Tanzania: Kushuka kwa thamani ya shillingi, mfumuko wa bei na siasa zetu!

Moja ya mikakati aliyotangaza Kikwete baada ya kuingia Ikulu ni kuitoa nchi mahala ilipo na kuifikisha mahali pengine! Je unajua kama ameshalitimiza hilo?

Ametutoa kutoka mchele kilo 01 Tshs 800/= hadi 2500/=, nyama kilo 01 Tshs 2500/= hadi 6000/=, kiberiti Tshs 20/= hadi 150/=, sembe Tshs 250/= hadi 1200/=, kutoka kuwa na ndege 11 za ATCL hadi ndege 1 mbovu, nauli ya daladala kutoka Tshs 150/= hadi 300/=, migomo ya vyuo vya elimu ya juu, walimu hadi madaktari, chaguzi za CCM bila rushwa hadi kutawaliwa na rushwa ile mbaya, kutoka kundi 01 ndani ya CCM hadi makundi 04 yanayopingana hivi sasa.

Hii ndiyo CCM na magamba yao, kwa uchache haya na mengineyo ndiyo yana tuweka hapa tulipo na kuendelea kulitafuna Taifa; unaweza kuongeza mengine ya kweli na ukawatumia watanzania wenzako ndani na nje ya nchi ili waweze kujipanga ili kuweza kuikomboa nchi yao ifikapo 2015.

Namba zako ulizoandika hapo hazina maana yeyote kama hutafanya comparison na kiwango cha mshahara wa wakati ule na wakati huu. Fanya hayo kwanza ndio watu waweze kujadili hoja yako tuone kama ina thamani ya kuwa hapa.
 
Kiuyahaki:
Hapo kwenye nyekundu umetumia vigezo gani? Una uhakika gani kuwa hiyo haitokani na "time value of money"? Ni miaka saba sasa imepita tangu achukue madaraka, wewe unataka purchasing power ya sh 800/= leo iwe sawa na 800/= ya miaka 7 iliyopita? Uchumi gani huo?
 
wewe mshahara wako wa enzi zile ni sh.ngapi???na sasa umeongezeka kwa sh.ngapi????
 
Pabaya zaidi ni bei ya mafuta ya taa kuwa juu ya mafuta ya dizeli!
 
Nakumbuka alisema 'TUTAZIUNGANISHA SHULE ZOTE ZA KATA KWENYE MKONGO WA TAIFA' hadi leo sijui alimaanisha nini?
 
wewe mshahara wako wa enzi zile ni sh.ngapi???na sasa umeongezeka kwa sh.ngapi????

Wakati ule nilikuwa napata kima cha chini cha serikali na hadi sasa napata kima cha chini cha serikali. Lakini pesa za wakati ule si sawa na hizi ninazopokea wakati huu.
 
Kwa wale wote walioegemea katika kujadili thread hii kiuchumi ni mtazamo wao tu;mimi nilicheza na matukio kuthibitisha hili"Moja ya mikakati aliyotangaza Kikwete baada ya kuingia Ikulu ni kuitoa nchi mahala ilipo na kuifikisha mahali pengine! Je unajua kama ameshalitimiza hilo?"
Hadi hapo nafikiri mmenisoma,haikatazwi mtu kuamua kuboresha kuliko kubomoa.
 
Kuongeza ajira....................... Vijana wanazidi kusota mtaani

on the contrary, kawahimiza wachina kuleta mapikipiki (bodaboda) na macontainer ya viungo bandia (ambavyo navyo ni feki)
 
Moja ya mikakati aliyo tangaza mh JK kwenye kampeni zake kama atachaguliwa na kuingia Ikulu,
basi ataitoa nchi mahali ilipo na kuifikisha mahali pengine penye neema akimaanisha maisha bora kwa kila raia wa Tz.
Je hivi unafaham kama ameshalitimiza hilo?
ametutoa kutoka Sukari kilo sh.600 hadi sh 2000,
mchele kilo sh.800 hadi sh.2500,
nyama kilo sh.2500 hadi sh.6000,
unga sh.250 hadi sh.1200,
petrol sh.600 hadi 2600,
kutoa kuwa na ndege za ATCL 11 hadi ndege 1.
Hii ndio CCM bwana Tumethubutu,Tumeweza na Tunazidi kusonga mbele,
kwa kasi zaidi,hali zaidi na kwa nguvu za ajabu..
CCM Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
 
