Tanzania yasema haina mpango kupokea chanjo za Covid19

Tanzania yasema haina mpango kupokea chanjo za Covid19

Kwa hiyo ACT wameudanganya umma kwa habari ya Makamu wa kwanza wa Rais, au Zanzibar siyo sehemu ya Tanzania na hivyo taarifa zao hatuzitumii?
 
Hivi mfano Maalim Seif akiamua yeye binafsi achajwe maana ametuambia anaumwa Corona watamzuia kweli? Swala la afya ya mtu binafsi ni personal huwezi kunipangia kwa kuwa tuu unataka political mileage.
 
Pls waziri wangu wa Afya kama hatuna covid 19 why umeweka sheria ya msafiri anayetoka hapa nchini kwenda nje ya nchi kulipa 100usd ili kupata covid certificate kama upo negative?au ndio mwendekezo wa sisi manyumbu?test ya nini wakati nchi haina covid?
 
Waziri wa afya Dr Gwajima amesema serikali haina mpango wa kupokea chanjo ya Corona kwa sababu nchi iko salama na haina maambukizi ya Covid 19...
Naona huyu mama kachanganyikiwa.

Eti nchi haina maambukizi....aiseee....Maalim anaumwa nini kwa mfano.

Huyo mtu aliewashauri watumie staili hii anawadhalilisha sana.

Haya hizo dawa za lishe zimewasaidia kwenye kitu gani.

Alafu na jumapili alienda kusali na akasimama mbele ya kanisa kusalimia......ila Mungu yupo.
 
Semeni tu mzigo unakuja kwa ajili yenu Masenior, sisi akina ngumbalu tujiongeze tu
 
Wao walishakunywa dawa ya madagascar kwa hiyo wametuacha tuangamie
 
... au Zanzibar siyo sehemu ya Tanzania na hivyo taarifa zao hatuzitumii?
Kama kweli waziri kasema nchi hii haina covid19, atakuwa anapingana na mkuu wa nchi aliyedai kuna watu walikwenda ughaibuni na wametuletea corona hivyo katushauri tuchukue tahadhari stahiki.
 
Kuna Uzi nimetoa mawazo yangu kuhusu COVID 19 nimeandamwa sana na wajuaji, nimesikia maelezo ya Dr. Gwajima, nimeshangaa sana akishauri tutumie dawa za asili, kweli?
katika karne hii Waziri na msomi wa level yake anashauri tukamuone Dr. Mwaka.

Busara kubwa sana inahitajka katika hili, Mungu atusaidie.
 
Siyo kwamba hawatumii wao washajiandaa kutumia hizo chanjo na washaanza kuwaandaa wananchi wao
View attachment 1691795
Hizo ni placebo tu hamna chanjo hapo, chanjo yenyewe ndio inaletwa huku Afrika kufanyiwa majaribio, itakayofaa ndio watawapelekea watu wao katika kila wanachoita followup shots, ndio maana hata wakichomwa wanaambiwa waendelee kuvaa mask na kuchukua tahadhari
 
Siasa UCHWARA zimetamalaki hata kudharau Sayansi. Taifa linaloongozwa na
Waziri wa afya Dr Gwajima amesema serikali haina mpango wa kupokea chanjo ya Corona kwa sababu nchi iko salama na haina maambukizi ya Covid 19....
 
Kuna Uzi nimetoa mawazo yangu kuhusu COVID 19 nimeandamwa sana na wajuaji, nimesikia maelezo ya Dr. Gwajima, nimeshangaa sana akishauri tutumie dawa za asili, kweli?...
Wasukuma na mambo yao ya kienyeji awamu hii.
 
Back
Top Bottom