Tanzania: Kushuka kwa thamani ya shillingi, mfumuko wa bei na siasa zetu!

ndugu katika jf, nilienda jana kununua bidhaa za kibandani kwangu bei nilizo zikuta zikanifanya ninunue bidhaa 2/3 ya kiwango nilichopanga kununua. je hali hii tutafika?
je tatizo lipo Arusha tu au na mikoa mingine?

Mfumko wa bei umeshuka toka 13% mpaka kufikia 5.6% ni tafauti na jirni zet ambapo makwao ni avarage ya 9.5%

Uchumi wetu unaenda vizuri kulinganisha na nchi nying afrika na wataalam wa uchumi wanatabiri kama Tanzania itaendelea na nguvu zake za uchumi kwa muda wa miaka kui nchi itakuwa mbali

Vyama vya upinzani hawana cha kuikejeli serikali na ukuuaji wa uchumi kwa sababau wkina Mchungaji Slaa na wenzakehawana uwezo wa kujieleza au kuuzungumzia uchumi kutokana na elimu aliokuwa nayo haisadii ktk karne hii ya sayansi na technologia
 
Dah! Mi mwenyewe leo nimetoka na waifu wangu kupata moja baridi moja moto na k-moto, dah! Bill iliyokuja toka jikoni nilitamani kukimbia.. Eti kilo ya k-moto ni elfu 7000 toka elfu 5000, kesho napaki vitu vyangu narudi kijijini.

Haya yote yamesababishwa na sisi wenyewe wadanganyika kwa kukubali kudanganyika.
 
Mfumko wa bei umeshuka toka 13% mpaka kufikia 5.6% ni tafauti na jirni zet ambapo makwao ni avarage ya 9.5%

Uchumi wetu unaenda vizuri kulinganisha na nchi nying afrika na wataalam wa uchumi wanatabiri kama Tanzania itaendelea na nguvu zake za uchumi kwa muda wa miaka kui nchi itakuwa mbali

Vyama vya upinzani hawana cha kuikejeli serikali na ukuuaji wa uchumi kwa sababau wkina Mchungaji Slaa na wenzakehawana uwezo wa kujieleza au kuuzungumzia uchumi kutokana na elimu aliokuwa nayo haisadii ktk karne hii ya sayansi na technologia
Acha uwongo.
Mfumko wa bei hivi sasa ni 14%. Badala ya kushuka unapanda kila kukicha. Angalia bei ya sukari na mkate kulinganisha na wakati Mkapa alipoondoka mamlakani ndipo useme. Usitetee visivyoweza kutetewa.
 
Jasusi kila kitu kimepanda kilo ya nyama, kilo ya mchele, gunia la mahindi, maharage n.k. Binti Ashura hali ndiyo itazidi kuwa mbaya maana bei ya petroli katika soko la dunia inatazamiwa kupanda kwa kiwango kikubwa na hii upandaji wake huathiri kila bidhaa muhimu.
 
Kwani huo mfumuko wa bei unasababishwa na nini?
Shaycas,
Umeuliza swali zuri. Mimi si mwanauchumi, lakini sababu mojawapo kubwa inayopelekea kupanda kwa gharama za maisha ni serikali kushindwa kudhibiti matumizi. Sababu nyingine ambazo wanauchumi watakwambia ni supply and demand kwamba soko lina bidhaa zisizoweza kukidhi demand. Lakini kwa Tanzania sababu kubwa ni serikali kushindwa kudhibiti matumizi, mfano umesoma mahali katika jukwaa hili Mkullo anakodisha ndege dola elfu tano kumpeleka Dodoma wakati huo huo anamwamuru dreva wake amfuate huko kwa gari kwa gharama ya serikali. Yanayotokea katika wizara ya Mkullo yanatokea katika kila wizara pamoja na Ikulu pia. Itafika wakati tutalazimika kuchapisha hela kama alivyofanya Mugabe huko Zimbabwe.
 
ndugu katika jf, nilienda jana kununua bidhaa za kibandani kwangu bei nilizo zikuta zikanifanya ninunue bidhaa 2/3 ya kiwango nilichopanga kununua. je hali hii tutafika?
je tatizo lipo Arusha tu au na mikoa mingine?

