Mkuu sijui kama umenielewa!! Burundi ina eneo kubwa - sasa inakuwaje vurugu zinazo tokea kwenye kiunga kimoja cha Bujumbura ndio tuchukulie kwamba kundi dogo hilo ndio wasemaji wa Warundi wote au ndio wanao juwa demokrasia kuliko majority ya Warundi - cha kujiuliza kuna nini nyuma ya pazia.
Ubakaji wa Demokrasia unaingiaje hapa kwani juzi juzi hapa Nkuruzinza hakupigiwa kura na Warundi wenzake? Sisi watu wa nje kwa nini tunamkalia kooni Nkuruzinza eti "amebaka demokrasia" kwa nini hatujiulizi hivi Nguezo kakaa madarakani kwa vipindi vingapi, Museveni na PK - hilo hamlioni!! Nkuruzinza si amesema hii ndio itakuwa term yake ya mwisho, kwa nini tikivuta subira na kuona akimaliza kipindi chake ataondoka madarakani au la?
Kuna kundi dogo la watu ndani na nje ya Burundi ambao wamepania ku-dramatise masuala ya kisiasa nchini Burundi, hao ndio wana sababisha mauuaji ili Burundi ionekane inakaribia ku-commit genocide wakati hiyo haina ukweli wowote, hivi tukitembelea vijiji vya Burundi na miji mingine si pako shwari tu - je hizo ni dalili za vita vya wenyewe kwa wenyewe kweli??
Nkuruzinza aliwahi kusema kipindi cha cha Uongozi wake wa kwanza baada ya kumalizika civil war kilikuwa ni kipindi cha mpito hivyo mananchi hawakumpigia kura - kwa akili za kawaida mtu uwezi kuchukulia kipindi cha mpito kama ni kipindi cha demokrasia kutokana na wananchi kutopewa fursa ya kupiga kura na kumchagua kiongozi wanaye mpenda, binafsi naona hatumtendei haki Nkuruzinza kwa kumshutumu kwamba amepania kug'ang'ania madarakani - kipindi cha mpito hakipaswi kujumuishwa - tuanzie kipindi ambacho Warundi walipiga kura kwa mara ya kwanza Chini ya Uongozi wa Nkuruzinza hiyo ndio maana halisi ya Demokrasia, kwa hiyo kihualisia Nkuruzinza yupo kwenye term yake ya pili na ya mwisho wa Uongozi wa Demokrasia Nchini Burundi,hilo kwa nini watu hawalioni/ignore. Chukulia Nchi kama Uganda hivi baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe(Museveni na Obote) Museveni alipo shinda vita iliwachukuwa muda gani Waganda kuchagua Viongozi wao kwa njia ya kidemokrasia/kupiga kura?? Sasa imekuwaje tena wakina M7 wamuone Nkuruzinza kakosea - wanajifanya wamesahau waliko toka.