Kiuyahaki:
Hapo kwenye nyekundu umetumia vigezo gani? Una uhakika gani kuwa hiyo haitokani na "time value of money"? Ni miaka saba sasa imepita tangu achukue madaraka, wewe unataka purchasing power ya sh 800/= leo iwe sawa na 800/= ya miaka 7 iliyopita? Uchumi gani huo?

Hii Forum kwakweli imeingiliwa na watu sidhani kma hata STD seven wamemaliza!

Mcsquared!

Don't waste your time !these are future Youth we have !too myopic and cynical,
It's ****!
I have been trying to engage myself on various threads here but I came to realize , you cannot learn anything from here!

Merely CARRIER CRITICS Platform!

Kibaya Zaidi ukija na mawazo positive ili ujikite kwenye objectivity!!

NiMatusi tu!
Sasa unamkosoa mtu lakini wewe unaekosoa huji na solution au alternative au hata mtazamo wako kitu kinachokufanya nawewe usiwe tofauti na unaemkosoa!

Note:
Ukikosoa Mtu usipokua na solutions au alternative tafsiri Yake wewe ni mpuuzi Zaidi ya uliemkosoa!

Tufanye tathmini Kabla ya kukosoa....
 
Kuna wakati walisema bei ya mafuta duniani na hyo walikuwa wanatumia sana propaganda hyo kwa Wa TZ wasiolewa chochote kuhusu uchumi, sasa wanakuambia hata nchi nza ulaya zipo kwnye mgogoro wa uchumi sembuse sisi kuwa na inflation 2 digits, ukiwaauliza mbona nchi za wenzetu Afrika hawakukumbana na inflation kubwa na hawakuwekeza knye matrekta kwann sisi. Inflation hujitokeza pale kukiwa hakuna mzunguko wa kutosha wa chakula na bidhaa muhimu.

Tuje knye suala la kilimo kwanza na matrekta , matrekta yale wanayouza ni kwa ajili ya wkulima wa kati.

Suala la kujitosheleza chakula tuanzie knye kaya hizi za kimasikini vijijini za kuwawezesha kutumia vitu kama walvyozungukwa navyo katika kuongeza tija knye kilimo kwa mfano wale wanaofuga wawatumie wanyamakazi kwnye kilimo na serkali kuwekeza kwnye viwanda vya usindikaji ili kuongeza thamani mazo yetu ili tuiingze fedha za kigeni nyngi na kupandisha thamani ya fedha zetu, maana uchumi wetu ni imported economy na viongozi wetu kutokuwa na uelewa wanafurahi baada ya kufanya mikakati exported iwe higher wanaona raha kuona wananchi pamoja na viongozi kuagiza hata samani nje.
 
Nashangaa bei za bidhaa zimepanda bei ila mishahara ya wafanyakazi wanaozalisha hizo bidhaa hazijapanda.

Example; Bidhaa za unga, mafuta, sabuni, n.k zimepanda bei, je hivo viwanda si vimeongeza bei za vitu, faida ni kubwa.

Je kwa nini wasiongeze mishahara sambamba na kuongezeka faida?? ama gharama za maisha
 
Mbona umeirudisha hii thread 2009,je hukuridhika na michango basi i-re-new na kuimodify ili watu wachangie.
 
Kaka Ruta hali hii kama itaendelea itawafanya watu wakimbie familia zao.
Unajua kuna wakati nilikuwa nampa wife kiasi fulani cha pesa kwa mahitaji ya ndani (chakula, umeme n'k) ambacho kilitosha mwezi mzima.
Ghafla hela ikawa haitoshi nikafikiri sasa wife kaamua kumjengea babake kibanda, RealMan nikajitosa sokoni mwenyewe. Pressure ikawa inapanda na kushuka kwa kila bidhaa niliyouliza bei. Tuko hapa tulipo kwa sababu tumechagua kuwa hapa na inabidi tuendelee kuwa wavumilivu.

