FT: Algeria 0-0 Tanzania | AFCON Qualifier | Tanzania yafuzu AFCON

Teko Modise

JF-Expert Member
May 20, 2017
1,914
6,033
Algeria vinara wa Kundi F katika kufuzu kwajili ya AFCON watawaalika Tanzania (Taifa Stars) katika mchezo utakaofanyika katika dimba la Annaba huko Algeria.

Taifa Stars yenye alama 7 inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili iweze kufuzu huku Algeria ikikamilisha ratiba ikiwa na alama zake 15.

Pia Taifa Stars itakuwa inaiombea mabaya Uganda (The Cranes) katika mchezo wake dhidi ya Niger. Ikumbukwe Uganda ina point 4 ikishinda kwa magoli mengi itaweka rehani nafasi ya Taifa Stars.

Mechi zote ni saa 4:00 usiku

Kila la heri Taifa Stars🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿

========

TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imekata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani, 2023 baada ya sare ya bila kufungana na wenyeji, Algeria katika mchezo wa mwisho wa Kundi F usiku huu Uwanja wa Mei 19, 1956 mjini Annaba.

Kwa matokeo hayo Taifa Stars inamaliza na pointi nane, nyuma ya vinara, Algeria wenye pointi 16 na wote wanafuzu AFCON ya Ivory Coast 2023 wakizipiku Uganda iliyomaliza na pointi saba na Níger pointi mbili.
Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi F leo Níger wamechapwa mabao 2-0 na Uganda Uwanja wa Marrakech nchini Morocco.

Hii inakuwa mara ya tatu kihistoria kwa Tanzania kufuzu AFCON baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria na 2019 nchini Misri.

Bin Zubeir

1694113218797.png

1694120682099.png
20230908072403.png
 
Tukipata hata sare tu inatutosha. Ingawa kwa kiasi fulani natamani tukose hiyo nafasi ya kufuzu. Maana wachezaji wetu kwa kweli na kocha wao huwa siwaelewi kabisa kwa ule mpira wao wa papatu papatu!

Hivyo tukifuzu tutaenda tu kushiriki na kuendeleza ule ukichwa wetu wa mwendawazimu.
 
Back
Top Bottom