Tanzania: Kushuka kwa thamani ya shillingi, mfumuko wa bei na siasa zetu!

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Jamani watanzania wenzangu.

Tangu Serikali ya awamu ya nne iingie madarakani shillingi imezidi kushuka thamani sambamba na mfumuko wa bei!

Swali la Kujiuliza, Rais wetu hana wachumi? Au hao wachumi wanamshauri nini rais wetu.

Raisi Mkapa wakati anaingia madarakani kulikuwa na mfumuko mkubwa wa bei ulioachwa na Mzee Mwinyi. Rais Mkapa aliweza kuudhibiti na bei hazikupanda ovyo ovyo, pia shillingi ilikuwa strong.

Sasa wakati wa Kikwete Shillingi imeporomoka thamani saaaana! Bei za bidhaa muhimu kama Sukari, Mafuta ya kula, unga wa kula - ngano, mahindi; mafuta taa. Mishahara au vipato vya watanzania havijapanda katika uwiano sawa na bei za vitu kupanda. Maisha ya watanzania yamekuwa ya shida zaidi.

Rais achukuwe Hatua ikiwepo 'Economic Stimulus'

Labda kodi kwenye bidhaa muhimu kama sukari, ugali, mchele, chapati zimepunguzwe.

Mie sio mchumi, naomba wachumi wanisahihishe hapa
Posted by dosama | May 15, 2012

TAMKO LA NEC JUU YA KUPANDA KWA GHARAMA ZA MAISHA NCHINI.

Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imejadili kwa kina suala la kupanda kwa gharama za maisha nchini. NEC inakiri kwamba ni kweli lipo tatizo la kupanda kwa gharama za maisha nchini. Tatizo hili pia limezikumba karibu nchi nyingi za Afrika Mashariki na kwakweli karibu sasa lipo dunia nzima. Baadhi ya sababu za kupanda kwa gharama za maisha hapa nchini ni pamoja na;

1. Hali mbaya ya mavuno inayotokana na uhaba wa mvua au mvua kunyesha kipindi cha nje ya msimu katika maeneo mengi nchini.

2. Kuongezeka kwa bei ya mafuta duniani, hivyo kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wa bidhaa na usafirishaji wa mazao.

3. Kuyumba kwa thamani ya dola ya Marekani.*

4. Kuwepo kwa soko huria ambapo sasa *mazao ya chakula yanapata soko nje ya nchi, na wakati mwingine kuuzwa nje kwa njia ya magendo na hivyo kusababisha uwepo wa ukubwa wa mahitaji na hivyo kuongezeka kwa bei ya chakula nchini.*

5. kuongezeka kwa walaji wakati uzalishaji ukiwa mdogo.

6. kutofanikiwa (ikiwemo kuhujumiwa na wafanyabiashara wasio waaminifu) kwa baadhi ya mikakati ya kudhibiti mfumko wa bei.

Uwamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

1. Pamoja na Serikali kuendelea kuchukua hatua za muda mrefu na wa kati za kukabiliana na tatizo hili, CCM inaiagiza Serikali kuchukua hatua za haraka za muda mfupi ikiwemo kuangalia upya baadhi ya kodi katika vyakula pamoja na kodi ya ongezeko la thamani VAT katika sukari.

2. Utaratibu wa ruzuku ya mbegu na mbolea upanuliwe ili kunufaisha wakulima wengi.

3. Serikali iongeze kasi ya utekelezaji wa mpango wake wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula nchini, hasa kwa kupitia Hifadhi ya Nafaka ya Taifa, ikiwa ni pamoja na kujenga maghala zaidi ya mazao ya chakula katika maeneo ya uzalishaji wa mazao, na kutenga fedha nyingi zaidi kwa ununuzi wa mazao hayo. Pamoja na hili, mipango ifanywe kuongeza uwezo wa wakulima kuhifadhi chakula chao wenyewe na kupunguza upotevu baada ya mavuno (post-harvest losses).*

3. Serikali iendelee kupanua utaratibu wake wa kutumia Hifadhi ya Nafaka ya Taifa (SGR) kama nyenzo ya kudhibiti kupanda kwa bei za vyakula. Wakati wa uhaba wa vyakula katika maeneo ya mijini, kasi ya kupeleka chakula maeneo hayo iongezwe na utaratibu mzuri zaidi wa usambazaji wa chakula utumike ili walaji, na sio wasafirishaji na wasindikaji, wanufaike.

