Tanzania: The Electronic And Postal Communications (Online Content) Regulations, 2017

hivi wanaomshauri Rais ni watu gani????

kwa nini wanamuweka Rais wetu kwenye vulnerable position kila siku?

ujinga watunge wao gizani,Rais ndio aje nayo kwenye media kudhalilika,

kwa nini nyie mnaomshauri Rais msikazanie kumuweka CLOSE na wananchi wake......?

kila siku baada ya speech ni another day ya 'matamko' kama sipangiwi etc,sasa hii inaleta picha gani??hamuoni mnaweka image ambayo inamuweka DISTANT na watu wake??

Mwisho,mkuu rais,kama kuiga tusiige mavazi tu kutoka amerika,tuige na freedom of speech,trump waliweka yale mamidoli makubwa,na Trump hakuwafunga,internet inakua kila siku kupigana nayo,ni kupigana na upepo.wastage of time and resources..................................

Besides,unafaidika na hii mitandao,ila its reality,you cant have the best of both worlds.
 
Dalili kubwa ya UDIKTETA hii inataka kulikumba Taifa letu pendwa.


GOD Forbid!
Hivi wamefikiria kuhusu cause and effect ya hichi wanachofanya, unapozuia/limit wananchi ku-vent kuhusu frustration zao( hapa nazungumzia frustrations ambazo zipo caused na mambo ya kisiasa, which is just about everything in this country).

Watu wana-tend kuhifadhi hizo frustrations moyoni and kutokana na kutokuwa na sehemu ya kuvent about them, hizo frustrations zitabuild up and reach a boiling point and at that moment, watu watakuwa tayari kwa lolote and do the unimaginable....

Basically serikali inatengeneza a ticking time bomb ambalo litakuja ku-errupt in such an uncontrollable manner, watashindwa kulizuia...
 
Kuna siku AKIDI itatimia tu ndani ya Bunge hata kupitia CCM wenyewe hapo ndio utaona utukufu wa Mungu na mabadiliko ya katiba kwenye kipengele cha Rais kutoshitakiwa ndio yatapatikana.

Haya wanayoyafanya ni upofu tu ila ni kitanzi kizuri sana kwao, unaweza kuzuia wanayama wakali kama Simba wasilete madhara kwa kutumia bunduki na vifaa vingine ila kwa binadamu ni swala la muda tu. Hakuna kiongozi yoyote duniani aliyeshindana na wananchi wake akashinda hiyo vita.

Kama viongozi wa nchi hii wanataka kuongoza kwa furaha wawaache wananchi waseme na wakosoe kuliko kuwapangia cha kufanya, ikumbukwe kila anayekosoa anataka kuona jambo likiwa zuri zaid kuliko lilivyo, sasa kama serikali yetu inaamini ipo kwa ajili ya watu basi iamini tu kuwa tunatumia njia nyingi kufikia lengo kama taifa, kwahiyo wanaokosoa kwa namna wanayoiona ni sawa nao wapewe uhuru wa kujieleza huko serikali nayo ikifanaya kwa namana inavyoona inafaa.

Kuimba tu NIA NJEMA bila kutoa haki za MSINGI ni kujisumbua tu kuligawa taifa na mwisho ni chuki.
 
Ukishakuwa na Uongozi usiothamini demokrasia, haya siyo ya kushangaza. Tunaoelewa mambo haya, tunajua yapo makubwa zaidi njiani. Wazalendo wote jifungeni mikanda tuone kama tutavuka kipindi hiki cha mpito.
 
Tumerudi enzi za ujima.

Zidumu fikra sahihi za mwenyekiti.

Kuna watu wanashangilia. Muda utaongea na historia itawahukumu.
 
Mhn! Wanazi wa vyama wanavyopenda kuporomosheana matusi, mtego huu utawanasa waliokuwemo na wasiokuwemo. Na hapo kwenye "indecent material " patanasa wengi.
 
Hizi ni regulations zisizo na sheria. Labda tuwaulize wanasheria what this means maana naamini haziendi Bungeni na zitaanza kutumika juu kwa juu
Mkuu hizi Ziko chini ya sheria ya "cyber crime Act"
 
Back
Top Bottom