Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,889
Ni hao wakuu. Wandugu uchumi wa China na ukuaji wake ni jambo la kuogopesha sana kwa ukubwa wake. Miaka michache ijayo China itaongoza kiuchumi karibu kwenye kila sekta. Kwa huo uchumi mkubwa China amekuwa mtumiaji mkubwa wa malighafi duniani . Pia ukuwaji huo umetengeneza mamilioni ya matajiri wenye njaa ya kutumia. Kwahiyo China ni mtumiaji mkubwa sana wa malighafi na anaenda kuwa mtumiaji mkubwa wa consumer goods. Iliwabidi Mercedes wajenge kiwanda China baada ya kuzidiwa na mahitaji.
Zamani uchumi wa China ulishikwa na makampuni ya serikali lakini leo zaidi ya 60% ya uchumi unashikwa na sekta binafsi. Makampuni mengi binafsi ya China hayajawekeza nje ya China. Makampuni ya serikali ndiyo yametoka kuwekeza kwenye malighafi. Ndani ya China kuna competition ya hatarl. Kwa kila kampuni moja inayofanikiwa basi kuna maelfu yamekufa. Kwahiyo haya makampuni yana njaa sana ya kuwekeza nje maana licha ya competition pia mishahara inapanda kwa kasi. Mampuni mengi yameanza kuoperate Vietnam na Indonesia. Kuja Afrika CEO mmoja alisema miundombinu(Barabara, bandari, umeme) ni mibovu na kuwa tuna poor work ethics.
Tufanye nini ili tufaidike na soko la mamilioni ya matajiri wa China? Tufanye nini tufaidike na makampuni ya China yenye njaa ya kuoperate nje ya China?
Tufanye nini kufaidika na ukuaji wa uchumi wa China?