4. Serikali iongeze kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kilimo nchini, hasa ASDP na SAGCOT, ambayo itasaidia kumaliza tatizo la chakula nchini na kuongeza ajira na kipato kwa Watanzania walio wengi.

5. Serikali idhibiti malipo ya huduma ya ndani kwa kutumia fedha za kigeni, hasa dola za kimarekani. Aidha, Serikali iongeze udhibiti wa Maduka na mahoteli yanayofanya biashara ya fedha za kigeni ili kuondoa hujuma kwa uchumi wa nchi inayofanywa kutokana na uhuru uliokithiri katika biashara hii.*

6. Waajiri wahimizwe kupandisha mishahara na malipo mengineyo kwa wafanyakazi wao ili waweze kumudu gharama za maisha.

7. Serikali iweke jitihada zaidi za kudhibiti ulanguzi wa bidhaa muhimu na upandishaji holela wa bei za vyakula, kodi za nyumba na usafiri.

Nape Moses Nnauye | Chama Cha Mapinduzi | Ideology and Publicity Secretary
 
BOT inalifanyia kazi suala hilo haliweze kutokea overnight tuwe wavumilivu na utendaji wa serikali yetu ya awamu ya nne mambo yatakuwa swali mkuu
 
BOT inalifanyia kazi suala hilo haliweze kutokea overnight tuwe wavumilivu na utendaji wa serikali yetu ya awamu ya nne mambo yatakuwa swali mkuu

Duh . Tuvumilie hadi lini? 4 years down the line gone for ever. BOT is full of problems from EPA to nepotism and can't solve them.

BOT itself is the source of mfumuko wa bei ,wataweza kutatua hili? Wewe bwana usicheze na mtu ambaye umemwamini akulindie mali zako halafu akaziiba .Ni hatari, maana hajali kitu. BOT iko hivyo hivyo haijali kitu maana kama ingekuwa inajali ingelinda hizo pesa zetu zilizibiwa na mafisadi kwanza then ingethibiti mfumko wa bei maana ni moja ya kazi zao enzi hizo za Mwalimu.
 
Mfumko wa bei Kenya ni 22% Burundi ni 20% na Rwanda ni 15%!

Ktk EA Tz ndo mfumuko wa bei uko chini zaidi!

Kwani kila kitu JK ni tatizo? Tuwe waungwana na kuwa positive kidogo kwake- may be tumpe mda zaidi kidogo!
 
BOT inalifanyia kazi suala hilo haliweze kutokea overnight tuwe wavumilivu na utendaji wa serikali yetu ya awamu ya nne mambo yatakuwa swali mkuu

Hii ni kauli ya kisiasa kweli, na hii ni 2009 JK ameingia madarakani 2005 tusubiri mpaka lini tena. Kwanini tusi admit kuwa uchumi pamoja na kuwa yeye ni mchumi umemshinda? Let us face it,
una excuse nyingi ya kwanza inaweza kuwa msukosuko wa uchumi duniani, nyingine inaweza kuwa bei ya mafuta, nyingine inaweza kuwa ile na hii....sababu ambazo hata Mkapa angeweza kuzitoa. Cha muhimu ni kwa hana watu makini na hajaweza kuprovide leadeship kama iliyokuwepo wakati wa Ben.
Ndiyo hivyo kwenye siasa za Tanzania, Julius alijenga, Ali alibomoa, Ben Akajenga Jakaya anabomoa. Au Julius alibomoa Ali akajenga, Ben akatuuza kwa wawekezaji, Jakaya anataka kutukomboa ndio hivyo tena.
 
Jamani watanzania wenzangu.

Tangu Serikali ya awamu ya nne iingie madarakani shillingi imezidi kushuka thamani sambamba na mfumuko wa bei!

Swali la Kujiuliza, Rais wetu hana wachumi? Au hao wachumi wanamshauri nini rais wetu.

Raisi Mkapa wakati anaingia madarakani kulikuwa na mfumuko mkubwa wa bei ulioachwa na Mzee Mwinyi. Rais Mkapa aliweza kuudhibiti na bei hazikupanda ovyo ovyo, pia shillingi ilikuwa strong.

