Tanzania nchi yenye ardhi nzuri kwa kilimo na makazi lakini wananchi wake ni masikini

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Tanzania nchi yenye kila aina ya raslimali nchi yenye nguvu kazi ya kutosha watu mil.60

Nchi yenye ardhi nzuri kwa kilimo na makazi lakini wananchi wake ni masikini wa kutupwa wamerundikiwa furushi la tozo kila mwananchi kalibeba furushi

Ili tuyaepuke hayo maisha ni muhimu katiba mpya ikapatikana ili tuwe na siasa safi na viongozi watakao wajibishwa na wananchi sio wananchi wawajibishwe na viongozi kama sasa Serikali ni ya wananchi sio ya viongozi

Sent from my sm-j600f using jamiiforums mobile app
 
Bd kdg
IMG-20210821-WA0008.jpg
 
Tanzania Nchi Yenye Kila Aina ya RASLIMALI Nchi yenye Nguvu kazi ya Kutosha Watu Mil.60
Nchi yenye ARDHI nzuri kwa KILIMO na MAKAZI lakini Wananchi Wake ni MASIKINI wa KUTUPWA wamerundikiwa FURUSHI la TOZO kila Mwananchi KALIBEBA FURUSHI
Ili Tuyaepuke hayo Maisha ni Muhimu KATIBA MPYA ikapatikana ili Tuwe na SIASA SAFI na VIONGOZI watakao Wajibishwa na WANANCHI sio Wananchi Wawajibishwe na VIONGOZI kama sasa
SERIKALI ni Ya WANANCHI sio ya VIONGOZI

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
Mwananchi lipa tozo kuipaisha nchi yako, usiwe mvivu wa kufikiri. Katiba mpya haitatoa kodi kwa wananchi katika nchi hii.

CHANGIA, CHANGIA, CHANGIA............
 
Tunatuma tozo inapobidi, tumerudia zile njia za kuweka pesa dukani kwa Wapemba Kinondoni na ndugu yako anachukua kwa mdogowake Dodoma
Utapotapeliwa pesa yako yote ndio utapokumbuka kuwa ni bora ungetoa tozo na kuepuka short cut ambayo ni wrong cut.
 
Sawa mke wa Mwigulu.
Endeleeni kujaza matumbo yenu kwa pesa za dhuluma.
Ipo siku, narudia Ipo Siku
Pole kwa kuguswa na maelezo yangu. Lakini kama kujenga zahanati, kutengeneza barabara za vijijini unakutafsiri kama kujaza matumbo, itakuwa tunasafari ndefu.

CHANGIA, CHANGIA, CHANGIA mwananchi kwa maendeleo ya nchi yako, afya na mawasiliano.
 
Huku tozo huku wanakopa.Au ndo mambo ya jiwe kujenga kwa pesa za ndani huku wanakopa
 
Pole kwa kuguswa na maelezo yangu. Lakini kama kujenga zahanati, kutengeneza barabara za vijijini unakutafsiri kama kujaza matumbo, itakuwa tunasafari ndefu.

CHANGIA, CHANGIA, CHANGIA mwananchi kwa maendeleo ya nchi yako, afya na mawasiliano.
Sawa nitachangia ili Miss Vasco Da Gama aendelee kudhurula kila Kona ya dunia
 
Pole kwa kuguswa na maelezo yangu. Lakini kama kujenga zahanati, kutengeneza barabara za vijijini unakutafsiri kama kujaza matumbo, itakuwa tunasafari ndefu.

CHANGIA, CHANGIA, CHANGIA mwananchi kwa maendeleo ya nchi yako, afya na mawasiliano.
Tulia wewe mke wa mwigulu, unadhani zahanati Ni majengo

Kitulize kimshono , subiria alizeti kutoka kijijini

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Tuliishi maisha haya kabla ya miamala, hakuna jipya.
Hata huko nyuma tuliishi maisha ya shule ya msingi yenye wanafunzi 100 darasa la saba na kufaulu 3 tu kuendelea na sekondari, chuo kikuu kimoja, na hospitali ya rufaa moja tu na... na... na.......

Tulisafiri na mamilioni ya mapesa mfukoni toka mwanza kwenda kununua gari Dar huku hofu ya kutekwa gari na kupoteza mamilioni yaliyopo kwenye begi yalikuwa makubwa sana. Leo uko mwanza unamlipa mamilioni mfanya biashara Dar akutumie hardwares na biashara mmemaliziana. Sizungumzii biashara za kwenye mtandao ambazo zinapamba moto, watu wanalipana na kutumiana bidhaa bila kujuana wala kuonana.

Kama huoni hizi tofauti za jana na leo, we baki tu huko. Mi natoa tozo na kusave pesa ya usafiri ya kufuata mzigo Dar, na kwa ajili ya usalama wa pesa zangu.
 
Pole kwa kuguswa na maelezo yangu. Lakini kama kujenga zahanati, kutengeneza barabara za vijijini unakutafsiri kama kujaza matumbo, itakuwa tunasafari ndefu.

CHANGIA, CHANGIA, CHANGIA mwananchi kwa maendeleo ya nchi yako, afya na mawasiliano.
Si uchumi wa kati hiyo hizo tozo za nini
 
Tulia wewe mke wa mwigulu, unadhani zahanati Ni majengo

Kitulize kimshono , subiria alizeti kutoka kijijini

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
Ni kweli zahanati ni Majengo, kwa tafsiri kuwa hatuwezi kumhifadhi mgonjwa wakati kuna mvua kali au jua kali kwenye mti wa muembe au kumzalisha mamawatoto barabarani.

Tunaanza na majengo ambayo unaweza kuyajenga kwa mwaka mmoja tu, lakini Nesi na Daktari inachukua miaka kumuandaa. Hivyo si dhambi tukaanza na majengo na baadae tutakuja kwenye wataalam na vifaa.

Ni nyie ndio mnakuwa mbele kuposti wagonjwa wakipata huduma katika kivuli cha miembe, barabarani au vichakani na kusema serikali haifanyi kitu

Anza kuchangia leo, CHANGIA, CHANGIA, CHANGIA ...........
 
Back
Top Bottom