leo hii miye nimeshupalia Kikwete avunje Bunge na baraza la Mawaziri. Akifanya hivyo na kuitisha uchaguzi mkuu baada ya miezi 6 au hata mwaka mmoja, je Upinzani una watu wa kutosha wenye uwezo na ushawishi kukubalika katika majimbo? au ni kusubiri mabaki kutoka CCM?
Nilipoleta ile mada ya Chadema must Reform na Focus 2010, niligusia vitu kama hivi, je kina Mnyika, Kitila na Zitto, mko tayari kuchukua nchi nzima?
Zaidi la hofu ambalo ndili linalofikia kusababisha wananchi waendelee kuchagua CCM (Zimwi likujualo) ni ukweli kwamba hata kama Upinzani ukishika hatamu, je unauwezo kuongoza nchi? wanawatendaji wa kutosha wanao waamini kufanya kazi na kutekeleza mikakati na sera za vyama hivi vikichukua madaraka?
Si nia yangu kuviogofya au kuvunja nguvu za upinzani, ila ni ukweli usiopinguika na hali halisi! Upinzani upo tayari kimaneno, lakini kiutendaji sidhani hata kama wana uwezo japo 40%. Upinzani umejaa misuguano na kikubwa ambacho wanafahamika sana sasa hivi ni kuhusu vita vya ufisadi vya Slaa na Zitto.
Swali ni hili, ikiwa CCM kesho watajirudi na kujisafisha kuhusiana na Richmond, BOT, ATCL, RADA na IPLT, je upinzani utakuwa na hoja gani kujiuza? watakimbilia Katiba? au ndio kula ruzuku ambazo no kodi zetu?
Napenda kutoa hoja!
1. Ni kitu gani kinafanya upinzani leo hii 17 years baada ya Multi-party bado kuzidi kuwa dhaifu Tanzania?
2. May be mda wa kukaa Bungeni uwe na ukomo kama ilivyo kwa Raisi?
Yaani Maximum mtu kuwa mbunge iwe vipindi vitatu vya miaka 5 yaani 15 years- ili pia kutoa nafasi kwa wengine!
Mugo"The Great";135184 said:Swali ni hili, ikiwa CCM kesho watajirudi na kujisafisha kuhusiana na Richmond, BOT, ATCL, RADA na IPLT, je upinzani utakuwa na hoja gani kujiuza? watakimbilia Katiba? au ndio kula ruzuku ambazo no kodi zetu?
CCM kujisafisha na kashfa hizi maana yake ni kufagia safu nzima ya uongozi. Kuanzia Muungwana mwenyewe, EL na wengineo. EL, Kara na wengineo hawatakubali wafe peke yao itabidi wamtumbukize na bosi wao. Hivyo itakuwa mwisho wa CCM. Kuhusu kama upinzani una watu wa kutosha, jibu ni kuwa watu wapo wa kutosha. Nani alimfahamu Zitto kama anaweza kuwa mwiba kwa mafisadi bungeni? Napenda umma wa Watanzania wajue kuwa tuna vijana wengi wanao-graduate Vyuo mbalimbali nchini na diaspora na wana-uwezo wa kuiongoza nchi ila wanakuwa frustrated na watawala ambao huhakikisha kuwa kama wanaingia kwenye siasa basi maisha yao yanaandamwa. Ukitaka kujua kuwa CCM inaelea hewani, ni wakati wagombea binafsi watakaporuhusiwa kikatiba.
kishoka ur too general,yaani issue moja kama hii ndio basi upinzani wote ushaona hawako tayari,hiyo ni juu yako na haki yako kusema chochote ingawaje ni tafauti sana na unayoandika kila siku, ila sisi tupo na tutaendelea kussuport wapinzani na hata hayo mafanikio madogo madogo amabayo yamekufanya uwe na issue ya kuandika humu kwangu mimi hiyo tosha na hatua moja mbele...bila hao ambao hawako tayari usingejua BOT,Richmond,Buzwagi etc na mafisadi wangeendelea bila kujulikana,anyway safari hii ni ya wachache wenye moyo.
kishoka ur too general,yaani issue moja kama hii ndio basi upinzani wote ushaona hawako tayari,hiyo ni juu yako na haki yako kusema chochote ingawaje ni tafauti sana na unayoandika kila siku, ila sisi tupo na tutaendelea kussuport wapinzani na hata hayo mafanikio madogo madogo amabayo yamekufanya uwe na issue ya kuandika humu kwangu mimi hiyo tosha na hatua moja mbele...bila hao ambao hawako tayari usingejua BOT,Richmond,Buzwagi etc na mafisadi wangeendelea bila kujulikana,anyway safari hii ni ya wachache wenye moyo.
Koba,
I have to face reality. Yes I have been fighting for good governance even pushing opposition to stand tall so that good governance and fairness will rule and lead Tanzanians. the fact remains the opposition is weak.
Let me throw you a challenge. Create a Tanzanian government using anyone in opposition. This includes President, Vice, President of Zanzibar, Prime Minister, Cabinet, speaker, RC, DC!
Kilichotokea Kiteto hata kama tutadai faulo za CCM ni dhahiri kuwa bado Upinzani haujaweza kujiuza kikamilifu kwa Taifa la Tanzania.
Mwalimu Kitila atakuja na kudai tuwape nafasi, Mnyika atasema tembeleeni tovuti, lakini juhudi za wao kujijenga (opposition) zinaelekea ni kwenye kutoa uozo na nyakati za uchaguzi. je ni lini watajiuza kukiwa na heri?
Tangu sakata la Lowassa kuaonguka, yaelekea kana kwamba upinzani umetimiliza kazi. Matamko waliyoyatoa kutaka mapendekezo ya Mwakyembe yafanyiwe kazi yanaonekana ni mepesi na si tya nguvu mpaka Serikali iamke.
Je n lini Upinzani utaanza kujijenga na kujiuza kwa Watanzania kwa umakini?
je ni lipi lililo tokea Kiteto ambacho kilisababisha Upinzani kushindwa kama tukiondoa fujo na faulo za CCM?
Sasa hapa Mnyika alikuja hapa akawasihi wenye interest na upinzani wawasiliane nae- sasa hata JF hakuna aliyemjibu!
We stay 'there' na kusema 'wale dhaifu'- sasa kama sii mimi na wewe ni nani ataimarisha upinzani?
Watz tunapenda chakula kilichoiva tu- yaani tupakue na kula!
Ila kulaumu- ni wa kwanza!
It couldn't put it better. Kwa maneno mengine unachosema ni kwamba watanzania wengi tunapenda kuwa sehemu ya mafanikio lakini sio sehemu ya mapambano!