Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,525
- 1,523
Pamoja na juhudi zetu kubwa za kuking'oa CCM, ukweli ni kuwa vyama vya Upinzani havijajiandaa vizuri kuliongoza Taifa letu.
Hili linatokana na ukweli kuwa havina watu wa kutosha ambao wanaweza kuwa Wabunge na kuendelea kwa migongano na kukosekana kwa watu wenye nguvu za kukubalika na jamii na hasa majimboni kuwa Wabunge.
Ni bahati mbaya sana Mzee Victor Kimesera mgombea uchaguzi wa CHADEMA Kiteto, yupo hoi bin taabani Dar kwa ajili ya matibabu. Wengi tumekimbilia "sumu" wengine watasema lwao. Lakini ukweli ni kuwa kama Mtoa uhai angemtwaa Malaika wake, je CHADEMA wangemsimamisha nani? Do opposition have a back up plan?
Kama sikosei, Mzee Kimesera anaweza kuwa na umri kati ya miaka 65-72. Hivyo basi CHADEMA wamekimbilia kumpa tunu hiii mtu mzee. Uzee si hoja au dhambi, bali jee hapakuwa na mtu mwingine yeyote ila Kimesera? Kumbukumbu zangu ni kuwa yeye Kimesera aligombea Kiteto 1995, hivyo miaka 12 baadaye, anaendelea kuwa mgombea pekee mwenye utashi na kukubalika kwa wananchi wa Kiteto?
Leo hii miye nimeshupalia Kikwete avunje Bunge na baraza la Mawaziri. Akifanya hivyo na kuitisha uchaguzi mkuu baada ya miezi 6 au hata mwaka mmoja, je Upinzani una watu wa kutosha wenye uwezo na ushawishi kukubalika katika majimbo? au ni kusubiri mabaki kutoka CCM?
Nilipoleta ile mada ya Chadema must Reform na Focus 2010, niligusia vitu kama hivi, je kina Mnyika, Kitila na Zitto, mko tayari kuchukua nchi nzima?
Zaidi la hofu ambalo ndili linalofikia kusababisha wananchi waendelee kuchagua CCM (Zimwi likujualo) ni ukweli kwamba hata kama Upinzani ukishika hatamu, je unauwezo kuongoza nchi? wanawatendaji wa kutosha wanao waamini kufanya kazi na kutekeleza mikakati na sera za vyama hivi vikichukua madaraka?
Si nia yangu kuviogofya au kuvunja nguvu za upinzani, ila ni ukweli usiopinguika na hali halisi! Upinzani upo tayari kimaneno, lakini kiutendaji sidhani hata kama wana uwezo japo 40%. Upinzani umejaa misuguano na kikubwa ambacho wanafahamika sana sasa hivi ni kuhusu vita vya ufisadi vya Slaa na Zitto.
Swali ni hili, ikiwa CCM kesho watajirudi na kujisafisha kuhusiana na Richmond, BOT, ATCL, RADA na IPLT, je upinzani utakuwa na hoja gani kujiuza? watakimbilia Katiba? au ndio kula ruzuku ambazo no kodi zetu?
Napenda kutoa hoja!