Tetesi: Tanzania inalipwa mabilioni ya fedha toka nje ambazo zimefanywa siri na serikali hazina rekodi, tumenunulia ndege, na kujenga SGR na Stiegler nk

"Lakini sasa kukawa na tatizo. Ikiwa Tanzania ingeruhusiwa kuchimba hii Helium na kuuza, basi ingeuza kwa bei poa kiasi kwamba ingeua kabisa uzalishaji wa hivi viwanda 14, USA akiwa mzalishaji mkubwa. Basi inaonekana kulikuwa na makubaliano kwamba Tanzania icheleweshe uzalishaji wa Helium hadi wakati unaokubalika. Lakini kwa kufanya hivyo, lazima kulikuwa na makubaliano kwamba Tanzaia ilipwe fedha nyingi kama "compensation" ya kuzuia uzalishaji wa Helium ili kunusuru kampuni zinazouza Helium kwa sasa. Hiyo ndiyo fedha inayofanya miradi yenu ambayo wanasiasa wenu wanawaambia eti ni kodi za wananchi ili kuji-promote kisiasa. Habari ya ugunduzi wa Heluim Tanzania na umuhimu wa hii gesi katika soko la dunia, ilipaswa kuwa kubwa kuliko kama Tanzania ingegundua mafuta. Sasa jiulize, kwa nini wanasiasa wenu wamekaa kimya kuhusu huu ugunduzi mkubwa uliofanyika Tanzania? Tanzania ni nchi pekee duniani unapata Helium ardhini na utatawala soko la dunia kama ilivyo kwa Tanzanite, na mnakaa kimya, kwa nini?"
Kwa vile umeanza na tetesi, then prove!.
Mimi kwa upande wangu, naiona hii story yako to be too good to be true!.
Taarifa ya TRA from time to time, inaonyesha makusanyo yote ya kodi na mapato mengine yote yanawekwa mfuko mkuu hazina, bajeti yote ya serikali inapelekwa bungeni na CAG anafanya ukaguzi. Hakuna hata maramoja Tanzania tumewahi kuwa na budget self sufficient, kila siku tunatengeneza bajeti tegemezi kwa mikopo, grants na misaada, hivyo ingekuwa ni kweli kuna haya malipo ya siri to that extent, tungeona na tusingekuwa tunakopa hivi tunavyokopa!.
Anyway, asante for food for thought kuhusu helium.
P
 
Kwa vile umeanza na tetesi, then prove!.
Mimi kwa upande wangu, naiona hii story yako to be too good to be true!.
Taarifa ya TRA from time to time, inaonyesha makusanyo yote ya kodi na mapato mengine yote yanawekwa mfuko mkuu hazina, bajeti yote ya serikali inapelekwa bungeni na CAG anafanya ukaguzi. Hakuna hata maramoja Tanzania tumewahi kuwa na budget self sufficient, kila siku tunatengeneza bajeti tegemezi kwa mikopo, grants na misaada, hivyo ingekuwa ni kweli kuna haya malipo ya siri to that extent, tungeona na tusingekuwa tunakopa hivi tunavyokopa!.
Anyway, asante for food for thought kuhusu helium.
P
Mkuu Paskali

Hata katika fraternity ya sheria, kuna kitu kinaitwa circumstantial evidence, kwa hiyo tetesi ambazo zinatoa circumstantial evidence kuna kipindi zinakubalika, albeit kama fuel for further investigations. As a lawyer, unapaswa kuelewa hilo.

Na wewe ndio journalist sio mimi. The onus to prove is on you. Kwa hiyo mimi nilidhani ungeanza angalau kutaka kujua kwa hii kampuni ya Helium iliyopo Tanzania, ni nini kimezuia ku-develop hizi discoveries za deposits za Helium kwa muda wote huu tangu walipozigundua? Hadi sasa wapo katika stage gani ya project development kuelekea kwenye Helium production?

You missed something katika maelezo ya thread - in fact kichwa cha thread. Thread inasema malipo yanayofanywa siri, na wewe unasema hakuna rekodi. Sasa kama kungekuwa na rekodi malipo hayo yangesemwaje yanafanywa siri? Did you think of that?

Sikiliza. Katika biashara hizi za kimataifa, kuna malipo huwa yanafanywa siri na huwa hayaingii katika rekodi za serikali. Kwa mfano, leo hii ukienda Angola au Nigeria, nchi zenye kuzalisha mafuta, ukawauliza, nionyesheni malipo yenu ya signature bonus katika mikataba ya kuchimba mafuta, hutapewa rekodi yeyote ya hayo malipo. NI malipo halali kutoka kampuni inayochimba mafuta, lakini wataweka hizo fedha pale wanapoambiwa waziweke na serikali wanakochimba mafuta. Serikali zao hazina msingi wa kuwatuhumu kuwa malipo ya signature bonus ni rushwa. Hayo ndio malipo ambayo kina Sani Abacha wanaliweza kuwa na mabilioni ya dola kwenye Swiss acounts

Sasa usifikirie kwamba hilo haliwezekani kwa Tanzania. Kwa mfano, naweza kujifanya raisi mzalendo namba 1 wa Tanzania, na kwa kuwa unataka malipo kwa nchi yetu ili tusichimbe Helium yawe siri, basi nitakuambia yanapaswa pia kufanywa kwa siri, kwenye account nje ya Tanzania. Na naweza kuwa na nia nzuri tu, kwamba fedha hizo nitazitumia kwa manufaa ya maendeleo ya nchi yangu, na labda chama changu cha siasa. Kwa hiyo nikitaka kununua Dreamliner, sina haja ya kutuma hela Boeing kutoka Tanzania, bali kutoka kwenye hiyo account iliyoko Swiss. Naweza hata kumfanya Vice president wangu signatory wa hiyo akaunti, kuonyesha sina nia mbaya na pia kujilinda dhidi ya shutuma za ufisadi ikija kujulikana.

Umewahi kujiuliza kwa mfano, ikiwa ripoti za CAG zilionyesha manunuzi ya vitu kama Dreamliner ambayo yalifanywa kwa cash bila bajeti ya Bunge? Nani alitoa hiyo cash, BoT? Umewahi kujiuliza raisi anawezaje kumpigia simu mkurugenzi wa TANROADS na kusema barabara fulani utaiweka lami, fedha nitakupa, usiwe na wasiwasi?

Lakini pengine pia, ni suala la kufikirisha tu. Ikiwa mimi kama raisi mzalendo nilikua na chanzo cha fedha nje ya nchi ambazo nilizitumia kizalendo, nani atakuwa na access ya hizo fedha ikiwa ninakufa ghafla?

You wanted foof for thought, I have given you more than that, desert included.
 
Back
Top Bottom