Mambo kama haya ndio sababu ya kuandamana, sio kuandamana kwa ajili ya meya mmoja!
 
Kwani huo mfumuko wa bei unasababishwa na nini?

Kwa ufahamu wangu mdogo, hili nilitegemea sana kutokea miezi michache ijayo. Uchaguzi umeingiza pesa nyingi sana katika mzunguko wa pesa.Pesa zilizoingizwa hazikutokana na production ni zawadi na hongo.
Pili, inaweza changiwa na trade imbalance kati ya import and export inayopelekea kushuka kwa thamani ya shilingi.
Wachumi tusaidieni zaidi.
 
ndugu katika jf, nilienda jana kununua bidhaa za kibandani kwangu bei nilizo zikuta zikanifanya ninunue bidhaa 2/3 ya kiwango nilichopanga kununua.

Je, kwa hali hii tutafika? Je, tatizo lipo Arusha tu au na mikoa mingine?

WATANZANIA NI WANGAPI HADI SASA (2005 - 2010) WENYE MAISHA BORA NA HADI HIVI SASA (2010 -2015) WAO WANAJIBIDISHA TU KUTAFUTA KIADA CHAKE NCHINI????

Watanzania wenzangu tuambizane ukweli hapa na tusifichane hali halisi ndani ya mifuko yetu. Mpaka hivi sasa wengi wetu HATUZUNGUMZII TENA UCHUMI wa maisha yetuTanzania bali hali halisi ni UCHUMA wa maisha yetu nchini. Je, wewe????

Baya zaidi, ajabu ninayoiona nkule bado CCM na JOPO LA MAFISADI wangependa Watanzania wote tukaseme tu YOTE NI MAISHA na kukimbilia kitanndani, baada kucheka na Masanja TBC, huku CC ya CCM wakibariki Dowans walimpwe.

Huku waliosbobea katika uchumi nchini wanatutahadharisha KIAMA DOWANS WAKILIPWA na kuongeza kuongeza kwamba tunachoona mpaka sasa kwa gharama ya maisha eti hapo bado ni mwanzo tu wa mapinduzi ya sinema nzima wa ahadi ya Maisha BORA ZAIDI kwa kila Mtanzania; na katika kutimiza hilo Mhe Kikwete na CCM wametuhakikishia dhamira zao za kutufikisha huko kwa Nguvu Zaidi, Ari Zaidi na Kasi Zaidi.

Sasa Mtu endapo utakuwa hauoni MAISHA BORA ZAIDI basi wala usisubiri kuambiwa na mtu, Wenye kuona UGUMU ZAIDI KWA KILA NAFSI YAKE huyu si Mtanzania tena maana WATANZANIA WOTE waliopata ahadi hizo tangu siku nyingi tu (2005 - 2010) maisha yao ni bora kabisa hivi sasa (2010 - 2015) wanacho kitafu kiukweli ni Uziada wa UBORA HUO WA MAISHA.
HOJA YANGU:

Kwa mantki hiyo Mhe Kikwete na CCM, watu wa Takwimu nchini acheni kutu fikicha ukweli, Watanzania ni wastani wa watu wangapi nchini maana hili la watu milioni 46 wala sihitaji tafsiri ya mtaalamu kubani kwamba si kweli.
 
