Tanzania: The Electronic And Postal Communications (Online Content) Regulations, 2017

Tanzania: The Electronic And Postal Communications (Online Content) Regulations, 2017

Sasa misheria kama hii,inasaidiaje kuinua hari ya mtanzania,kiuchumi,ki afya,ki elimu?.badala ya kutumia rasilimali hizi chache kuboresha kilimo,kiwe cha kisasa,tunapoteza muda kutunga sheria za ajabu ajabu,
Yaani bongo inafanywa kama ilivyokuwa soviet union chini ya ucomunist,na KGB,yaani kila unachofanya,kuongea,kuandika,kama kinakwenda kinyume na matakwa ya walio juu,umeumia,
Sisi tunataka open society kama magharibi,sio kuishi kama mazombie,
Hivi mnafikiri mtakaa hapo milele,IPO siku tutawachomoa,tuwatie adabu
 
Tumeshaanza kuzoea ironic rules hakuna kipya na hakuna cha kuogopa kwa vile tumeshajua ni serikali ya aina gani, wanaogopa ni wale wanadhani bado tuna serikali ya kidemokrasia, serikali ya kidikiteta haihitaji kanuni wala sheria inapohitaji kunyonga uhuru wowote.
Hii serikali nilishaipuuza
Hii kufunga watu midomo ktk dunia hii ni umbumbumbu tu.
Ukiziba hapa itatokea pale na mbaya zaidi ni kwamba hamna lolote la maana inalolufanya
 
Ni KENYA tu katika EAC ndie itanusurika na UDIKITETA. Na KENYA ndio itakuwa baba wa uchumi endelevu na kiini cha stability licha ya ukabila.

Mnajua UDIKITETA ni zaidi ya ukabila. Yetu macho.
 
Nakubalina na maneno ya zitto kuwa mihimili yote inaongozwa na washamba na malimbukeni
 
Duh yaani hii itakuwa kama North Korea inavyothibiti matumizi mitandao kwa raia wake. That's too much I can't stand it! Awamu hii ya tano inapeleka nchi kubaya kwa sheria kama hizi za kijinga.
 
Kibisa vita ya kikwete na lowasa imezaa hili dude


Yaani acha tu Mkuu

Mi namlaumu JK sababu yale mambo yalikuwa ya kukaa chini kama binadamu na tena wanaume kisha kuyajenga basi halas mambo yanakuwa settled.Na pia mzee Lowassa nae kwa upande wake hakutakiwa kudinda bali kuwa humble na kuyamaliza

Sasa wakamweka mtu wanaemtaka wao kama kamati kuu wakati Taifa na Demokrasia lilimtaka jamaa. Matokeo yake ndio haya tunayoyaona!
 
Halafu kuna mijitu humu ina comment, raisi wa China haongeagi English, jee sheria china zinaandikwa kwa English?
 
Tushazioea hizi sheria:ilianza ya makosa mtandaoni tukasurvive ikapita,ikaja ya takwimu ikapita,ikaja ya vyombo vya habari tukasurvive...ikaja ya mawasiliano mpaka leo tunadunda!
Leteni na hii tutasurvive tu!
Ukiziba njia mmoja,Mungu anafungua nyingine!
 
Sheria ni cyber crime act na hizo ni kanuni tuu...kwa hiyo hicho si kipya...hiyo sheria ilishapitishwa toka 2015 kwa hiyo usijaribu kufanya kama ni jambo jipya...
 
Na kama hivi yule mwenye uthubutu wa kutoka hadharani kutuhabarisha ubaya wa mambo kama haya keshapigwa risasi yuko hoi hospitalini. Nani wa kutusemea? Job naye kauza taasisi yake kwa mhimili mwingine. Tutaponaje?
 
Back
Top Bottom