Sasa wakati wa Kikwete Shillingi imeporomoka thamani saaaana! Bei za bidhaa muhimu kama Sukari, Mafuta ya kula, unga wa kula - ngano, mahindi; mafuta taa. Mishahara au vipato vya watanzania havijapanda katika uwiano sawa na bei za vitu kupanda. Maisha ya watanzania yamekuwa ya shida zaidi.

Rais achukuwe Hatua ikiwepo 'Economic Stimulus'

Labda kodi kwenye bidhaa muhimu kama sukari, ugali, mchele, chapati zimepunguzwe.

Mie sio mchumi, naomba wachumi wanisahihishe hapa

Mkuu kuna baadhi ya mambo hayahitaji uwe mchumi, ni common sense tu. Lakini inashangaza sana kuona hayafanyiki, wakati mwingine unatambua kuwa hakuna anayemjali mpiga kura. Nadhani inatakiwa wakati wa uchaguzi wanayosema wapiga kura yawe yanahifadhiwa, na baadaye kuwauliza wameyatekeleza vipi.
 
Mfumuko wa bei ulionekana wazi mara tu alipoingia Kikwete madarakani.
Yeye ni mchumi aliyetuahidi maisha bora lakini unaweza kujionea mwenyewe jinsi hali inavyozidi ku tight kila asububuhi.
Watanzania tumeshakuwa ni kichwa cha mwenda wazimu. Kila raisi anajaribu kufanyia majario ya kutawala kwetu.
 
Mfumko wa bei Kenya ni 22% Burundi ni 20% na Rwanda ni 15%!

Ktk EA Tz ndo mfumuko wa bei uko chini zaidi!

Kwani kila kitu JK ni tatizo? Tuwe waungwana na kuwa positive kidogo kwake- may be tumpe mda zaidi kidogo!

Ukikatika kidole, knowledge kwamba kuna watu wamekatika miguu inakupunguzia maumivu?

Sisi tunajua hii awamu ya sasa ilikabithiwa uchumi wenye kasi ya mfumuko wa bei ya 4.5%. Kwa nini wameshindwa kuupunguza zaidi, na badala yake kuupandisha? Mbona awamu iliyowatangulia ilipokea uchumi wenye kasi ya mfumuko wa bei ya 30% na wakaweza kuushusha hadi hiyo 4.5%?
 
....Wakulu swala la kwamba tumuongezee muda kidogo JK ni kujimaliza kabisaaa. Hapa sera ziwe kama slogan ya Obama ''..we plan and implement straight away,..if we find that the plan is not working kick it out and find new move..'' High level managent kawaida mtu anatakiwa kupewa only 3 years akishindwa kuperform kick of get somebody else. Mfumo huu ni maarufu sana katika nafasi za u Chief Executive Officer's (CEO) or Managing Director's (MD).

Alichokifanya JK juu ya uchumi wa Bongo hakina tofauti na kilichotokea katika uchumi wa Marekani tofauti na scope ya economy itself. Kule malekani Bushi kachukiwa kulikorais yeyote aliyewahi tawala malekani na hivyo kurahisisha ushindi kwa wapinzani wake ..why not Tanzania????. Tanzania ingekuwa ni private Company na JK kaajiriwa kama Chief Executive surely angekuwa fired withing the first year of service kwa kigezo kidogo tu. First annual Plan and Budget ilifeli kwa kiwango kisichovumilika pasipokuwa na maelezo, mbaya zaidi pamoja na hilo haikufanyika review kurekebisha Plan.

Review iliyofanyika juzi juu ya swala la mfumuko wa bei kutoka 13.5% mpaka 7..% ifikapo Juni, 2009 pia na false itafeli vibaya kwasababu mikakati (strategies) haiendani na target. Kimsingi anatuyeyusha. Nchi inatakiwa iendeshwa kwa semester system maana watu hawawajibiki kabisa.
 
Mfumuko wa bei ulionekana wazi mara tu alipoingia Kikwete madarakani.
Yeye ni mchumi aliyetuahidi maisha bora lakini unaweza kujionea mwenyewe jinsi hali inavyozidi ku tight kila asububuhi.
Watanzania tumeshakuwa ni kichwa cha mwenda wazimu. Kila raisi anajaribu kufanyia majario ya kutawala kwetu.

