Tanzania yasema haina mpango kupokea chanjo za Covid19

Tanzania yasema haina mpango kupokea chanjo za Covid19

Kwa mtizamo na mawazo yangu ,kweli ni vizuri kujilizisha kabla hatuanza kuzitumia,kwani UK chanjo yao baada ya kuitumia ndipo kikaibuka kirusi cha aina nyingine cha Corona ambacho kina nguvu kuliko cha kwanza.

Kama ingekuwa vizuri,tungepata sample ya chanjo zote za Corona ambazo zimegunduliwa kuanzia ya UK,US,Russia,China,Iran na Israel tuzipime tujilizishe na tujue ipi ni nzuri na ipi ni bora kuliko hivi tunavyo lazimishwa na WHO ambao nao sizani kama Wamezipima kujilizisha.

Chanjo sasa hivi naona zinaendeshwa kibiashara kila mtu anadai chanzo yake ni bora,huku tokea chanjo zinguduliwe na kuanza kutumika ndipo virusi vipya vimeanza mara kuna cha south,cha UK na Brazil.Yaani kwa kivupi vurugu zimekuwa nyingi sana upande wa hizi chanjo,mpaka najiuliza hivi WHO hawana maabara zao ,wazipime chanjo zote baadae basi watuambie zipi ni nzuri na zipi hazifai.

Wamewaachia makampuni haya ya madawa hawa hawajali afya za watu wanacho angalia ni faida na ndio maana wanapeleka vitu haraka ili waliteke soko,hawajali afya za watu wanafanya trial and errors mpaka kwenye afya za watu,sometimes hizi chanjo ni full kubet.
 
Chanjo itafanya nchi nyingine zisiwe na corona, na kama Tanzania tutakuwa nayo, TUTATENGWA. Na utalii itakuwa byebye
 
Kwa hali ya sasa serikali haina haja ya kukimbizana kuchukua chanjo ambayo bado iko kwenye majaribio..unakuwa unacheza kamari kwenye afya za watu.
 
Kwa mtizamo na mawazo yangu ,kweli ni vizuri kujilizisha kabla hatuanza kuzitumia,kwani UK chanjo yao baada ya kuitumia ndipo kikaibuka kirusi cha aina nyingine cha Corona ambacho kina nguvu kuliko cha kwanza...
Una mawazo mazuri sana.
 
Sisi WaAfrika ndio wanataka kutufanyia testing ndio maana wanaforce hizo chanjo
Siyo kwamba hawatumii wao washajiandaa kutumia hizo chanjo na washaanza kuwaandaa wananchi wao
 
View attachment 1691739
Ukiona mtu anaamini hadithi za kitaahira kama hizi unasikitka sana, cha ajabu unakuta ana familia wanamtegemea kwa ushauri. Ndio maana hii nchi ujinga hautaisha.
 
kwa nia njema kabisa ni hadi tujiridhishe na si vinginevyo,” amesema Dk Gwajima.


Ili kujiridhisha ni hatua zipi zinazochukuliwa?? Isitoshe hizo hatua zinaweza kuchukua muda gani??

Hayo ni maswali muhimu sana huyo Waziri anatakiwa atujibu Watz kwani maisha yetu yanapotea kila uchao. Akumbuke kwamba Waziri wa afya ni sawa na waziri wa uhai.
 
A
Acha ujinga kwa ARV ndio nini bhana wewe kama una ngoma jibebe, ila chanjo hatuitaki
Hata ARV hatuzitaki, ni virusi hivyo hivyo tumeshaambiwa ni futa likifukizishwa linayeyuka. Hizo hela za misaada ya kununua ARV zitumike kupunguza deni la taifa
 
Hata ARV hatuzitaki, ni virusi hivyo hivyo tumeshaambiwa ni futa likifukizishwa linayeyuka. Hizo hela za misaada ya kununua ARV zitumike kupunguza deni la taifa
kwani wewe unachotaka ni nini, mbona unaweweseka sana una corona nini maana sio kwa kudai huko
 
Serikali kupitia Wizara ya afya imesema kuwa haina mpango wa kupokea chanjo ya Covid19 ambayo imekuwa ikiripotiwa kuwepo na kutumika katika mataifa mengine...
Mlipuko uko Tanzania au nchi jirani? Udaktari tupa kule, sasa ni uongo uliokomaa, yaani siasa!
 
Serikali kupitia Wizara ya afya imesema kuwa haina mpango wa kupokea chanjo ya Covid19 ambayo imekuwa ikiripotiwa kuwepo na kutumika katika mataifa mengine...
Suala la kutokuwa na mpango wa chanjo ya Covid-19 sio la kupenda kwa Tanzania, bali ni hali imelazimisha kwa kuwa serikali haina kabisa fedha za kununua chanjo. Kumbuka tukitaka kuleta chanjo lazima ije ya kutosha watanzania wote, karibu milioni 45. Hatuna fedha, period.

Sasa yanayobaki ni visingizio tu kwamba ooh chanzo wazungu wnataka kutumaliza, ooh Tanzania hatuna Covid.

Serikali inaona aibu na fedheha kuwatangazia wananchi kwamba hatuwezi kuagiza chanjo za Covid-19 kwa kuwa hatuna fedha. Jiulize, unafikriri serikali ikisema hatuna fedha za kununua chanjo, huku tumekuwa tunatamba tuna fedha za kujenga SGR, Stiegler Gorge, madaraja baharini, flyovers, wananchi watailewaje serikali?

Mbaya zaidi, fikiria serikali iseme haina fedha za kununulia chanjo wakati kuna miradi ya mabilioni kule Chato ambayo mingine haina hata umuhimu au uharaka.

Labda jambo serikali isiloelewa ni kwamba katika suala la chanjo kwa mataifa masikini, Umoja wa Mataifa una namna ya kuyasaidia. Lakini sasa hata kuko tulishawatibua kwa kukataa kushirikiana nao kuhusu data za Covid-19.

Ukweli ni kwamba serikali inakosea sana kuwaamulia Watanzania wasichanje. Aina ya matibabu huwa ni hiari ya anaetibiwa, ili mradi tu aina hiyo ya matibabu impepitishwa na vyombo vinavyokubalika kimataifa. Viongozi wa siasa hawana haki ya kuwaamulia Watanzania wachanjwe au wasichanjwe dhidi ya Covid-19. Huo ni ukiukwaji wa haki za wananchi.
 
kwani wewe unachotaka ni nini, mbona unaweweseka sana una corona nini maana sio kwa kudai huko
Mimi nasema hivi, tuachane na hizi dawa kutoka mataifa ya nje kwa hata magonjwa mengine, kwa sababu hao hao tusiowaamini na chanjo zao wanaweza kutuwekea vitu visivyo salama kwenye chanjo na dawa dhidi ya magonjwa mengine wanazotupa. Unafikiri tunavyogomea hizo chanjo kama wana nia ovu watuacha salama ?
 
Kwamba chanjo nyingine ni sawa ila si hii ya korona siyo? Hii Sirikali ina nini na korona? Huko kwa wazungu ndo imewafyeka zaidi wao ndo walipaswa waanze kuzikataa.
 
Waziri wa afya Dr Gwajima amesema serikali haina mpango wa kupokea chanjo ya Corona kwa sababu nchi iko salama na haina maambukizi ya Covid 19.

Dr Gwajima amewataka watanzania kutumia dawa lishe ambazo hata yeye na familia yake wanazitumia na zimewasaidia sana.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom