JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Safari ya timu ya taifa ya Tanzania kufuzu kucheza Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN 2023) imefikia tamati baada ya kupata kipigo cha magoli 3-0 dhidi ya Uganda, leo Jumamosi Septemba 3, 2022.
Kwa matokeo ya mechi hiyo iliyochezwa Uganda, Tanzania imetolewa kwa jumla ya magoli 4-0 kwa kuwa mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliochezwa Dar es Salaam wageni walishinda 1-0.
Hivyo, Uganda imefanikiwa kufuzu michuano hiyo kwa mara ya 6 mfululizo wakati Tanzania ikiwa na rekodi ya kushiriki mara mbili pekee.