Bukyanagandi Ipo siku mtanielewa, tatizo langu ni kwamba sijui kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa, huwa naiweka wazi jinsi ilivyo. Wabongo nyie shida yenu mnapenda kulalamika kwa kila kitu, kwamba mnaonewa, yaani kila kitu ni nyie mnaeonewa. Hii mada ipo kwa ajili ya Burudni, jinsi ndugu zetu kule wanaendelea kuuawa kinyama, kwamba suluhu inafaa ipatikane haraka na kusitisha maafa zaidi. Halafu ghafla nyie mumeibuka na yale malalamiko yenu ya kawaida eti vurugu zimeanzishwa Burundi kusudi ndio mzuiwe kuwafikia Wakongo kwenye matumizi ya bandari.
Mimi nimefanya kazi na Wabongo kwa muda, na kwa kweli hilo la kulalamika ovyo hamjambo. Lipo sana ndani yenu. Unakuta hata boss Mtanzania na anawalipa mshahara sawa na wengine wote, lakini wageni humo wanajituma ila Wabongo siku kutwa ni malalamiko tu jinsi wanavyoonewa. Mara hiki mara kile, na muda mwingi hawajitumi, hawaonyeshi sababu za wao kuongezwa mishahara, bora hata ulalamike ilhali unajituma, boss ataona ubora wako na afanye kitu. Lakini hapa unalalamika muda wote, ila hata muda wa kuingia kazi hauzingatii, halafu kila mara unaomba ruhusa mara msiba, mara harusi mara mgonjwa n.k.
Fuatilia hii mada hapa chini uone kuna baadhi yenu wameliona hili na wapo tayari kubadilika, ila wengine mtaishi kulaumu tu
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...i-cha-wasomi-wezi-na-wavivu.html#post14951457