Takwimu za Ndulu ni zakuwafurahisha watawala na wafadhili ndio maana akatunukiwa Gavana bora Africa (kama sikosei). Wanasema inflation has gone down to single digit wakati bei ya chakula imepanda twice as much ilivyokuwa 5yrs back.
Tatizo watanzania hawajatambua siasa inahusika na maisha yao ya kila siku

pindi tukilijua hilo basi ccm lazima iondoke madarakani. Utasikia mtu anasema mimi sina mpango na siasa harafu kesho ananunua sukari kilo mia tano ,kesho kutwa analala na njaa anabaki kulalamika
 
Solution za mambo haya mimi naamini hizi:-
  1. Tumlazimishe bwana mkubwa kukaa ofisini muda mrefu badala ya yeye kutwa kucha kuwaza safari, hii itawafanya watu wake wa muhimu kama wachumi na wale watu wa mipango kufanya kazi, Watanzania wengi/hasa wanasiasa wa magamba hawapendi kufanya kazi bila supervision, so mkuu akiwa safari tu na wao wanaanza kusoma magazeti na wengine kufikiria namna ya kupiga deals then hakuna kinacho fanyika.
  2. Wafanya biashara wakubwa wabanwe na walipe kodi stahiki, kodi nyingi kwenye makampuni makubwa utakuta zinalipwa na wafanyakazi yaani PAYE na wale waagizaji wa bidhaa nje ya nchi utakuta sehemu kubwa wanalipa VAT tu ambayo kimsingi mlipaji wa VAT hua ni mteja wa mwisho kabisa.
  3. Serikali itengeneze utaratibu utakao wabana wafanya biashara kuaigiza vitu ambavyo Locally vinapatikana, maziwa toka Africa kusini, Colgate Sabuni sijui na nini, nadhani pia hata samani za maofisini, binafsi bado napa shida kuona tunagiza China while Keko pale vijana wanatoa hadi Soffa za ukweli, mambo haya ndio yanayodidimiza uchumi wetu.
  4. Kwa upande mwingine, kunahitajika elimu ya ziada kwetu Watanzania, Wabongo wengi utafikiri tumerogwa, yaani tunapenda vit vya nje ya nchi sijui hata ni kwanini, kabla sijaoa, ukweli nilikua sijui tofauti kati ya Kanga na Kitenge (Sitanii, niko serious) mara baada ya kuoa ndio nilipojua tofauti, kichekesho ni hiki, wakati huo Kiwanda cha Urafiki kilikua kinafanya kazi, nilikua nashangaa sana akina mama wengi walikua wakipenda Kanga toka India na Kenya, lakini kwa makini nilikua naona Kanga za Urafiki zilizidi kwa Ubora mbali sana ya hzi zingine. Hapa ni kuanzia viongozi wetu na sisi wananchi, tupende vitu vya ndani, hapa pia ndipo Wakenya wengi wanapotupiga bao, wanpenda sana vya kwao, utakuta Mkenya yupo Tanzania halafu anauliza hivi, huo Mkate ni wa Kenya?
  5. Wale watu wa Board ya Biashara ya nje (sina hakika kama hii kitu ipo hadi leo) watafute masoko ya bidhaa zetu na sio kwenda tu ofisini doing nothing.
  6. Nadhani pia Viongozi wetu tuanze kuwapa kitu kinaitwa KPI (Key Performance indicator) kama hufikii malengo uliopewa na yale uliojiwekea then aidha uachie ofisi au uachishwe kazi, vinginevyo tutaendelea kulalamika na kuwa mashahidi wa wenzetu tu kama Rwanda, leo wanaleta Ndege hadi kwetu na wana destination zaidi ya 14 nje ya nchi while sisi ATC, shirika kongwe Africa lina Destination moja tu, Mwanza-Dar, tena mara baada ya Mwakyembe kuja.
 
Kuongeza mishahara ni kucreate inflation. Ushauri wangu ni kwamba bunge la February JK apigiwe kura ya NO CONFIDENCE kwa kutuingiza kwenye lindi hili la umaskini
 
Back
Top Bottom