Mfumko wa bei umeshuka toka 13% mpaka kufikia 5.6% ni tafauti na jirni zet ambapo makwao ni avarage ya 9.5%

Uchumi wetu unaenda vizuri kulinganisha na nchi nying afrika na wataalam wa uchumi wanatabiri kama Tanzania itaendelea na nguvu zake za uchumi kwa muda wa miaka kui nchi itakuwa mbali

Vyama vya upinzani hawana cha kuikejeli serikali na ukuuaji wa uchumi kwa sababau wkina Mchungaji Slaa na wenzakehawana uwezo wa kujieleza au kuuzungumzia uchumi kutokana na elimu aliokuwa nayo haisadii ktk karne hii ya sayansi na technologia
Kwa majibu yako wewe ni mmojawapo wa mafisadi au unanufaika na hali iliyoko. Unasema wapinzani hawana uwezo wa kuielezea hali ya uchumi wanchi hii? Kwani unahitaji kuwa na digrii kufahamu kwamba maisha yamepanda? mmezoea kutupa takwimu feki za uchumi na kuna wakati mlisema uchumi wa nchi hii unapaa; hiyo ilikuwa yapata miaka kama mitano iliyopita, ingekuwa kweli ulikuwa unapaa kama mlivyotusadikisha hali ingekuwa bora sasa. Lakini ukweli ni kwamba kila kukicha hali ni ngumu kuliko ya jana. Sasa ni uchumi gani huo mnaosemaunakuwa? Wa wake zenu na watoto wenu wanaobadilisha magari kama nguo na kukamatwa nje waki-deposit madola? Acheni kukejeli watu maana walivyopigika wanaweza kuamua wakafie ikulu.
 
Waungwana mfumuko wa bei za vitu duniani kote wanalalamika sasa hivi. Kilichosababisha mfumuko huo ni kutokana na bei za malighafi ya mafuta toka nchi zinazozalisha kupanda juu.
Juzi nilitembelea nchi moja kati ya mataifa yaliyoendelea nikaona leo gallon moja ya petrol ni zaidi ya $3 wakati mwaka mmoja uliopita ilikuwa ni $2. Hao hawalalamiki kama wabongo.
Jamani wabongo tunalalamika mno, tusome ishara za nyakati pia.
 
ndugu katika jf, nilienda jana kununua bidhaa za kibandani kwangu bei nilizo zikuta zikanifanya ninunue bidhaa 2/3 ya kiwango nilichopanga kununua. je hali hii tutafika?
je tatizo lipo Arusha tu au na mikoa mingine?

Mkuu,
Hii hali inayoendelea ni nchini kote,kila kipembe, mkoa, mji na kijiji.
Lililo baya ni kuwa kiwango cha wagonjwa wa kisukari itazidi sana kwa sababu watu watalazimika kula vyakula vya uwanga tu zaidi. Pia utapia mlo kwa watoto na watu wazima.
Hii itapelekea watu kufa kama kuku na kuziumiza familia nyingi kiuchumi zaidi ya huu umaskini walionao leo.

wakati watawala wetu wanataka tuamini uchumi unaboreka, uhalisia wa maisha kwa wananchi wa kawaida uko tofauti, maisha yao yanazidi kudidimia na kuwa ya shida zaidi.

Katika nchi nyengine wananchi yamewashinda na wamepeleka ujumbe kwa watawala, sisi hatujafikia kiwango cha ujasiri bado. Tunakula "amani na utulivu wetu" huku tunajifea kama kuku na hata wa kutuzika hatuna.....Lakini tutafika! Lini!!???
 
mfumko wa bei umeshuka toka 13% mpaka kufikia 5.6% ni tafauti na jirni zet ambapo makwao ni avarage ya 9.5%

uchumi wetu unaenda vizuri kulinganisha na nchi nying afrika na wataalam wa uchumi wanatabiri kama tanzania itaendelea na nguvu zake za uchumi kwa muda wa miaka kui nchi itakuwa mbali

vyama vya upinzani hawana cha kuikejeli serikali na ukuuaji wa uchumi kwa sababau wkina mchungaji slaa na wenzakehawana uwezo wa kujieleza au kuuzungumzia uchumi kutokana na elimu aliokuwa nayo haisadii ktk karne hii ya sayansi na technologia

hiki sio kijiwe , zungumza mambo y msingi, kuna watu wenye fani. Usilete madudu kama huna ihakika. Hata kama ni madudu toa vidhibitisho sio nani kasema hata humjataji. Sorry.
 
