CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 4,984
- 4,083
Nchi ya Tanzania kuelekea 2025 Rais Samia Suluhu amedhibiti mfumuko wa bei|| US, UK, Uturuki, Ujerumani hali ni mbaya.
===Nchi tajiri kabisa dunia ya Marekani inayomiliki zaidi ya asilimia 20 ya Uchumi wote wa dunia hii nayo ni muhanga wa hili,
Marekani inashuhudia mfumuko mkubwa na mbaya zaidi wa bei kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo unaofikia asilimia 6.8,
Ahueni ni kwamba,Tanzania sisi tumesalia kwenye mfumuko wa bei uliyo kati ya asilimia 3 & 5.
Mfumuko huu wa bei wa nchi ya Marekani haujawahi kutokea kwa zaidi ya miaka 40 iliyopita,
Nchi ya Marekani kwa mara ya mwisho ilishuhudia mfumuko wa bei unaokaribiana na huu mwaka 1982,
Watanzania lazima mwelewe vizuri kadhia hii ya mfumuko wa bei Si kwa Tanzania na Marekani tu,UK, Uturuki, Ujerumani nako hali ni mbaya kuliko Tanzania,
Wakati watanzania wengi tunalalamika kwamba vitu vimepanda bei nchini hali ni tofauti sana kwa majirani zetu na duniani kote,
Watanzania lazima mwelewe,Kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa Covid -19 bei ya bidhaa na huduma karibu dunia nzima iko juu sana,
Ushauri wa bure kwa Watanzania wenzangu tufanye bidii kuelewa yanayoendelea huko duniani sio kulalamika na kuilalamika serikali yenu pekee ,
Kwa mujibu wa World Population Review Tanzania ilikuwa na Inflation ya asilimia 3.4 mwaka 2021 ambayo ni nzuri na yaafya,
Kenya wao inflation ilifikia asilimia 6.06 huku Rwanda ikipaa na kufikia asilimia 13.16 na Uganda ni asilimia 3.0 japo inflation imeendelea kupanda maeneo mengi,
Wakati huo huo huko duniani Venezuela wao hali ni mbaya zaidi kwani wanashika mkia kwa kuwa na inflation rate ( CPI ) ya asilimia 9,986,
Kwa Upande wa Africa Zimbabwe wanashika mkia kwa asilimia 56.8 ,
Zimbabwe wanaifanya SADC kuwa na ongezeko la inflation kwa mwaka 2020|21 linalofikia asilimia 3.5 na kuifanya SADC kuwa na annual inflation ya asilimia 46.9,
Inflation inachangiwa na mambo makubwa matatu ambayo ni Demand|Mahitaji ya bidhaa na huduma , Gharama za Uzalishaji|Cost of Production na Nguvu kazi au built in inflation
Tanzania kinachotusumbua ni "Cost Push Inflation " yaani mfumuko wa bei unaosababishwa na gharama za uzalishaji kupanda,
Hili limechangiwa zaidi na kuongezeka kwa bei za "mafuta" na kukosekana kwa Umeme wa uhakika wakati flani pia kupanda kwa malighafi mbalimbali,
Mpaka naandika makala hii mfumuko wa bei Tanzania kwa bidhaa na huduma kwa Vipimo vyote vya CPI,PPI na WPI unakisiwa kufikia kati ya asilimia 3 & 5 hii ni kwa mujibu wa ripoti ya mwisho ya BOT,
Tunaposema Tanzania ipo salama sana chini ya Mhe Samia Suluhu Hassan tunamaanisha haya,
Watanzania lazima tutambue kuwa kupanda kwa bei ya bidhaa na huduma Tanzania ni "JAMBO LA DUNIA NZIMA"
Kupanda kwa bei za bidhaa si jambo la Mama Samia Suluhu Hassan wala CCM, ACT-Wazalendo,NCCR-Mageuza au CHADEMA bali " Nijambo la dunia nzima" Tushikamane,
" Kilio cha wengi hugeuka sherehe "
VIVA TANZANIA VIVA || VIVA SAMIA VIVA