Tanzania: The Electronic And Postal Communications (Online Content) Regulations, 2017

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,577
6,582
ILANI: Hizi sio kanuni za Sheria ya Makosa ya Mtandao.

Kanuni hizi zinakuja mwezi mmoja baada ya kuambiwa kuna sheria nyingine inakuja pia > Tanzania: Authorities drafting another law targeting the Cyberspace

Zimewekwa hapa: http://habari.go.tz/uploads/documents/sw/1505716716-Online Content Regulations - 20 January, 2017.pdf

- Kanuni hizi naamini bado ni draft (kama sijakosea)

- Zitagusa karibu kila kitu kinachoandikwa mitandaoni

- Hizi si kanuni za Sheria ya Makosa ya Mtandaoni

3b05f967029234e52ecd5d963c93dcd5.jpg


- Vyombo vya Habari vyenye kuwa mtandaoni navyo havitapona!

- Forums kama JF nazo zimeguswa!

1c625daaa2455281a76945eabecb3f71.jpg


- Social Media Platforms (hadi Makundi ya WhatsApp/Facebook/Instagram/Twitter) nako hakuko salama

0d59b9ef8b3967d95d59cece433835ec.jpg


- Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imepewa nguvu za kutosha kabisa!

4b8f37c83d1428656d2c5ca8222b9fa6.jpg


- Sect 5(1) inamtaka mwenye kumiliki mtandao kuhakikisha anakusanya taarifa za kutosha za wateja wake! (Inalengwa JF?).

- Sect 5(1) pia inamtaka mwenye kumiliki mtandao akiona kitu ambacho wao TCRA wamekwambia hakifai uwe umekiondoa ndani ya saa 12!

- Watanzania walio nje ya Tanzania (diaspora) nao wameguswa!

- Maneno FORUM yametumika mara nyingi kitu kinacholeta picha juu ya nani mlengwa haswa!

38f6df92bf07c138ce2d4e00a4b31a82.jpg


- Kanuni hizi zinakuja wakati JF ikiwa inakabiliwa na kesi 3 mahakama ya Kisutu na mojawapo ya kesi wanaoishtaki JF ni TCRA (kuwa na website yenye .com).

- Internet Cafe zitalazimika kuweka kamera za kunasa kila kinachoendelea ndani

f4387676ec6513c61d29e8548b036ba5.jpg


- Serikali yetu sasa inataka watu kuandika habari za kufikirika!

294603df95b68c645e915423402dfbe0.jpg


Na mwisho, Serikali yetu tukufu kupitia kwa Waziri ambaye ni msomi wa sheria na "Mmoja wa Wapambanaji walio ndani ya CCM" imeweka adhabu kali kwa atakayekiuka taratibu hizi!!!

8727ae5790134c6d457a1637035627d5.jpg


Je, TUTAFIKA?



UPDATE:

Serikali yakaribisha maoni ya wadau

47b9d6b24744eb7ffbb956f6bbd8cb31.jpg

de3003db62adabd20ed8b0c092a809a0.jpg

b8e9479f46bb9147a88f834fd1deee65.jpg
 

Attachments

  • 1505716716-Online Content Regulations - 20 January 2017.pdf
    387.4 KB · Views: 85
Kibatala yupo,

Hivi mwanza na mbeya huwa kuna mawakili?

Maana mawakili wenye nguvu,uthubutu ni Dar na Arusha

Hizi kanuni za kupiga chini mahakamani kwanza kwa kuzizuia zisifanye kazi,pili kufungua kesi ya kikatiba

Mambo mengi tunayoyajua yalianza kama habari za kufikirika,

Kuzuiwa kwa bombadia na wanaotudai ni mfano mzuri,serikali kukopa dola milioni 500 kwa riba ya dola milioni 400,ilianza kama tetesi,kutekwa kwa Roma,Ney wa Mitego

Hizi loophole wanataka kuziziba

Na kwamba habari ifutwe ndani ya masaa 12,Roma ilichukua zaidi ya siku mbili kwa bashite kusema atamleta!!!!! Sasa ukiifuta hiyo habari inakuwaje?
 
Kweli wamedhamiria

Halafu kuna baadhi ya kanuni humo zinapingana moja kwa moja na vipengele vya katiba

Also this is a fruitless endeavour, NO-ONE has ever tried to control the internet and won, not now not ever

Kwa hali inavyoendelea, nadhani ni muda muafaka Jamiiforums wawe na warrant canary na waanze kupublish transparency reports
 
Tumeshaanza kuzoea ironic rules hakuna kipya na hakuna cha kuogopa kwa vile tumeshajua ni serikali ya aina gani, wanaogopa ni wale wanadhani bado tuna serikali ya kidemokrasia, serikali ya kidikiteta haihitaji kanuni wala sheria inapohitaji kunyonga uhuru wowote.
 
Tumeshaanza kuzoea ironic rules hakuna kipya na hakuna cha kuogopa kwa vile tumeshajua ni serikali ya aina gani, wanaogopa ni wale wanadhani bado tuna serikali ya kidemokrasia, serikali ya kidikiteta haihitaji kanuni wala sheria inapohitaji kunyonga uhuru wowote.

Nawaonea huruma wapiga Makofi
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom