Tanzania yasema haina mpango kupokea chanjo za Covid19

Tanzania yasema haina mpango kupokea chanjo za Covid19

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Serikali kupitia Wizara ya afya imesema kuwa haina mpango wa kupokea chanjo ya Covid19 ambayo imekuwa ikiripotiwa kuwepo na kutumika katika mataifa mengine.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Februari Mosi, 2021 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima wakati akitoa tamko lake katika ofisi za wizara hiyo jijini Dodoma.

Dk Gwajima amesema dhumuni ya ufafanuzi huo ni juu ya maswali kadhaa ambayo amekuwa akiyapokea kutoka kwa wanahabari ambao wamekuwa wakimuuliza kuhusu kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.

“Kufuatia taarifa za uwepo wa mlipuko wa pili wa ugonjwa wa corona, Covid19 katika nchi jirani nimekuwa nikipokea maswali mengi kutoka kwa wanahabari.

“Wizara ya Afya haina mpango wa kupokea chanjo ya Covid19 inayoripotiwa kuwepo na kutumika katika mataifa mengine, ifahamike kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya inayo taratibu za kufuata pale inapotaka kupokea bidhaa yoyote ya afya baada ya Serikali kujiridhisha hivyo kwa nia njema kabisa ni hadi tujiridhishe na si vinginevyo,” amesema Dk Gwajima.

Chanzo: Mwananchi
 


1CE5786F-F2A6-4AD5-8767-1F5E2A4120A3.jpeg
 
Safi! Kabla wazungu hawajaivamia Afrika kwani si tulikuwa tunaishi?

Tangu wamekuja huku na magonjwa yamekuwa mengi.... Kwanini tusiamini wao ndio wanatutengenezea magonjwa kwa sababu wanazozijua wao?

Niko pamoja na serikali katika hili
 
Serikali kupitia Wizara ya afya imesema kuwa haina mpango wa kupokea chanjo ya Covid19 ambayo imekuwa ikiripotiwa kuwepo na kutumika katika mataifa mengine...
Heading is misleading. Inapotosha, wanataka kujiridhisha wataipokea baada kuonekana ufanisi wake. Itakusaidia na wewe, familia yako.
 
Wakatae na chanjo nyingine basi! Wasiishie kwenye hiyo chanjo ya Corona tu. Waende mbali zaidi! Ikibidi hata madawa yote yatengenezwe Nchini.
 
Wako mbioni wanajiridhisha au wameshajiridhisha kwamba haifai ?, Na kama wamefanya hivyo na sisi pia ni WHO, kwanini tusiwape hizo findings wenzetu wasiangamie ?, AU ndio genes za Uchawi, na Roho Mbaya ?
 
Kwani zile huwa ni bure si huwa tunanunua, walifanikiwa kusambaza magonjwa saivi ndio wanatuuzia hizo dawa. HIV walisambaza wenyewe miaka hiyoooo, na hayo magonjwa mengine
Wakatae na chanjo nyingine basi! Wasiishie kwenye hiyo chanjo ya Corona tu. Waende mbali zaidi! Ikibidi hata madawa yote yatengenezwe Nchini.
 
Wako mbioni wanajiridhisha au wameshajiridhisha kwamba haifai ?, Na kama wamefanya hivyo na sisi pia ni WHO, kwanini tusiwape hizo findings wenzetu wasiangamie ?, AU ndio genes za Uchawi, na Roho Mbaya ?
More data, testing, result, efficacy, effectiveness are needed.

Inavyofanya kazi kwa wenye magonjwa mengine, watoto (not tested yet).

Chanjo ngapi utapewa, zitakusaidia vipi kupunguza ugonjwa.v

Sipo kupinga chanjo yoyote.

Muhimu kujua details, everything.

Quote
 
Nashindwa kuielewa Tanzania yangu, sawa lakini

ngoja niendelee kujifukiza.
 
Back
Top Bottom