...more data, Mkapa alipokea inflation kwa Ali 48% akaikabidhi kwa JK 4%! Alikuwa na nia ya single digit inflation! Good work. Mtu akisema mafuta or world economy e.t.c ndio sababu, mbona Swaziland, Botswana, South Africa and so have stable inflation? Tunaruhsu hata maduka kuuza vitu kwa US$ hapa kwetu? Kikwete na Mugabe tofauti ndogo sana. I doubt upstairs ya mkuu wetu
 
Jamani
Angalia mfumuko wa bei unavyotuleta maisha boarer kwa kila mtanzania
Mshahara wangu wa 2005 umeongezeka mara tatu zaidi hadi hiv sasa lakini mfumo wa bei umemeza ongezeko lote

Watanzani tubadilishe haya maisha boarer
 
Attachments

  • BUGET.pdf
    44.7 KB · Views: 107
Bahati mbaya kuna ma **** ambao hawajui kitu. Wamepewa fulana na kofia wanamshangilia. Nikawauliza, 'Kafanya nin?' Eti 'Kafanya mengi!' 'Yapi?' 'Tuna amani. Wapinzani wateleta vita.'
My heart broke. Nilitaman kumusagasaga ubongo wake. Duh.
Nimepita Mbeya. Sugu anapeta. Vijana wanamkubali. Wanavaa ID za Dr. Slaa.
 
kikwete na familia yake ya mafisadi (na vilaza) wanafilisi hii nchi. Kama Kikwete akitumia maguvu kuingia term ya pili, nchii hii itageuka kuwa kama Zimbabwe
 
Bahati mbaya kuna ma **** ambao hawajui kitu. Wamepewa fulana na kofia wanamshangilia. Nikawauliza, 'Kafanya nin?' Eti 'Kafanya mengi!' 'Yapi?' 'Tuna amani. Wapinzani wateleta vita.'
My heart broke. Nilitaman kumusagasaga ubongo wake. Duh.
Nimepita Mbeya. Sugu anapeta. Vijana wanamkubali. Wanavaa ID za Dr. Slaa.

Fulana na kofia zisikutie hofu hata mimi juzi nipewa na mgombea mahanga nikaikubali nimepata dekio la nyumba.Ila kuna taarifa wana-ccm wengi wanavaa tu lakini wanjua kura yao inakwenda kwa nani.
 
Tangu baada ya uchaguzi kumekuwa na mfumuko mkubwa wa bidhaa muhimu nchini. Ninafahamu kiasi kuhusu 'Soko huru (huria?)' lakini kwa hali najikuta napata maswali mengi:

1. Ni nani (mtu au idara au wizara) anayehusika na regulation ya soko?
2. Soko huru (huria?) linasimamiwa na nani? Au linajisimamia?
3. Je, kuwa na soko huru (huria?) kunamaanisha kuwa serikali kuu haina udhibiti wa bei?
4. Ukimya huu wa Serikali kuu kuhusiana na mfumuku huu wa bei maana yake nini?

Naghafilika.
 
2. Endapo soko huru (huria?) linajisimamia lenyewe, walaji wanalindwa na nani?
3. Je, kuwa na soko huru (huria?) kunamaanisha kuwa serikali kuu haina udhibiti wa bei?
4. Ukimya huu wa Serikali kuu kuhusiana na mfumuku huu wa bei maana yake nini?

Naghafilika.
 
Tangu baada ya uchaguzi kumekuwa na mfumuko mkubwa wa bidhaa muhimu nchini. Ninafahamu kiasi kuhusu 'Soko huru (huria?)' lakini kwa hali najikuta napata maswali mengi:

1. Ni nani (mtu au idara au wizara) anayehusika na regulation ya soko?
2. Soko huru (huria?) linasimamiwa na nani? Au linajisimamia?
3. Je, kuwa na soko huru (huria?) kunamaanisha kuwa serikali kuu haina udhibiti wa bei?
4. Ukimya huu wa Serikali kuu kuhusiana na mfumuku huu wa bei maana yake nini?

Naghafilika.

Subiri kidogo, mkuu wa nchi hajamaliza kuunda serikali. Mfumko utatulia atakapomaliza kuwanunulia viongozi wa serikali yetu mpya ma- vx na akimaliza kulipa madeni ya Dowans na kulipa bill za uchaguzi na ku nini vile??? nk

Mwanangu twafwaaaaa, ila usikate tamaa.
 
soda 600 mtaani hakuna anayeuliza wkt kiwanda kinasema retail price 500 hivi maafisa biashara wa wilaya wapo?kazi yao nini au kutoa leseni basi
 
Back
Top Bottom