Kweli hali ni mbaya sana, binafsi imenigusa jana nimeenda kununu nondo nikakuta zimepanda bei kutoka 13,500= na sasa ni 16,000=. Sijajua kama mabati nayo yamepanda bei na kama ni hivyo ujenzi sasa utakuwa mgumu sana.
 
Waungwana mfumuko wa bei za vitu duniani kote wanalalamika sasa hivi. Kilichosababisha mfumuko huo ni kutokana na bei za malighafi ya mafuta toka nchi zinazozalisha kupanda juu.
Juzi nilitembelea nchi moja kati ya mataifa yaliyoendelea nikaona leo gallon moja ya petrol ni zaidi ya $3 wakati mwaka mmoja uliopita ilikuwa ni $2. Hao hawalalamiki kama wabongo.
Jamani wabongo tunalalamika mno, tusome ishara za nyakati pia.

Mwanangu tufike mahali tujiulize Hivi haya maneno tunayolishwa kwamba haya ni matatizo ya uchumi ni ya dunia ni ya kweli? maana hata mh alisema yeye hajui sasa wewe vipi? mali asili tulizo nazo kama kweli viongozi wetu wangekuwa na maono na mawazo mapya basi nchi hii tungeishi vizuuri sana! wewe ona kuna nchi inategemea utalii na kilimo uchumi wao uko juu zaidi ya kuliko nchi hii Ya maziwa na asali tumebaki kuchonga bla bla kwa saaana kila mtu mjuaji kalaga...wayago woja!

TUMELAANIWA!
 
Waungwana mfumuko wa bei za vitu duniani kote wanalalamika sasa hivi. Kilichosababisha mfumuko huo ni kutokana na bei za malighafi ya mafuta toka nchi zinazozalisha kupanda juu.
Juzi nilitembelea nchi moja kati ya mataifa yaliyoendelea nikaona leo gallon moja ya petrol ni zaidi ya $3 wakati mwaka mmoja uliopita ilikuwa ni $2. Hao hawalalamiki kama wabongo.
Jamani wabongo tunalalamika mno, tusome ishara za nyakati pia.
Wewe Candid scope acha hizo. Kwanza kabisa wewe sio representive ya MTANZANIA halisia. Inaonekana umekulia mazingira ya AC na bado wala imported duck.(NOT HATING) Lakini mwenzetu juzi tu umetoka majuu kweli utaamini watu tuna re plan menu za majumbani kwetu. Sawa mfumuko wa bei hapa TZ unachangiwa na mfumuko wa malighafi lakini sisi waTZ tunaamini pia sera mbovu,wizi,ufisadi na rushwa za viongozi walioko sasa ndio kwa kiasi kikubwa sana unaleta ugumu huu wa maisha,so please usituletee sababu ndogo ukazifanya ndio principle causes na kutuita WAUNGWANA. Tactic hizo za kutupooza hazifanyi kazi tena. A hungry man is an angry man! Robert Nesta.
 
Huko ughaibuni wanalalamika bei ya mafuta! Posts hapo juu umeona watu wanalalamika nini? CHAKULA!! And you think it's ok,tuko sawa na watu wa huko ulaya? Tuna billions za kulipa DOWANS ila sio za kuwalipa walimu na mikopo ya wanafunzi. Tunabilions za kununua mashangingi lakini sio kusubsidize wakulima wetu na ku implement miundo mbinu ya uzalishaji au ku increase subsidies za umeme na mafuta.
 
Hapa nilipo nanasi ni sh 3500 hadi 4500. Embe 500 hadi 1000. Nyama kilo buku 4. Kodi ya nyumba laki 2. Kiwanja ambacho 2006 kili demand laki 6 sasa hivi mil 7. Bila wizi nasi tutaweza kweli?
 
Back
Top Bottom