Tanzania katika mtanziko; Hakuna umeme, sukari wala dola. Serikali inachukua hatua gani?

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,696
40,963
Tanzania hakuna umeme, sukari wala dola.

Huku tukiambiwa kuwa awamu hii uchumi unakua kuliko awamu yoyote ile, makusanyo ya TRA yakivunja rekodi.

Tatizo la umeme nalo limekua sugu bila kupata ufumbuzi wa kudumu na hali ikizidi kuwa mbaya kila siku.

Sukari nayo kila mtu anauza anavyojisikia.

Uhaba wa dola nao ukishika kasi.

Kama kweli uchumi unakua, itakua ajabu kama dola zitaadimika.

Maana factor moja wapo ya kukua kwa uchumi ni ongezeko la mauzo ya nje , na mauzo ya nje ni fedha za kigeni. Dola inaadimikaje.

Kukua kwa uchumi means ongezeko la uzalishaji.

Uzalishaji unaongezekaje kama hakuna nishati ya uhakika??

Kukua kwa uchumi means bei ya bidhaa kuwa stable, huu uchumi wa kukamiana kwa bei za bidhaa ni kwa baadhi ya wafanyabiashara tu sio wananchi.

Viongozi wetu hatuwaoni wakijihusisha na mambo haya.

Serikali ina mpango gani kuaddress hizi issues.??
 
IMG-20240218-WA0152.jpg
 
Back
Top Bottom